Iyobu 10

Iyobu 10

Iyobu analia, ya kuwa Mungu anamwumiza zaidi.

1Roho yangu inachukizwa na kuwapo kwangu, kwa hiyo sitajikataza kupiga kite, na niseme kwa uchungu wa roho yangu.

2Nitamwambia Mungu: Usiniwazie kuwa mwovu! Ila nijulishe sababu za kunigombeza!

3Je? Kwako ni vema, ukimkorofisha mtu? Kiumbe, mikono yako ilichokisumbukia, ukatitupa, uyaangaze mashauri yao wasiokucha?

4Je? Wewe nawe unayo macho ya kimwili? Kama mtu anavyoona, ndivyo, unavyoona nawe?[#1 Sam. 16:7.]

5Kama siku za mtu zilivyo, ndivyo, zilivyo nazo siku zako? Au miaka yako inafanana nazo siku zake mtu mume?

6Kwani unaninyatia, uone manza, nilizozikora, ukayatafuta makosa yangu mimi.

7Tena unanijua kuwa mtu asiyeacha kukucha, ya kuwa hakuna atakayeniponya mkononi mwako.

8Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunitengeneza, ikanipatia yote, niliyo nayo, nawe unaniangamiza![#Sh. 139:14.]

9Kumbuka, ya kuwa ulinifinyanga kama udongo! Tena unataka kunirudisha uvumbini?[#Iy. 33:6; 1 Mose 2:7; 3:19.]

10Kama maziwa mabichi ulinimwaga ukanigandisha kuwa kama maziwa mabivu.

11Kisha ukanivika ngozi na nyama, kazi ya kuiunga mifupa na mishipa yangu, ilipokuwa imekwisha.

12Ukanipatia uzima na upendeleo, ukaikagua roho yangu na kuiangalia.

13Tena ukaficha moyoni mwako mawazo kama hayo, najua, ya kuwa unayo kweli yale ya kutaka,

14uniangalie, kama ninakosa, usinikomboe katika manza, nitakazozikora.

15Kama nafanya maovu, nitaangamia; lakini hata nisipokosa, sitaweza kukiinua kichwa changu, kwani nashiba kwa kuona soni nikiutazama unyonge wangu.

16Kama kichwa changu kingeinuka, ungenikimbiza kama simba, ukanirudia na kunionyesha mastaajabu yako;[#Yes. 38:13.]

17ungetoa mara kwa mara mashahidi wa kunisuta, upate kuyazidisha makali ya kunitolea, wawe vikosi vizima vyao wanaopokeana kunitesa.

18Kwa sababu gani ulinitoa tumboni mwa mama? Macho ya watu yalipokuwa hayajaniona bado, ningalizimia hapo,[#Iy. 3:3,11; Yer. 20:14.]

19ningalikuwa kama mtu asiyepata kuwapo, ningalipelekwa kaburini hapo, nilipotoka tumboni mwa mama.

20Siku zangu zilizosalia si chache tu? Kwa hiyo na akome, na aniache, nipate kuchangamka kidogo,

21nikiwa sijaenda bado hapo, ambapo sitaweza kutoka, nirudi huku, nikikaa katika ile nchi yenye giza penye kivuli kiuacho;[#Iy. 7:10.]

22ni nchi yenye giza jeusi kama usiku wa manane, ni nchi ikaayo kivuli kiuacho, tena ni nchi ikosayo matengenezo yo yote, nayo ikiangazika huwa vilevile kama usiku wa manane.

Sofari anasema: Iyobu sharti amnyenyekee Mungu.

Sofari na Nama akajibu akisema:

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania