The chat will start when you send the first message.
1Sefatia, mwana wa Matani, na Gedalia, mwana wa Pashuri, na Yukali, mwana wa Selemia, na Pashuri, mwana wa Malkia, wakayasikia yale maneno, Yeremia aliyowaambia watu wote wa ukoo huu kwamba:[#Yer. 21:1.]
2Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Akaaye humu mjini atakufa kwa panga na kwa njaa na kwa magonjwa mabaya; lakini atakayewatokea Wakasidi atapona, roho yake itakuwa pato lake.[#Yer. 21:9.]
3Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Mji huu utatiwa kweli mikononi mwao vikosi vya mfalme wa Babeli, atauteka.
4Wakuu wakamwambia mfalme: Mtu huyu sharti auawe! Kwani anailegeza mikono ya wapiga vita waliosalia humu mjini, nayo mikono yao wote walio wa ukoo huu, akiwaambia maneno kama hayo; kwani mtu huyu hatafuti, jinsi watu watakavyokaa salama, ila jinsi watakavyoona mabaya.[#Amo. 7:10.]
5Mfalme Sedekia akawaambia: Tazameni! Yumo mikononi mwenu. Kwani hakuna mfalme awashindaye ninyi jambo lo lote.
6Wakamchukua Yeremia, wakamtupa katika kisima cha Malkia, mwana wa mfalme, kilichokuwa hapo uani penye kifungo, wakamshusha Yeremia mle kwa kamba. Mle kisimani hamkuwa na maji, ila ni matopetope tu, Yeremia akaanza kuzama matopeni.
7Mnubi Ebedimeleki aliyekuwa mtumishi nyumbani mwa mfalme akasikia, ya kuwa wamemtumbukiza Yeremia mle kisimani. Siku moja, mfalme alipokaa penye lango la Benyamini,[#Yer. 39:16.]
8Ebedimeleki akatoka nyumbani mwa mfalme, akaja kusema na mfalme kwamba:
9Bwana wangu mfalme, yote, watu waliyomfanyizia mfumbuaji Yeremia, ni mabaya, wakimtupa kisimani, afie mle ndani kwa njaa, kwani hamna mkate tena humu mjini.
10Ndipo, mfalme alipomwagiza yule Mnubi Ebedimeleki kwamba: Chukua hapa kwa mkono wako watu thelathini, umwopoe mfumbuaji Yeremia mle kisimani, angaliko hajafa bado!
11Ebedimeleki akawachukua wale watu kwa mkono wake, akaingia nyumbani mwa mfalme chumba cha chini cha kuwekea malimbiko, akachukua mle vitambaa vya nguo zilizopasuka na vitambaa vya nguo chakavu, akavishusha kwa kamba kisimani kwake Yeremia.
12Yule Mnubi Ebedimeleki akamwambia Yeremia: Hivi vitambaa vya nguo zipasukazo na vya nguo chakavu vitie makwapani chini ya kamba! Yeremia akayafanya hivyo.
13Kisha wakamvuta Yeremia kwa hizo kamba, wakamwopoa kisimani, Yeremia akakaa tena uani penye kifungo.
14Mfalme Sedekia akatuma kumchukua mfumbuaji Yeremia, aje kwake penye lango la tatu la kuiingilia Nyumba ya Bwana, mfalme akamwambia Yeremia: Mimi ninataka kukuuliza neno, lakini usinifiche lo lote!
15Yeremia akamwambia Sedekia: Je? Nikikujulisha yote, hutaniua? Tena nikikupa shauri, hutanisikia.
16Ndipo, mfalme alipomwapia Yeremia penye njama kwamba: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima, aliyetuumbia hii roho yetu, sitakuua, wala sitakutia mikononi mwao watu hawa wanaoitafuta roho yako.[#Yer. 38:4-5.]
17Ndipo, Yeremia alipomwambia Sedekia: Hivi ndivyo, Bwana Mungu Mwenye vikosi, Mungu wa Isiraeli, anavyosema: Kama utawatokea wakuu wa mfalme wa Babeli, roho yako itapona, nao mji huu hautateketezwa kwa moto; hivyo utapona wewe na mlango wako.
18Lakini usipowatokea wakuu wa mfalme wa Babeli, mji huu utatiwa mikononi mwao Wakasidi, wauteketeze kwa moto, wewe nawe hutapona mikononi mwao.
19Mfalme Sedekia akamwambia Yeremia: Mimi ninawaogopa Wayuda waliorudi upande wa Wakasidi, wasinitie mikononi mwao, nao wakanizomea.
20Yeremia akamjibu: Hawatakutoa. Isikie tu sauti ya Bwana, niliyokuambia mimi! Ndivyo, utakavyoona mema, nayo roho yako itapona.
21Lakini wewe ukikataa kuwatokea, basi, neno, Bwana alilonionyesha, ni hili:
22Utaona, wanawake wote waliosalia nyumbani mwa mfalme wa Yuda wakitolewa na kupelekwa kwa wakuu wa mfalme wa Babeli; nao watakwenda wakisema: Wamekupoteza, wakakushinda wale, uliotengemana nao! Lakini hapo, miguu yako iliposhikwa na matope, wamerudi nyuma![#Yer. 6:14.]
23Wakeo wote na wanao wa kiume wote watawatoa na kuwapeleka kwa Wakasidi, wewe nawe hutapona mikononi mwao, kwani utakamatwa kwa mikono ya mfalme wa Babeli, nao mji huu utateketea kwa moto.[#Yer. 32:4; 34:3.]
24Ndipo, Sedekia alipomwambia Yeremia: Mtu ye yote asiyajue haya maneno, wewe usife!
25Kama wakuu wanasikia, ya kuwa nimesema na wewe, wakija kwako kukuambia: Tusimulie, uliyomwambia mfalme, usitufiche! Hatutakuua, tusimulie nayo, mfalme aliyokuambia!
26ndipo, utakapowaambia: Mimi nimekuwa nikimlalamikia mfalme na kumwangukia, asinirudishe nyumbani mwa Yonatani, nisifie mle!
27Wakuu wakaja kwake Yeremia, wakamwuliza, akawaambia hayo maneno yote, kama mfalme alivyomwagiza, wakamwacha na kunyamaza, kwani lile shauri halikujulikana.
28Kisha Yeremia akakaa uani penye kifungo mpaka siku ile, Yerusalemu ulipotekwa.[#Yer. 37:21.]