The chat will start when you send the first message.
1Bwana, nimeusikia utume wako, nikaogopa.
Bwana, itokeze kazi yako, iwepo katika miaka ijayo!
2Ijulishe katika miaka ijayo!
Ukikasirika zikumbuke
huruma! (Kituo.)
3Mungu alikuja toka Temani, Mtakatifu alitoka mlimani
kwa Parani.
Utukufu wake huzifunika mbingu, nchi hii nayo hujaa
matukuzo yake.
4Huangaza kama mwanga wa jua,
miali hutoka mkononi mwake;
ndimo, nguvu zake zifichikamo.
5Magonjwa yauayo humtangulia,
nazo homa kali huifuata miguu yake.
6Anaposimama ndipo, anapoitetemesha nchi;
anapochungulia ndipo, anapoyastusha mataifa.
Milima iliyoko toka kale huatuka,
vilima vilivyoko kale na kale huangukiana chini;
ni vilevile, alivyovikanyaga juu tangu kale alipopita.
7Vijumba vya Wanubi niliviona vyenye shida,
nayo mahema ya nchi ya Midiani yakatikisika.
8Je? Bwana anaikasirikia mito?
Makali yako yataitokea mito?
Je? Machafuko yako yanaiendea bahari?
Kwa kuwa unavutwa na farasi katika gari lako lishindalo!
9Uta wako umefunuliwa, utokee waziwazi,
kama ulivyoziapia koo za watu kwa neno lako (Kituo.)
Unapoipasua nchi, hapo hutokea majito.
10Ukioneka, milima hustuka, nayo
mafuriko ya maji huzidi,
vilindi vya baharini huvuma na kuikweza mikono yao juu.
11Jua na mwezi husimama kwao, mishale yako ikija kumulika,
nao umeme wa mkuki wako ukimetameta.
12Kwa kukasirika unaikanyaga nchi,
kwa kuchafuka unayaponda mataifa.
13Umetokea kuwaokoa walio ukoo wako,
upate kumwokoa uliyempaka mafuta,
ukaviponda vichwa vyao wasiokucha nyumbani mwao,
ukazibomoa toka misingi hata vipaani. (kituo.)
14Kwa mikuki yao unavichoma vichwa vya vikosi vyao
vijavyo mbio kama kimbunga kunikimbiza mimi
na kunizomea kama watu wanaotaka kula mnyonge fichoni pake.
15Lakini wewe ukaja na kuikanyaga bahari
ukipanda farasi wako, ijapo maji mengi yavume.
16Nilipoyasikia, ndipo, tumbo langu lilipotetemeka,
midomo yangu nayo ikajipigapiga kwa uvumi wao,
ugonjwa wa ubovu ukaingia mifupani mwangu,
nikatetemeka wote hata chini, niliposimama,
kwa sababu sina budi kuingoja siku ya kusongwa,
itakapolipata lile kabila lililokuja kutushambulia.
17Kwani mkuyu hauchanui, wala mizabibu haizai,
vichipukizi vya mchekele navyo hudanganya,
mashamba ya ngano hayaleti chakula,
kondoo wametoweka mazizini kwao,
hata ng'ombe hamna vibandani mwao.
18Lakini mimi ninayemfurahia, ndiye Bwana,
ninamshangilia Mungu wangu aliyeniokoa.
19Bwana Mungu ndiye aliye nguvu yangu!
Anipa miguu ipigayo mbio kama yake kulungu,
akiniendesha vema, nifike juu vilimani kwangu.
Kwa mwimbishaji, ayaimbie mazeze yangu.