The chat will start when you send the first message.
1Yasikieni haya, ninyi wa mlango wa Yakobo! Mnajiita kwa jina la Isiraeli, mlitoka viunoni mwa Yuda, mnaapa na kulitaja Jina la Bwana, naye Mungu wa Isiraeli mnamtukuza; lakini si kwa kweli wala kwa wongofu.[#Yes. 51:1.]
2Wanajiita kwa jina la mji mtakatifu, wanajishikiza kwake Mungu wa Isiraeli, Bwana Mwenye vikosi na Jina lake.
3Yale ya mbele, niliyoyatangaza hapo kale, yalitoka kinywani mwangu, nikawaambia, myasikie; maana nitakapoyafanya, yatatimia.
4Kwani nimekujua, ya kuwa u mgumu, ya kuwa ukosi wako ni mshipa wa chuma, ya kuwa kipaji cha uso wako ni shaba.[#Yer. 5:3.]
5Nikakutangazia hapo kale, nikakuambia uyasikie, yalipokuwa hayajatimia bado, usiseme: Kinyago changu kimeyafanya! wala: Kinyago changu cha mti uliochongwa au cha shaba iliyoyeyushwa kimeyaagiza!
6Umeyasikia, basi, yatazame hayo yote! Mbona ninyi hamyaungami? Tangu sasa ninakuambia mapya, uyasikie, ni mambo yaliyofichwa, usiyoyajua bado.
7Yameumbwa sasa, si kale; mpaka leo hukuyasikia bado, usiseme: Hayo nimekwisha kuyajua.
8Kweli hukuyasikia, wala hukuyajua, wala masikio yako hayajazibuka, kwani nimekujua, ya kuwa u mdanganyifu, ukaitwa mpotovu tangu kuzaliwa kwako.
9Ni kwa ajili ya Jina langu, nikayakawilisha makali yangu kwa kwamba: Na wanishangilie, nikajizuia, nisikujie, nikakung'oa.
10Tazama! Nimekung'aza na kukuyeyusha, lakini sikukuona kuwa fedha; nikakujaribu na kukutia motoni mwenye mateso.[#Sh. 66:10.]
11Kwa ajili yangu mimi nimeyafanya, Jina langu lisitiwe uchafu; maana utukufu wangu sitampa mwingine.[#Yes. 42:8.]
12Nisikilize, Yakobo, nawe Isiraeli, niliyekuita! Mimi ndiye! Mimi ni wa kwanza, tena mimi ni wa mwisho.[#Yes. 41:4.]
13Mkono wangu ndio uliozishikiza nchi, mkono wangu wa kuume ndio ulioziwamba mbingu; ninapoyaita yawayo yote, ndipo, yanapotokea.
14Kusanyikeni ninyi nyote, msikie! Kwao yuko nani aliyeyatangaza haya ya kwamba: yeye, Bwana ampendaye, ataufanyia Babeli yampendezayo, nao mkono wake utawatokea Wakasidi?[#Yes. 41:2.]
15Mimi ndimi niliyeyasema! Kisha nikamwita, nikamleta, naye na aitimize njia yake.
16Nifikieni karibu, myasikie haya! Tangu mwanzo sijasema mafichoni, tangu hapo yalipokuwapo mimi nipo!
Na sasa Bwana Mungu amenituma na kunipa roho yake.
17Ndivyo, anavyosema Bwana aliyekukomboa, aliye Mtakatifu wa Isiraeli: Mimi Bwana ndimi Mungu wako; ninakufundisha yafaayo, ninakuongoza katika njia, utakayoishika.
18Kama ungaliyaangalia maagizo yangu, utengemano wako ungalikuwa kama mto, nao wongofu wako ungalikuwa kama mawimbi ya bahari.[#5 Mose 5:29.]
19Wao wa uzao wako wangalikuwa wengi kama mchanga, nao waliotoka mwako wangalikuwa wengi kama vijiwe vya chembe yake. Majina yao hayatang'olewa hayataangamia mbele yangu.
20Tokeni Babeli! Wakimbieni Wakasidi! Yatangazeni na kupiga vigelegele, yasikilike mpaka mapeoni kwa nchi, mkiyatokeza kwamba: Bwana amemkomboa mtumishi wake Yakobo![#Yes. 52:11; Yer. 51:6; 2 Kor. 6:17; Ufu. 18:4.]
21Hawakupata kiu, alipowapitisha majangwani, akawatolea maji miambani; alipopasua miamba, maji yakabubujika.[#2 Mose 17:6.]
22Lakini hakuna utengemano kwo wasiomcha Mungu; ndivyo, Bwana anavyosema.[#Yes. 57:21; 66:24.]