Ezera 2

Ezera 2

Wayuda waliorudi Yerusalemu.

(Taz. Neh. 7:5-73.)

1Hawa ndio wana wa lile jimbo waliotoka katika kifungo cha kuhamishwa, aliowateka Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, na kuwahamisha kwenda Babeli, wakapanda kurudi Yerusalemu na Yuda, kile mtu mjini kwake.

2Waliokuja na Zerubabeli ndio: Yesua, Nehemia, Seraya, Relaya, Mordekai, Bilsani, Misipari, Bigwai, Rehumu, Baana. Hesabu ya waume wa ukoo wa Isiraeli ni hii:[#Ezr. 1:8; 2:63.]

3wana wa Parosi 2172;

4wana wa Sefatia 372;

5wana wa Ara 775;

6wana wa Pahati-Moabu, ndio wana wa Yesua na wa Yoabu 2812;

7wana wa Elamu 1254;

8wana wa Zatu 945;

9wana wa Zakai 760;

10wana wa Bani 642;

11wana wa Bebai 623;

12wana wa Azgadi 1222;

13wana wa Adonikamu 666;

14wana wa Bigwai 2056;

15wana wa Adini 454;

16wana wa Ateri walio wa Hizikia 98;

17wana wa Besai 323;

18wana wa Yora 112;

19wana wa Hasumu 223;

20wana wa Gibari 95;

21wana wa Beti-Lehemu 123;

22waume wa Netofa 56;

23waume wa Anatoti 128;

24wana wa Azimaweti 42;

25wana wa Kiriati-Arimu, wa Kefira na wa Beroti 743;

26wana wa Rama na wa Geba 621;

27waume wa Mikimasi 122;

28waume wa Beteli na wa Ai 223;

29wana wa Nebo 52;

30wana wa Magibisi 156;

31wana wa Elamu wa pili 1254;

32wana wa Harimu 320;

33wana wa Lodi na wa Hadidi na wa Ono 725;

34wana wa Yeriko 345;

35wana wa Senaa 3630.

36Watambikaji walikuwa hawa: wana wa Yedaya wa mlango wa Yesua 973;

37wana wa Imeri 1052;

38wana wa Pashuri 1247;

39wana wa Harimu 1017.

40Walawi walikuwa hawa: wana wa Yesua na wa Kadimieli walio wa wana wa Hodawia 74.[#Neh. 12:8.]

41Waimbaji walikuwa wana wa Asafu 128.

42Wana wa walinda malango walikuwa wana wa Salumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni, wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Sobai, wote pamoja walikuwa 139.

43Watumishi wa Nyumbani mwa Mungu walikuwa hawa: wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaoti,[#Ezr. 8:20.]

44wana wa Kerosi, wana wa Siaha, wana wa Padoni,

45wana wa Lebana, wana wa Hagaba, wana wa Akubu

46wana wa Hagabu, wana wa Samulai, wana wa Hanani,

47wana wa Gideli, wana wa Gahari, wana wa Raya,

48wana wa Resini, wana wa Nekoda, wana wa Gezamu,

49wana wa Uza, wana wa Pasea, wana wa Besai,

50wana wa Asina, wana wa Munimu, wana wa Nefisimu,

51wana wa Bakibuki, wana wa Hakufa, wana wa Harihuri,

52wana wa Basiluti, wana wa Mehida, wana wa Harsa,

53wana wa Barkosi, wana wa Sisera, wana wa Tema,

54wana wa Nesia na wana wa Hatifa.

55Wana wa watumwa wa Salomo walikuwa hawa: wana wa Sotai, wana wa Sofereti, wana wa Peruda,[#1 Fal. 9:21.]

56wana wa Yala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli,

57wana wa Sefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokereti-Hasebaimu, wana wa Ami.

58Watumishi wa Nyumbani mwa Mungu na wana wa watumwa wa salomo wote pamoja walikuwa 392.

59Nao hawa ndio waliopanda toka Teli-Mela na Teli-Harsa na Kerubu-Adani na Imeri, lakini hawakuweza kuijulisha milango ya baba zao, wala vizazi vyao, kama ndio Waisiraeli:

60wana wa Delaya, wana wa Tobia, wana wa Nekoda; nao walikuwa watu 652.

61Tena kwao watambikaji: wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai aliyechukua mmoja wao binti Barzilai wa Gileadi, awe mkewe, kwa hiyo aliitwa kwa jina lao.[#2 Sam. 19:31.]

62Hawa walikitafuta kitabu chao cha udugu wao, lakini hawakukiona, kwa hiyo wakakatazwa utambikaji.

63Mtawala nchi akawaambia: Msile kabisa vyakula vitokavyo Patakatifu Penyewe, mpaka atakapoondokea mtambikaji mwenye Urimu na Tumimu (Mwanga na Kweli).[#Ezr. 2:2; 2 Mose 28:30.]

64Huo mkutano wote pamoja walikuwa watu 42360,

65pasipo watumwa na vijakazi wao, nao walikuwa 7337; tena walikuwako waimbaji wa kiume na wa kike 200.

66Farasi wao walikuwa 736, nyumbu wao 245,

67ngamia wao 435, tena punda 6720.

68Walipofika penye Nyumba ya Bwana iliyokuwamo Yerusalemu, ndipo, wakuu wa milango walipoitolea wenyewe Nyumba ya Mungu vipaji vya kuijengea tena mahali hapo, ilipokuwa.

69Kwa hiyo, walivyoweza, wakatoa vipaji vyao, wakavitia katika kilimbiko cha jengo: vipande vya dhahabu vilivyoitwa Dariko 61000, ndio shilingi kama milioni mbili na 440000 na vipande vya fedha vilivyoitwa Mane 5000, ndio shilingi kama milioni, na mavazi ya watambikaji 100.

70Kisha watambikaji na Walawi, nao watu wengine na waimbaji na walinda malango nao watumishi wa Nyumbani mwa Mungu wakakaa katika miji yao, nao Waisiraeli wote wakakaa katika miji yao.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania