The chat will start when you send the first message.
1Tunao mji ulio wenye nguvu,
anatumia wokovu kuwa kuta za boma lake.
2Yafungueni malango, watu waongofu waingie,
washikao welekevu!
3Mawazo ya moyo yakiwa yamejishikiza,
utaendelea kuutengemanisha, utengemane kweli,
kwani tumekutegemea.
4Mtegemeeni Bwana kale na kale!
Kwani mnapokuwa naye Bwana Mungu,
mnao mwamba wa siku zote za kale na kale.
5Kwani amewanyenyekeza waliokaa juu mjini mwenye boma,
akawainamisha chini kabisa, mpaka akawaangusha uvumbini,
6wakanyagwe na miguu,
ndiyo miguu yao wakiwa na mateke yao wanyonge.
7Njia ya mwongofu hunyoka,
napo pa kupitia, unapomlinganyia mwongofu, huwa pamenyoka.
8Kweli penye maamuzi yako, Bwana, tulikungojea,
roho zetu zikalitunukia Jina lako, likumbukwe.
9Moyoni mwangu nilikutamani usiku,
namo rohoni mwangu ninakutafuta mapema,
kwani maamuzi yako yakiitokea nchi,
wakaao ulimwenguni hujifunza wongofu.
10Asiyekucha akihurumiwa hajifunzi wongofu.
ila katika nchi yenye mambo yanyokayo, huendelea kuyapotoa,
lakini utukufu wa Bwana hauoni.
11Bwana, ijapo mkono wako utukuke, hawautazami;
na wapatwe na soni wakivitazama,
jinsi unavyouhimiza wokovu wa watu.
Moto uliowamaliza wabishi wako na uwale nao.
12Ila sisi, Bwana, utatupa kutengemana,
kwani yote, tuliyoyafanya sisi, ni kazi zako, ulizotutendea.
13Bwana Mungu wetu, kuliko wewe
hata mabwana wengine walitutawala,
lakini wewe peke yako tunakutangaza, Jina lako likumbukwe.
14Wafu hawatarudi uzimani, wala wazimu hawatainuka;
kweli ulipowajia uliwaangamiza,
ukalitowesha kumbukumbu lao lote.
15Kabila hili umeliongeza, Bwana, umeliongeza kweli,
ukalitukuza, ukaipanua mipaka yote ya nchi yake.
16Bwana, wanaposongeka wanakutokea;
ulipowapiga, ndipo, walipokuja
kukunong'onezea maneno yao ya kukuomba.
17Mwenye mimba akifikisha kuzaa
hujipinda na kulia kwa uchungu wake,
ndivyo, nasi tulivyokuwa mbele yako, Bwana.
18Tulikuwa na mimba, tukashikwa na uchungu,
lakini tulipozaa, ni upepo tu!
Hatukuipatia nchi wokovu,
wala hawakupatikana wenye kukaa ulimwenguni.
19Wafu wako watarudi uzimani,
miili yao wa kwetu waliokufa itainuka.
Amkeni, mshangilie, mlalao uvumbini!
Kwani umande utokao kwenye mianga ni umande wako,
nchi iwaweke wazimu, wapate kukaa tena.
20Njoni, mlio ukoo wangu, mwingie vyumbani
na kuifunga milango yenu nyuma yenu!
Jificheni kitambo kidogo,
mpaka hayo mapatilizo makali yatakapopita!
21Kwani tazameni! Bwana anatoka mahali pake,
aje kuwalipisha wakaao katika nchi manza walizozikora.
Hapo ndipo, nchi itakapozifunua damu zilizomwagwa kwake,
haitawafunika tena waliouawa juu yake.