The chat will start when you send the first message.
1Bwana akaniambia: Jitwalie ubao mkubwa, kauandike kwa kalamu ya kimtu, watu waweze kuusoma: Teka upesi! Pokonya hima!
2Nami nitachukua mashahidi welekevu, wanishuhudie, ni mtambikaji Uria na Zakaria, mwana wa Yeberekia.
3Kisha nikafika kwake mfumbuaji wa kike; akapata mimba, akazaa mwana wa kiume. Bwana akaniambia: Ita jina lake Teka upesi! Pokonya hima!
4Kwani kijana atakapokuwa hajajua kuita: Baba! au: Mama! watu watakuwa wameyachukua mapato ya Damasko na mateka ya Samaria, wakiyapeleka machoni pake mfalme wa Asuri.[#Yes. 7:16; 2 Fal. 15:29; 16:9.]
5Bwana akasema tena na mimi mara nyingine akiniambia:[#Yes. 30:15.]
6Kwa kuwa watu hawa wameyakataa maji ya Siloa yaendayo polepole, wakamfurahia Resini na mwana wa Remalia,
7kwa sababu hii wataona, Bwana akiwaletea maji makali ya jito kubwa yaliyo mengi; kwani mfalme wa Asuri atakuja na utukufu wake wote. Hapo ndipo, vijito vyote vitakapopanda kwa kuwa na maji mengi, nayo yatapita kingo zao zote.
8Ataiingia nchi ya Yuda kwa nguvu, maji yatafika mpaka shingoni kwa kujaa na kufurika, nayo mabawa yake yakunjukayo yataieneza nchi yako, Imanueli, ijapo iwe pana.[#Yes. 7:14.]
9Kasirikeni, ninyi makabila ya watu, kalegeeni kwa kituko! Sikilizeni, nyote mkaao katika nchi za mbali! Jifungeni, kisha legeeni kwa kituko![#Sh. 2.]
10Pigeni shauri, kisha livunjike! Semeni neno, kisha lisitimie! Kwa kuwa Imanueli yuko.[#Yes. 8:8.]
11Kwani hivi ndivyo, Bwana alivyoniambia aliponishika mkono na kunionya, nisiifuate njia ya watu wa ukoo huu, akisema:
12Msiite angamizo vyote, watu wa ukoo huu wanavyoviita angamizo! Wala msiyaogope, wanayoyaogopa, wala msiyastukie!
13Ila mtakaseni Bwana Mwenye vikosi! Yeye ndiye, mmwogope na kumstukia![#Yes. 29:23; Mat. 10:28; 1 Petr. 3:15.]
14Hivyo atakuwa mwenye kutakasa, tena atakuwa jiwe la kujigongea na mwamba wa kujikwalia kwao milango yote miwili ya Isiraeli; nao wakaao Yerusalemu atawawia kama mtego wa tanzi.[#Yes. 28:16; Rom. 9:33; 1 Petr. 2:7-8.]
15Wengi watajikwalia papo hapo, waanguke, wachubuke; wengine watanaswa, watekwe.
16Yafunge, uliyoshuhudiwa! Kisha yatie muhuri pamoja na Maonyo machoni pao wanafunzi wangu!
17Basi, sasa nitakuwa ninamwegemea Bwana na kumngojea, maana amewaficha uso wake walio mlango wa Yakobo.
18Tazama, mimi pamoja na hawa watoto, Bwana alionipa, tunakuwa vielekezo na vioja kwao Waisiraeli; ndivyo, alivyotuwekea Bwana Mwenye vikosi akaaye mlimani kwa Sioni.[#Yes. 7:3; 8:3; Ebr. 2:13.]
19Kama wanawaambia: Watafuteni wajuao kukweza mizimu nao wapunga pepo wanaonong'ona na kusema na sauti ndogo! wajibuni: Wasimtafute Mungu wao, wamwulize? Waulizeje wafu kwa ajili yao walio hai?[#2 Fal. 1:3.]
20Yarudieni Maonyo yaliyoshuhudiwa! Kweli wawezao kusema maneno kama yale hawajatokewa bado na mionzi ya jua.
21Hutangatanga katika nchi kwa kuumizwa na ukiwa na njaa; tena kwa kuumizwa na njaa huchafuka, amtukane mfalme wao na mungu wao na kutazama juu.[#Ufu. 16:9,11.]
22Kisha hutazama chini tena kwa kusongeka na kukosa mwanga, kwani wamo katika giza, nalo linawaogopesha, kwani wamesukumwa kukaa katika usiku mweusi.[#Yes. 5:30.]