The chat will start when you send the first message.
1Tembeeni katika barabara za Yerusalemu! Tazameni, mjue! Tafuteni katika viwanja vyake, kama mnaona mtu awaye yote afanyaye yanyokayo, atafutaye welekevu! Ndipo, nitakapowaondolea makosa.
2Wakisema: Hivyo, Bwana alivyo Mwenye uzima! huapa kwa uwongo.
3Bwana, kumbe macho yako hayautazami welekevu? Uliwapiga, lakini hawakuzizimuka; ukawapiga tena, lakini wakakataa kuonyeka. Wakazishupaza nyuso zao kupita miamba, wakakataa kurudi.[#Yer. 2:30; Yes. 48:4.]
4Nami nalisema moyoni: Ndio wanyonge tu walio wapumbavu hivyo, kwani hawaijui njia ya Bwana wala yampasayo Mungu wao.
5Na niende kwenye wakuu kusema nao! Kwani hao wanaijua njia ya Bwana nayo yampasayo Mungu wao; nikaona, hao wote pamoja wamevivunja vyuma vyao, hata kamba wamezikata.[#Yer. 2:20.]
6Kwa sababu hii simba wa mwituni amewapiga, naye mbwa wa jangwani akawaangamiza, naye chui huwavizia kwenye miji yao, kila atakayetoka mle araruliwe. Kwani mapotovu yao ni mengi, ukatavu wao ni wenye nguvu.[#3 Mose 26:22.]
7Hayo nitakuachiliaje? Wanao wameniacha, huapa na kutaja isiyo miungu; nilipowashibisha, huzini, hukusanyikia nyumbani mwa wagoni.
8Wakatembea kama farasi walionona, kila mmoja akimlilia mke wa mwenziwe.
9Mambo kama hayo nisiyapatilize? ndivyo, asemavyo Bwana; watu walio hivyo roho yangu isiwalipize?[#Yer. 5:29.]
10Pandeni juu kutani kwao, mwaangamize! Lakini msiwamalize kabisa! Yaondoeni matawi yake! Kwani siyo yake Bwana![#Yer. 4:27.]
11Kwani walio mlango wa Isiraeli nao walio mlango wa Yuda wameniacha kwa udanganyifu; ndivyo, asemavyo Bwana.
12Walimkana Bwana, wakasema: Hayupo, wala hakuna kibaya kitakachotujia, hatutaona upanga wala njaa.
13Nao wafumbuaji watakuwa upepo tu, lakini Neno halimo mwao; wenyewe na wafanyiziwe waliyoyasema.
14Kweli hivi ndivyo, Bwana Mungu Mwenye vikosi anavyosema: Kwa kuwa mmesema neno hilo, mtaniona, nitayageuza maneno yangu kinywani mwako kuwa moto, nao watu wa ukoo huu watakuwa kuni, nao moto utawala.
15Mtaniona, ninyi wa mlango wa Isiraeli, nikiwaletea taifa litokalo mbali, ndio watu wenye nguvu, ndio watu wa kale, ndio watu, usiowajua msemo wao, usiwasikie, wakisema; ndivyo, asemavyo Bwana.[#Yer. 6:22.]
16Mapodo yao ni kama makaburi yaliyo wazi, wote ndio mafundi wa vita.
17Nao watayala mavuno yako na vilaji vyako; watawala hata wanao wa kiume na wa kike, watawala kondoo wako na ng'ombe wako, wataila mizabibu yako na mikuyu yako; wataibomoa kwa panga zao miji yako yenye maboma, uliyoikimbilia.
18Lakini hata siku hizo, sitawamaliza kabisa; ndivyo, asemavyo Bwana.
19Napo, watakapouliza: Kwa sababu gani Bwana Mungu wetu ametufanyizia hayo yote? ndipo, utakapowajibu: Kama mlivyoniacha na kutumikia miungu migeni katika nchi yenu, ndivyo, mtakavyotumikia wageni katika nchi isiyo yenu.
20Yatangazeni haya nyumbani mwa Yakobo, yasikilike kwa Wayuda, kwamba:
21Yasikieni haya, mlio watu wenye upumbavu pasipo mawazo ya moyoni! Macho mnayo, lakini hamwoni; masikio mnayo, lakini hamsikii.[#Yes. 6:9-10.]
22Mimi hamniogopi, wala uso wangu hamwuzizimukii; ndivyo, asemavyo Bwana. Nami ndimi niwekaye mchanga kuwa mpaka wa bahari, ni tengenezo la kale na kale, nayo haipapiti; ijapo ichafuke, haipashindi, ingawa mawimbi yake yaumuke, hayapapiti.[#Iy. 38:8-11.]
23Lakini wao wa ukoo huu wanayo mioyo ikataayo kutii, iliyo yenye ubishi, wakaondoka kwenda zao.
24Hawakusema mioyoni mwao: Na tumwogope Bwana Mungu wetu atupaye mvua za masika na za vuli, siku zao zinapotimia, atulindiaye majuma ya mavuno mwaka kwa mwaka.[#Tume. 14:17.]
25Lakini manza zenu zimeyatengua haya, makosa yenu yakawanyima mema.[#Yes. 59:2.]
26Kwani kwao walio ukoo wangu wameonekana wasionicha; wanavizia na kunyatia kama wategea ndege, hutega mitego, wakanasa watu.
27Kama tundu linavyojaa ndege, ndivyo, nyumba zao zinavyojaa madanganyo, kwa hiyo wakawa wakubwa, wakapata mali nyingi.
28Wamenenepa kwa kunona; maneno yao mabaya hupita kiasi; kuamua hawaamui, nao waliofiwa na wazazi hawawaamulii, wawaponye, wala wakiwa hawawakatii mashauri yao.[#2 Mose 22:22; Yes. 1:23.]
29Kumbe haya nisiyapatilize? Mambo kama hayo roho yangu isiyalipize? ndivyo, asemavyo Bwana.[#Yer. 5:9.]
30Mambo ya kustuka yazizimuayo hufanyika katika nchi hii.
31Wafumbuaji hufumbua yenye uwongo, nao watambikaji hufanya shauri moja nao, nao walio ukoo wangu, basi, hupenda hivyo. Lakini mtafanya nini, mwisho utakapofika?