The chat will start when you send the first message.
1Haya ni maneno ya Yeremia, mwana wa Hilkia aliyekuwa miongoni mwa watambikaji wa Anatoti katika nchi ya Benyamini.
2Neno la Bwana likamjia siku za Yosia, mfalme wa Yuda, mwana wa Amoni, katika mwaka wa kumi na tatu wa ufalme wake.[#2 Fal. 21:24.]
3Likamjia tena siku za Yoyakimu, mfalme wa Yuda, mwana wa Yosia, mpaka mwisho wa mwaka wa kumi na mbili wa Sedekia, mfalme wa Yuda, mwana wa Yosia, kuufikisha mwezi wa tano wa kuhamishwa kwao Wayerusalemu.[#2 Fal. 23:34; 24:17; 25:2,8.]
4Neno la Bwana likanijia kwamba:[#Yes. 49:1; Gal. 1:15.]
5Nilipokuwa sijakutengeneza tumboni mwa mama bado, nilikujua, nawe ulipokuwa hujatoka tumboni, nilikutakasa, nikakupa kuwa mfumbuaji wa mataifa.
6Nami nikasema: E Bwana Mungu, tazama! Sijui kusema, kwani mimi ni kijana.[#2 Mose 3:11; Yes. 6:5-8.]
7Bwana akaniambia: Usiseme: Mimi ni kijana! Kwani po pote, nitakapokutuma, utakwenda; nayo yote, nitakayokuagiza, utayasema.
8Usiwaogope! Kwani mimi niko pamoja na wewe, nikuponye; ndivyo, asemavyo Bwana.
9Ndipo, Bwana alipoukunjua mkono wake, akakigusa kinywa changu, naye Bwana akaniambia: Hivi ndivyo, ninavyoyatia maneno yangu kinywani mwako.[#5 Mose 18:18.]
10Tazama! Siku hii ya leo nimekupa kuwa mkuu wa mataifa na wa milango ya wafalme, uwe mkuu wa kung'oa na wa kuponda, wa kuangamiza na wa kubomoa, tena wa kujenga na wa kupanda.[#Yer. 18:7-10.]
11Neno la Bwana likanijia kwamba: Wewe Yeremia, unaona nini? Nikasema: Mimi ninaona tawi lenye kufunua maua.
12Bwana akaniambia: Umeona vema, kwani mimi nitayafumbua macho, yalilinde Neno langu, nilitimize.[#Yer. 31:28.]
13Neno la Bwana likanijia mara ya pili kwamba: Wewe unaona nini? Nikasema: Mimi ninaona chungu chenye maji yanayochemka, nao upande wake wa mbele ulioelekea kaskazini umegeuka.
14Bwana akaniambia: Upande wa kaskazini ndiko, mabaya yatakakofunuliwa, yawafikie wote wakaao nchini.
15Kwani ndivyo, asemavyo Bwana: Nitazameni! Ninaiita milango yote ya kifalme wakaao upande wa kaskazini. Nao watakuja, waweke kila mmoja wao kiti chake cha kifalme malangoni mwa Yerusalemu na ng'ambo za kuta zote za boma lake liuzungukalo, hata kwenye miji yote ya Yuda.
16Ndipo, nitakapowatokezea mapatilizo yangu kwa ajili ya ubaya wao wote, kwa kuwa wameniacha wakavukizia miungu mingine, wakatambikia yaliyofanywa na mikono yao.
17Nawe vifunge viuno vyako! Kisha inuka, kawaambie yote, nitakayokuagiza! Usizistuke nyuso zao, nisije kukustusha nyusoni pao!
18Tazama! Mimi nimekuweka leo kuwa ngome ya mji na nguzo ya chuma na boma la shaba, nchi zote zishindwe nao wafalme wa Yuda, nao wakuu wao, nao watambikaji wao, nao watu waliomo katika nchi hii.[#Yer. 15:20; Ez. 3:8-9.]
19Watapigana na wewe, lakini hawatakuweza, kwani mimi niko pamoja na wewe. Ndivyo, asemavyo Bwana, akuponye.