The chat will start when you send the first message.
1Mbona hazikuwekwa na Mwenyezi siku zake za mapatilizo? Mbona hawazioni hizo siku zake wao wamjuao?
2Wasogezao mipaka wako huku, nao wanyang'anyao makundi ya kondoo, wayachunge kuwa yao.[#5 Mose 27:17.]
3Punda wao waliofiwa na wazazi huwachukua, nao ng'ombe wa wajane huwakamata kuwa rehani.
4Huwakumba maskini, waondoke njiani, wanyonge wa huku chini wote pia hawana budi kujificha.
5Watazameni, kama hawafanani nao vihongwe vya nyikani: hutoka na mapema kufanya kazi zao za kujipatia chakula, wanakojipatia chakula cha watoto, ndiko porini.
6Mashambani kwa watu huchuma ya kujilisha, nayo mizabibu yao wasiomcha Mungu huiokoteza.
7Hulala usiku wenye uchi pasipo nguo za kujifunika, hawana mablanketi ya kujizuilia baridi ya kipupwe.
8Hulowa kwa kunyewa na mvua za milimani, kwa kukosa kimbilio hujibana mwambani.
9Tena wako wapokonyao kifuani kwa mama waliofiwa na baba, nao wanyonge huwavua mavazi kuwa rehani;
10kisha huwaacha, wajiendee wenye uchi pasipo nguo yo yote; nao wenye njaa huchukuzwa viganda vya ngano.[#Yes. 58:7.]
11Uani pa mabwana zao hutengeneza mafuta, ijapo wenyewe wawe wenye kiu, huwakamulia wao zabibu.[#Yak. 5:4.]
12Wenye kufa wakipiga kite, husikilika toka mjini, nazo roho zao waliouawa kwa nguvu hulilia malipizo, lakini wakipumbazwa vibaya hivyo, Mungu haviangalii.
13Wenye kuchukizwa na mwanga ndio wenzao wale, hukataa kuzitambua njia zake hivyo, zilivyo, penye mikondo yake hawakai.
14Mwuaji huinuka, kukipambazuka, aje kumwua mnyonge naye mkiwa, mambo ya usiku hufanana nayo yake mwizi.
15Macho ya mzinzi hungoja kuchwa kwa kwamba: Pasipatikane jicho litakaloniona; kwa hiyo huuficha uso wake.
16Penye giza hujipenyeza nyumbani mwa watu, kwa kukataa kuona mwanga hujifungia mchana.
17Mapema yao hao wote pamoja ndio giza kuu, kwani huvijua mastusho yake hilo giza kuu.
18Yeye kwa kuwa kama aendaye juu ya maji laiti angepita upesi, fungu lake la huku chini liapizwe, njia ya kwenda mizabibuni asiishike tena![#1 Mose 49:4.]
19Kama kiangazi kinavyotowesha maji ya theluji kwa ukali wa jua, vivyo hivyo kuzimu na kuwatoweshe wakosaji walio hivyo.
20Nalo tumbo la mama na limsahau, wadudu wakiufurahia utamu wa mwili wake; kwa kuwa mpotovu na avunjwe kama mti, asikumbukwe tena.
21Kwa maana aliwanyang'anya vyao wanawake wasiozaa, nao wajane hakuwafanyizia chema cho chote.
22Kwa uwezo wake Mungu huwakalisha sana walio wenye nguvu, hata aliyekwisha kukata tamaa ainuke tena na kupata uzima.
23Humpa kukaa na kutulia kwa kupata egemeo, nayo macho yake huzielekea njia zao.
24Wakiisha kujipatia utukufu mara hawako tena, hutoweka kwa kupokonywa kama wote wengine; nao hukatwa kama masuke yaliyoko juu mabuani.
25Au sivyo vilivyo? Yuko nani awezaye kuniumbua kuwa mwongo na kuyatokeza maneno yangu kuwa ya bure?
Bildadi wa Sua akajibu akisema: