Yesaya 20

Yesaya 20

Wamisri na Wanubi watatekwa na Waasuri.

1Mwaka wake ulipotimia, Sargoni, mfalme wa Asuri, alimtuma Tartani kwenda Asdodi; akapiga vita kule Asdodi, akauteka mji huo.[#2 Fal. 18:17.]

2Mwaka uleule Bwana alisema na kumtuma Yesaya, mwana wa Amosi, akamwambia: Nenda, uvue gunia, ulilolifunga kiunoni juu, navyo viatu uvivue miguuni! Akafanya hivyo, akatembea akiwa mwenye uchi wa kifuani na miguuni.[#Ez. 24:24.]

3Bwana akasema: Kama mtumwa wangu Yesaya alivyotembea akiwa mwenye uchi wa kifuani na miguuni miaka mitatu kuwa kielekezo cha kuwaonya Wamisri nao Wanubi,

4ndivyo, mfalme wa Asuri atakavyopeleka mateka ya Misri nao Wanubi watakaokamatwa, vijana na wazee, waende wenye uchi vifuani na miguuni, hata matakoni, Wamisri watiwe soni.

5Hapo watu watastuka na kuingiwa na soni kwa ajili ya Wanubi, waliowatazamia, na kwa ajili ya Wamisri, ambao walijivunia.

6Nao wakaao kule pwani watasema siku ile: Tazameni, wale, tuliowatazamia, walivyo! Nasi twalitaka kukimbilia kwao, watusaidie, tujiponye machoni pake mfalme wa Asuri. Hivyo tungeponaje sisi?

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania