Yeremia 21

Yeremia 21

Mji wa Yerusalemu utaangamia.

1Hili ndilo neno lililotoka kwa Bwana, likamjia Yeremia, mfalme Sedekia alipomtuma Pashuri, mwana wa Malkia, na mtambikaji Sefania, mwana wa Masea, kwenda kwake kwamba:[#Yer. 29:25.]

2Mwulize Bwana kwa ajili yetu, kwani Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, ametuletea vita. Labda Bwana atatufanyizia nasi, kama mataajabu yake yote yalivyo, akiwaondoa kwetu.

3Yeremia akawaambia: Hivi ndivyo, mmwambie Sedekia:

4Hivi ndivyo, Bwana Mungu wa Isiraeli anavyosema: Mtaniona, nikivirudisha vyombo vya vita vilivyo mikononi mwenu, mlivyovitumia kupiga vita na mfalme wa Babeli na Wakasidi wanaowasonga! Nitavitoa huko nje, nivilete kwenye boma, kisha nitavikusanya humu mjini katikati.

5Nami mwenyewe nitapigana nanyi kwa kiganja kilichofumbuka cha mkono ulio wenye nguvu kwa kuwa na makali yenye moto na machafuko makubwa.

6Nitawatoa wakaao humu mjini, watu hata nyama, watakufa kwa ugonjwa mbaya uuao kabisa.

7Ndivyo, asemavyo Bwana: Hayo yatakapokwisha, nitamtoa Sedekia, mfalme wa Yuda, pamoja na watumishi wake nao walio wa ukoo huu waliosalia humu mjini kwa ule ugonjwa mbaya na kwa panga na kwa njaa, nitawatia mikononi mwa Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, nami mikononi mwa adui zao namo mikononi mwao wanaozitafuta roho zao, naye atawapiga kwa ukali wa upanga, hatawaonea uchungu, wala hatawachagulia, wala hatawahurumia.

8Nao walio wa ukoo huu utawaambia: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Nitazameni! Ninalinganya machoni penu njia ya uzima na njia ya kufa.[#5 Mose 11:26.]

9Atakayekaa humu mjini atakufa kwa upanga na kwa njaa na kwa magonjwa mabaya. Lakini atakayetoka na kuwaangukia Wakasidi wanaowasonga atapona, nayo roho yake itakuwa pato lake.[#Yer. 38:2.]

10Kwani nimeuelekeza uso wangu kwenye mji huu, niupatie mabaya, mema siyo; utatiwa mkononi mwake mfalme wa Babeli, auteketeze kwa moto; ndivyo, asemavyo Bwana.

11Nao wa mlango wa mfalme wa Yuda waambie: Lisikieni neno la Bwana!

12Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Ninyi wa mlango wa Dawidi, asubuhi pigeni mashauri, mwaponye walionyang'anywa mkiwatoa mikononi mwa wakorofi, makali yangu yasitokee kuwa moto uwakao, asipopatikana mwenye kuuzima kwa ajili ya ubaya wa matendo yenu![#Yer. 7:20; 22:3.]

13Ndivyo, asemavyo Bwana: Utaniona, nikikujia wewe ukaaye bondeni, uliye kama mwamba mbugani. Ninyi husema: Yuko nani atakayetushukia? Yuko nani atakayeingia katika makao yetu?

14Mimi nitawapatiliza, kama matendo yenu yalivyowapatia; ndivyo, asemavyo Bwana. Nitawasha moto mwituni kwao utakaozila nchi zote ziwazungukazo.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania