The chat will start when you send the first message.
1Katika mwaka wa kwanza wa Kiro, mfalme wa Wapersia, ndipo, lilipotimia neno la Bwana, alilolisema kinywani mwa Yeremia, maana Bwana akaiamsha roho yake Kiro, mfalme wa Wapersia, akatangaza mbiu katika ufalme wake wote kwa vinywa vya watu na kwa barua kwamba:[#2 Mambo 36:22-23; Yer. 25:11; 29:10.]
2Hivi ndivyo, anavyosema Kiro, mfalme wa Wapersia: Ufalme wote wa nchi hii amenipa Bwana Mungu wa mbinguni, naye mwenyewe akaniagiza kumjengea Nyumba kule Yerusalemu katika nchi ya Yuda.[#Yes. 44:28; 45:1.]
3Ye yote wa kwenu aliye wa ukoo wake Mungu wake awe naye, na apande kwenda Yerusalemu katika nchi ya Yuda kuijenga Nyumba ya Bwana Mungu wa Isiraeli. Yeye akaaye Yerusalemu ni Mungu.
4Tena kila atakayesalia mahali po pote, anapokaa ugenini, watu wa mahali pale sharti wamsaidie kwa kumpa fedha na dhahabu na vyombo na nyama wa kufuga pamoja na vipaji vingine, wanavyovitaka wenyewe vya kuitolea Nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu.
5Ndipo, wao waliokuwa vichwa vya milango ya Yuda na ya Benyamini pamoja na watambikaji na Walawi walioamshwa roho zao na Mungu wakaondoka kwenda kuijenga Nyumba ya Bwana iliyoko Yerusalemu.
6Nao waliokaa na kuwazunguka wakaitia mikono yao nguvu kwa kuwapa fedha na dhahabu na vyombo na nyama wa kufuga na vitu vyenye kima, tena vipaji vyote, walivyovitoa wenyewe vya tambiko.
7Naye mfalme Kiro akavitoa vyombo vyote vya Nyumba ya Bwana, Nebukadinesari alivyovitoa Yerusalemu na kuvitia jumbani mwake.
8Hivyo Kiro, mfalme wa Wapersia, akavitoa na kuvitia mikononi mwa mtunza malimbiko Mitiridati, naye akavihesabu alipompa Sesebasari, mkuu wa Wayuda.[#Ezr. 2:2,63; 5:14.]
9Hii ndiyo hesabu yao: sinia za dhahabu 30, sinia za fedha 1000, visu 29;
10vinyweo vya dhahabu 30, vinyweo vya fedha vya namna ya pili 410, vyombo vingine 1000.
11Vyombo vyote vya dhahabu na vya fedha vilikuwa 5400. Hivi vyote Sesebasari alikwenda navyo, wale waliotekwa na kuhamishwa walipotoka Babeli kwenda kupanda Yerusalemu.