The chat will start when you send the first message.
1Wewe Bwana hushinda, nikiulizana wa wewe; lakini na tusemeane hukumu zipasazo! Mbona njia zao wasiokucha huendelea vema, nao wadanganyifu wanaodanganya hutengemana?[#Iy. 21:7; Sh. 73:3.]
2Uliwapanda, wakatia mizizi; huendelea kukua, mpaka wakizaa matunda. Wewe u karibu vinywani mwao, lakini u mbali mioyoni mwao.
3Nawe Bwana unanijua, ukaniona, ukanijaribu moyo wangu, kama u kwako. Wakamate kama kondoo wa kuchinjwa, kawachagulie, wawe tayari siku ya kuchinjwa!
4Nchi na iomboleze mpaka lini, majani ya mashamba yote yakinyauka? Kwa ajili ya ubaya wao waikaao hata nyama na ndege wametoweka, nao husema: Hatauona mwisho wetu![#Yer. 9:10.]
5Kama waendao kwa miguu wamekuchokesha, ulipokimbizana nao, utawezaje kushindana na farasi? Tena: Wewe ukitulia tu katika nchi itengemanayo utafanyaje ukikaa katika machaka makuu ya Yordani?
6Kwani nao ndugu zako nao mlango wa baba yako hukudanganya, kweli hawa nao hupaza sauti za kupiga kelele nyuma yako; usiwategemee! Kwani usoni pako husema mema.
7Nimeiacha Nyumba yangu, nikalitupa fungu langu, nikayatoa, roho yangu iliyopendezwa nayo, nikayatia mikononi mwa adui zao.
8Fungu langu likaniwia kama simba wa mwituni: Ameningurumia, kwa hiyo nimechukiwa naye.
9Je? Fungu langu ni kama bundi, ambaye makunguru humkusanyikia po pote? Nendeni kuwakusanya nyama wote wa porini! Kisha waleteni, wale!
10Wachungaji wengi wameiharibu mizabibu yangu, wakalikanyagakanyaga fungu langu; fungu langu, nililopendezwa nalo sana, wameligeuza kuwa mapori kama ya nyikani.
11Kweli wameligeuza kuwa peke yake tu; hivyo lilivyo peke yake linanililia, nchi hii nzima iko peke yake, kwa kuwa hakuwako mtu aliyeyaweka hayo moyoni.
12Milimani po pote katika nyika wenye kuiharibu nchi wamefika; kwani Bwana yuko na upanga ulao; huanzia kula kwenye mpaka mmoja wa nchi, hata ufike kwenye mpaka mwingine. Ndipo, wote wenye miili wanapokosa kutengemana.
13Walipopanda ngano huvuna miiba; hujisumbua, lakini hawapati kitu. Ndivyo, mtakavyopatwa na soni kwa ajili ya mavuno yenu, moto wa makali yake Bwana utakapowaka.[#5 Mose 28:38; Hos. 8:7.]
14Hivi ndivyo, Bwana anavyosema kwa ajili ya wabaya wote, tuliokaa nao, waliolitwaa fungu lile, nililowapa wao walio ukoo wangu wa Isiraeli, liwe fungu lao: Wataniona, nikiwang'oa katika nchi yao, tena nikiwang'oa walio wa mlango wa Yuda katikati yao!
15Itakuwa, nitakapokwisha kuwang'oa nitawahurumia tena, niwarudishe kila mmoja penye fungu lake, kila mmoja katika nchi yake.
16Tena itakuwa, kama wale watajifundisha vema njia zao walio ukoo wangu, waape na kulitaja Jina langu na kusema: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, kama wenyewe walivyowafundisha walio ukoo wangu kuapa na kumtaja Baali, basi, ndipo, watakapojengwa katikati yao walio ukoo wangu.[#Yer. 4:2; 5 Mose 6:13.]
17Lakini kama hawasikii, nitaling'oa taifa hilo kabisa, liangamie; ndivyo, asemavyo Bwana.