The chat will start when you send the first message.
1Mimi Paulo ni mtume, lakini sikutumwa na watu wala kwa agizo la mtu, ila nimetumwa kwa agizo lake Yesu Kristo nalo lake Mungu Baba aliyemfufua katika wafu.[#Gal. 1:11-12.]
2Mimi pamoja na ndugu wote walio pamoja nami tunawaandikia ninyi wateule wa Galatia.
3Upole uwakalie na utengemano unaotoka kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo![#Rom. 1:7.]
4Ndiye aliyejitoa kwa ajili ya makosa yetu, apate kutuokoa katika dunia hii mbaya ya sasa. Ndivyo, Mungu, Baba yetu, alivyotaka.[#Gal. 2:20; 1 Tim. 2:6; Tit. 2:14; 1 Yoh. 5:19.]
5Huyu atukuzwe kale na kale pasipo mwisho! Amin.
6Nastaajabu, ya kuwa mwageuzwa upesi hivyo, mwondoke kwake yeye aliyewaita, mgawiwe kipaji chake Kristo, mkafuata utume mwema mwingine.
7Tena hakuna utume mwema mwingine, ila wako watu tu wanaowahangaisha; ndio wanaotaka kuugeuza Utume mwema wa Kristo.[#Tume. 15:1,24.]
8Lakini ikiwa sisi, au ijapo malaika wa mbinguni, akiwatangazia utume mwema mwingine kuliko ule, tuliowapigia sisi, na awe ameapizwa![#1 Kor. 16:22.]
9Tuliyoyasema sasa hivi, narudia kuyasema tena: Mtu akiwatangazia utume mwema mwingine kuliko ule, mlioupokea, na awe ameapizwa!
10Je? Hayo nayasemea kuitikiwa nao watu au naye Mungu? Au je? Natafuta kuwapendeza watu? Kama ningependeza watu bado, basi, singekuwa mtumwa wake Kristo.[#1 Tes. 2:4.]
11Ndugu zangu, nawatambulisha, ya kuwa Utume mwema uliotangazwa nami sio wa kimtu.
12Kwani nami sikuupokea kwa mtu, wala sikufundishwa, ila nimefunuliwa na Yesu Kristo.[#Tume. 9:1-15.]
13Kwani mmesikia, nilivyoendelea hapo, nilipolifuata tambiko la Kiyuda, ya kuwa nalijipingia kuwafukuza wateule wa Mungu na kuwajengua.[#Tume. 26:4-20.]
14Nami hapo, nilipolifuata tambiko la Kiyuda, nikapita wenzangu wengi, ambao tulizaliwa nao mwaka mmoja, maana nilikaza kujihimiza, niandamane nayo, tuliyoyapokea kwa baba zetu.
15Lakini Mungu alikuwa amenitenga hapo, nilipokuwa tumboni mwa mama yangu, akaniita, nigawiwe kipaji chake.[#Yer. 1:5; Rom. 1:1.]
16Hapo, alipopendezwa kumfunua Mwana wake moyoni mwangu, kusudi nije, niwapigie wamizimu hiyo mbiu yake njema, papo hapo nikakata mawazo pasipo kuuliza mwili wangu ulio wenye nyama na damu,[#Gal. 2:7; Mat. 16:17.]
17wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwao waliokuwa mitume mbele yangu, ila nalikwenda Arabuni, kisha nikarudi tena Damasko.
18Miaka mitatu ilipokwisha kupita, nikapanda kwenda Yerusalemu, nijuane na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano.[#Tume. 9:26.]
19Lakini hakuna mtume mwingine, niliyemwona, asipokuwa Yakobo, nduguye Bwana.
20Lakini haya, ninayowaandikia, tazameni, Mungu anayajua, ya kuwa sisemi uwongo.
21Kisha nikafika upande wa Ushami na Kilikia.[#Tume. 9:30.]
22Nami nilikuwa sijajulikana uso kwa uso nao wateule wake Kristo walioko Yudea.
23Ila walikuwa wamesikia tu: Yule aliyetufukuza kwanza sasa huipiga hiyo mbiu njema ya kumtegemea Bwana, alikokuwa amekujengua. Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.