Ezera 10

Ezera 10

Wanawake wa kimizimu wanatengwa nao Waisiraeli.

1Ezera alipoomba na kuungama hivyo akilia na kujiangusha chini mbele ya Nyumba ya Mungu, ndipo, walipokusanyika kwake Waisiraeli, ukawa mkutano mkubwa mno, waume na wake na wana, nao hao watu wakalia kilio kikubwa.

2Kisha akasema Sekania, mwana wa Yehieli, wa wana wa Elamu, akamwambia Ezera: Sisi tumemvunjia Mungu maagano kwa kuoa wanawake wageni wa makabila ya nchi hizi; lakini tena kiko kingojeo, Waisiraeli walicho nacho kwa ajili ya jambo hili.

3Sasa tufanye agano na Mungu wetu, tuwatoe hao wanawake pamoja na wana waliozaliwa nao kwa shauri lako, bwana wangu, na kwa shauri lao wanaoyaogopa maagizo ya Mungu wetu, kisha na yafanywe, kama Maonyo yanavyoyataka.

4Inuka! Kwani jambo hili linakupasa wewe, sisi nasi tutakuwa upande wako; jipe moyo, uyafanye!

5Ndipo, Ezera alipoinuka, akawaapisha wakuu wa watambikaji nao wa Walawi na watu wote wa Isiraeli kufanya hivyo, nao wakaapa.

6Kisha Ezera akaondoka hapo mbele ya Nyumba ya Mungu, akaingia chumbani mwa Yohana, mwana wa Eliasibu; alipofika humo, hakula chakula, wala hakunywa maji, kwani alikuwa amesikitika kwa hilo kosa lao waliorudi kwenye kutekwa, kwani waliyavunja maagano.

7Kisha wakapiga mbiu katika nchi ya Yuda namo Yerusalemu kwamba: Wote waliorudi kwenye kutekwa wakusanyike Yerusalemu!

8Kila asiyekuja katika muda wa siku tatu kwa shauri hili lao wakuu na wazee, basi, mali zake zote zitatiwa mwiko wa kuwa mali ya mtu, naye mwenyewe atatengwa katika mkutano wao waliorudi kwenye kutekwa.

9Ndipo, walipokusanyika Yerusalemu waume wote wa Yuda na wa Benyamini katika muda wa siku tatu, ikawa siku ya ishirini ya mwezi wa tisa. Watu wote wakakaa uwanjani penye Nyumba ya Mungu, wakatetemeka kwa ajili ya jambo hilo, tena kwa kunyewa na mvua nyingi.

10Hapo mtambikaji Ezera akaondokea, akawaambia: Mmevunja maagano mlipooa wanawake wageni, mkaziongeza manza za Waisiraeli.

11Sasa mwungamieni Bwana Mungu wa baba zenu! Kisha mfanye yampendezayo, mkijitenga na makabila ya nchi hii, mkijitenga nao wanawake wageni.

12Mkutano wote pia wakamwitikia na kupaza sauti sana kwamba: kweli inatupasa kuyafanya, uliyoyasema;

13Lakini watu ni wengi, tena sasa ni masika, watu wasiweze kusimama nje, nayo kazi hii si ya siku moja au mbili, kwani tumezidisha kufanya maovu katika jambo hili.

14Wakuu wetu na waondokee kuupigia mkutano wote shauri hili, kisha wote waliooa wanawake wageni mijini mwetu na waje siku zitakazowekwa; tena pamoja nao na waje hata wazee na waamuzi wa kila mji, mpaka watakapoyatuliza makali hayo ya Mungu wetu yawakayo moto kwa ajili ya jambo hili, yakatuacha.

15Waliovibishia hivi walikuwa Yonatani tu, mwana wa Asaheli, na Yahazia, mwana wa Tikwa, naye Mesulamu na Mlawi Sabutai wakawasaidia.

16Lakini wao wengine waliorudi kwenye kutekwa wakafanya hivyo; wakachaguliwa mtambikaji Ezera na wakuu wa milango ya baba zao, nao wote wakaandikwa majina. Kisha siku ya kwanza ya mwezi wa kumi wakaja kukaa pamoja, walichunguze jambo hili,

17wakayamaliza mashauri haya ya watu wote waliooa wanawake wageni mpaka siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza.

18Kwao wana wa watambikaji waliooneka, ya kuwa walioa wanawake wageni, ndio hawa: kwa wana wa Yesua, mwana wa Yosadaki, na kwa ndugu zake: Masea na Eliezeri na Yaribu na Gedalia.[#Ez. 3:2; 9:2.]

19Hawa wakaapa na kupeana mikono, ya kuwa watawaondoa wake zao, tena kwa manza zao, walizozikora, wakatoa dume la kondoo kuwa ng'ombe yao ya tambiko ya upozi.

20Nako kwa wana wa Imeri: Hanani na zebadia.

21Nako kwa wana wa Harimu: Masea na Elia na Semaya na Yehieli na Uzia.

22Nako kwa wana wa Pashuri: Eliyoenai, Masea, Isimaeli, Netaneli, Yozabadi na Elasa.

23Tena kwa Walawi: Yozabadi na Simei na Kelaya aitwaye Kelita, Petaya, Yuda na Eliezeri.

24Nako kwa waimbaji: Eliasibu; nako kwa walinda malango: Salumu na Telemu na Uri.

25Nako kwa Waisiraeli wengine: kwa wana wa Parosi: Ramia na Izia na Malkia na Miyamini na Elazari na Malkia na Benaya.

26Nako kwa wana wa Elamu: Matania, Zakaria na Yehieli na Abudi na Yeremoti na Elia.

27Nako kwa wana wa Zatu: Eliyoenai, Eliasibu, Matania na Yeremoti na Zabadi na Aziza.

28Nako kwa wana wa Bebai: Yohana, Hanania, Zabai, Atilai.

29Nako kwa wana wa Bani: Mesulamu, Maluki na Adaya, Yasubu na Sali, Yeremoti.

30Nako kwa wana wa Pahati-Moabu: Adina na Kelali, Benaya, Masea, Matania, Besaleli na Binui na Manase.

31Nako kwa wana wa Harimu: Eliezeri, Isia, Malkia, Semaya, Simeoni,

32Benyamini, Maluki, Semaria.

33Kwa wana wa Hasumu: Matinai, Matata, Zabadi, Elifeleti, Yeremai, Manase, Simei.

34Kwa wana wa Bani: Madai, Amuramu na Ueli,

35Benaya, Bedia, Keluhi,

36Wania, Meremoti, Eliasibu,

37Matania, Matinai na Yasai,

38na Bani na Binui, Simei,

39na Selemia na Natani na Adaya,

40Makinadebai, Sasai, Sarai,

41Azareli na Selemia, Semaria,

42Salumu, Amaria, Yosefu.

43Kwa wana wa Nebo: Yieli, Matitia, Zabadi, Zebina, Yadai na Yoeli na Benaya.

44Hawa wote walikuwa wamechukua wanawake wageni, namo mwao hao walikuwamo wanawake waliozaa watoto.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania