The chat will start when you send the first message.
1Akaita kwa sauti kuu masikioni mwangu kwamba: Mapatilizo ya mji huu yamekaribia; kila mtu na ashike mkononi mwake chombo chake cha kuangamizia!
2Nikaona watu sita, waliotokea katika njia ya lango la juu lililoelekea kaskazini, kila mtu alikuwa ameshika mkononi mwake chombo chake cha kupondea; lakini mtu mmoja aliyekuwa katikati yao alikuwa amevaa vazi la ukonge, napo kiunoni pake alikuwa na kichupa cha wino cha mwandishi, wakaja, wakasimama kando ya meza ya shaba ya kutambikia.[#Ez. 10:2; Dan. 10:5.]
3Ndipo, utukufu wa Mungu wa Isiraeli ulipoondoka kwenye Kerubi, ulikokuwa, ukaja kwenye kizingiti cha mlango wa hiyo nyumba, akamgutia yule mtu aliyevaa vazi la ukonge, aliyekuwa na kichupa cha wino cha mwandishi kiunoni pake.[#Ez. 1:4-28.]
4Bwana akamwambia: Pitia humu mjini katikati, humu Yerusalemu katikati, uwaandike kichoro mapajini wale watu wapigao kite na kuyaugulia hayo machukizo yote yafanyikayo humu mjini![#2 Petr. 2:8; Ufu. 7:3.]
5Wale wengine akawaambia masikioni pangu: Piteni humu mjini nyuma yake, kapigeni! Macho yenu yasiwaonee uchungu, wala msiwahurumie!
6Wazee, wasichana, wavulana, watoto, wanawake, waueni wote pia, waangamie! Lakini kila mtu mwenye kichoro msimguse kabisa! Anzieni hapa Patakatiu pangu! Wakawanzia wale wazee waliokuwa mbele ya hiyo Nyumba.[#Yer. 25:29; 1 Petr. 4:17.]
7Kisha akawwambia: itieni Nyumba hii uchafu, nkizijaza nyua zake mizoga yao waliouawa! Kisha tokeni! Basi, wakatoka humo, wakawapiga mjini namo.
8Ikawa walipokwenda kuwapiga watu vivyo, hivyo, mimi nikasalia hapo peke yangu; ndipo, nilipoanguka kifudifudi, nikalia nikisema: E Bwana Mungu, wewe utayaangamiza masao yote ya Isiraeli, ukiumwagia Yerusalemu makali yako yenye moto?[#Ez. 11:13.]
9Akaniambia: Manza za mlango wa Isiraeli na wa Yuda ni kubwa sanasana, nchi hii imeenezwa damu, walizozimwaga, mji huu nao ikajaa mapotovu, kwani husema: Bwana ameondoka katika nchi hii, hakuna Bwana anayeyaona.[#Ez. 8:12.]
10Basi, mimi nami jicho langu halitawaonea uchungu, wala mimi sitawahurumia, nitawapatilizia njia zao vichwani pao.
11Kisha nikamwona yule mtu aliyevaa nguo ya ukonge aliyekuwa na kichupa cha wino kiunoni pake, akileta majibu kwamba: Nimefanya, kama ulivyoniagiza.