The chat will start when you send the first message.
1Siku ile wake saba watamshika mume mmoja na kumwambia:
Tutajipatia wenyewe vilaji na mavazi,
tunataka tu kuitwa kwa jina lako, utuondolee soni zetu!
2Siku ile mche wa Bwana
utakuwa wenye urembo na macheo,
nao uzao wa nchi
utakuwa wenye ukuu na utukufu
kwao Waisiraeli waliopona.
3Atakayekuwa amebakizwa Sioni,
naye atakayekuwa amesazwa Yerusalemu ataitwa mtakatifu,
ni kila mmoja wao aliyeandikiwa kuwapo Yerusalemu.
4Hapo ndipo, Bwana atakapokuwa amekwisha kuyaosha
machafu yao wanawali wa Sioni,
napo ndipo, atakapokuwa amekwisha kuzitowesha mwao
damu zilizomwagwa Yerusalemu;
atavifanya kwa nguvu za roho yenye mapatilizo
na kwa nguvu za roho yenye moto.
5Kwenye makao yote ya mlimani kwa Sioni
nako kwenye makutano ya kumtambikia
Bwana atakuumbia siku zote wingu
litakalokuwa lenye moshi la mchana
na lenye mwanga wa moto uwakao usiku,
kwani chote chenye utukufu hupaswa na kifuniko chake.
6Hivyo watapata pa kukalia kivulini mchana,
ukali wa jua usiwaumize,
tena pa kukimbilia na pa kujifichia,
kimbunga kisiwaangushe, wala mvua isiwapige.