The chat will start when you send the first message.
1Hili ndilo neno lililomjia Yeremia likitoka kwa Bwana, Nebuzaradani, mkuu wao waliomlinda mfalme, alipompa ruhusa huko Rama kujiendea; naye alimpata, alipokuwa amefungwa kwa minyororo, katikati ya mateka yote ya Yerusalemu na ya Yuda waliokwenda kupelekwa Babeli.[#Yer. 39:11-14.]
2Hapo, mkuu wao waliomlinda mfalme alipomchukua Yeremia, akamwambia: Bwana Mungu wako aliyasema haya mabaya, ya kuwa yatapajia mahali hapa.
3Basi, ameyaleta, akayafanya, kama alivyoyasema, kwani mmemkosea Bwana, msipoisikia sauti yake; ndipo, jambo hili lilipofanyika kwenu.
4Sasa tazama! Nimekufungulia leo minyororo, mikono yako iliyofungwa nayo; vikiwa vema machoni pako kwenda na mimi kufika Babeli, njoo! nitakuangalia kwa macho yangu. Lakini vikiwa vibaya machoni pako kwenda na mimi kufika Babeli, acha! Tazama, nchi hii yote iko mbele yako, patakapokuwa pema kwa kufaa machoni pako, nenda pale!
5Alipokuwa hajaenda bado huko wala huko, akamwambia: Rudi kwake Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Safani, mfalme wa Babeli aliyemweka kuwa msimamizi katika miji ya Yuda, ukae naye katikati yao walio wa ukoo wako! Au po pote palipofaa machoni pako kwenda kukaa, nenda hapo! Kisha mkuu wao waliomlinda mfalme akampa pamba za njiani na matunzo, akampa ruhusa kujiendea.[#Yer. 39:14.]
6Yeremia akaja Misipa kwake Gedalia, mwana wa Ahikamu, akakaa naye katikati yao walio wa ukoo wake, waliosazwa katika nchi hiyo.
7Wakuu wote wa vikosi waliokuwa bado porini na watu wao waliposikia, ya kuwa mfalme wa Babeli amemweka Gedalia, mwana wa Ahikamu, kuisimamia nchi hiyo, akimpa waume na wake na watoto nao wanyonge wa nchi hiyo nao wasiopelekwa Babeli,[#2 Fal. 25:22-24.]
8ndipo, walipokuja Misipa kwa Gedalia. Ndio Isimaeli, mwana wa Netania, na Yohana na Yonatani, wana wa Karea, na Seraya, mwana wa Tanumeti, nao wana wa Efe wa Netofa na Yezania, mwana wa mtu wa Maka, hao wenyewe na watu wao.[#Yer. 41:1,11.]
9Waume hawa na watu wao Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana Safani, akawaapia kwamba: Msiogope kuwatumikia Wakasidi! Kaeni katika nchi hii na kumtumikia mfalme wa Babeli! ndipo, mtakapoona mema.
10Nami mnaniona: ninakaa Misipa, nisimame mbele yao Wakasidi, watakaokuja kwetu. Nanyi mtachuma zabibu na matunda mengine ya kiangazi nayo yaliyo yenye mafuta, myaweke katika vyombo vyenu mkikaa katika miji yenu, mtakayoichukua.
11Nao Wayuda wote waliokuwako Moabu kwa wana wa Amoni na Edomu na katika nchi zote waliposikia, ya kuwa mfalme wa Babeli ameacha masao katika nchi ya Yuda, akamweka Gedalia, mwana wa Ahikamu, mwana wa Safani, kuwaangalia,
12ndipo, waliporudi Wayuda wote wakitoka mahali po pote, walipotupiwa, wakaja Misipa katika nchi ya Yuda kwa Gedalia, wakachuma zabibu na matunda ya kiangazi mengi sana.
13Yohana, mwana wa Karea, nao wakuu wote wa vikosi waliokuwa porini bado walipokuja Misipa kwa Gedalia,
14wakamwambia: Unajua, ya kuwa Balisi, mfalme wa wana wa Amoni, amemtuma Isimaeli, mwana wa Netania, akuue wewe? Lakini Gedalia, mwana wa Ahikamu, hakuwategemea.
15Ndipo, Yohana, mwana wa Karea, alipomwambia Gedalia penye njama huko Misipa kwamba: Na niende, nimwue Isimaeli, mwana wa Netania, mtu asijue! Kwa nini akuue wewe mwenyewe, Wayuda wote waliokusanyika kwako watawanyike tena, hayo masao ya Yuda yaangamie?
16Lakini Gedalia, mwana wa Ahikamu, akamwambia Yohana, mwana wa Karea: Usilifanye neno hili! Kwani unamsemea Isimaeli uwongo.