The chat will start when you send the first message.
1Mtu anayeweza kumfalia Mungu yuko wapi?
2Kwani mwenye akili hujifalia mwenyewe tu.
3Itampendeza Mwenyezi, ukiwa mwongofu? Anapata nini, ukizitengeneza njia zako, zisikukoseshe?
4Je? Anakupatiliza kwa kumwogopa? Hii ndiyo sababu ya kukupeleka shaurini?
5Siyo mabaya yako yaliyo mengi? Hakuna kikomo cha manza, unazozikora.
6Kwani ndugu zako uliwatoza rehani bure tu, nao wakosao nguo ukawavua mavazi.[#Iy. 24:9-10; 2 Mose 22:26-27; Yes. 58:7.]
7Mwenye kiu hukumpa maji, apate kunywa, naye mwenye njaa ukamnyima chakula.[#Mat. 25:42-43.]
8Aliyekuwa mwenye mkono, nchi ikawa yake, naye aliyejivuna usoni pa watu ndiye aliyepata kukaa huku.
9Wajane uliwafukuza kwako, wajiendee mikono mitupu, nao waliofiwa na wazazi wakaumizwa mikono.[#Iy. 29:12.]
10Kwa hiyo sasa matanzi yanakuzunguka pande zote, mara yanafyatuka, yakutie woga.
11Au hiyo giza nayo huioni? Wala furiko la maji litakalokufunika?
12Je? Mungu hayuko mbinguni juu? Zitazame nazo nyota zilizoko mbali juu ya kichwa chako!
13Nawe unasema: Mungu anayoyajua ndio nini? Akiwa mawinguni mwenye weusi atawezaje kutuamua?
14Hujificha mle mawinguni, asione kitu; hutembea na kuzunguka mbinguni tu.
15Je? Unaiangalia njia ya kale, usiiache? Nao walioikanyaga ni watu waovu.
16Siku zao zilipokuwa hazijatimia bado, ndipo, walipopokonywa, msingi wao ulipoyeyuka kuwa kama jito;[#Iy. 15:32-33; 1 Mose 7:21.]
17ndio, waliomwambia Mungu: Ondoka kwetu! Yako mambo gani atakayotufanyizia huyo Mwenyezi?[#Iy. 21:14.]
18Naye ndiye aliyezijaza nyumba zao vitu vyema; kwa hiyo mawazo yao wasiomcha na yawe mbali, yasinifikie![#Iy. 21:16.]
19Waongofu wakiyaona watafurahi, naye atakataye atawasimanga kwamba:[#Sh. 107:42.]
20Kumbe waliotuinukia wametoweka, nayo masao yao moto umeyala!
21Jizoeze kuandamana naye Mungu, upate kutengemana! Mema yake yatakavyokufikia, ndivyo hivyo.
22Kinywa chake kikikuonya, mwitikie, nayo maneno yake yaweke moyoni mwako!
23Utakaporudi kwake Mwenyezi utajengwa, ni hapo, utakapoutoa upotovu mahemani mwako, usikukaribie tena.[#Iy. 8:5-7; 11:14-19.]
24Huo mchanga wenye dhahabu uutupe uvumbini, nayo dhahabu ya Ofiri itupe penye vijiwe vya mito![#1 Fal. 9:28.]
25Ndipo, Mwenyezi atakapokuwa dhahabu zako na fedha zako zipitazo nyingine kwa kima kikuu.
26Hapo ndipo, utakapomfurahia aliye Mwenyezi na kumwelekezea Mungu uso wako.[#Sh. 37:4.]
27Utakapomlalamikia, atakusikia, nawe utayalipa uliyoyaapa, umtolee yayo hayo.[#Sh. 50:14-15.]
28Nalo utakalowaza kulifanya, utafanikiwa, hata katika njia zako mwanga utakumulikia.
29Zitakapokunyenyekeza, utasema: Na nitukuke, naye aliye mnyenyekevu machoni pake mwenyewe atamwokoa.[#1 Petr. 5:5.]
30Naye asiyetakata atamponya, kweli atapona kwa mikono yako, ikiwa imetakata.[#Sh. 18:21,25.]
Iyobu akajibu, akisema: