Iyobu 26

Iyobu 26

1Kweli umemsaidia sana asiye na uwezo,

2ukamwokoa mwenye mikono isiyo na nguvu!

3Asiyeerevuka kweli umemwongoza vema ukimjulisha mizungu iliyo mingi!

4Ni nani, uliyemwambia hayo maneno yako? Tena ni roho ya nani iliyokusemesha?

5Nao wazimu walioko chini hutetemeka, nayo maji pamoja nao wakaao humo.

6Kuzimu kuko waziwazi machoni pake, huko ndani ya nchi hakuna kabisa ficho lo lote.[#Fano. 15:11.]

7Aliutandaza upande wa kaskazini mahali pasipokuwa na kitu, nayo nchi aliiweka kuwa juu ya hapo pasipokuwa lo lote kabisa.

8Katika mawingu yake hufunga maji, lakini hakuna wingu lipasukalo chini yao.[#Sh. 104:3.]

9Hukifunika kiti chake cha kifalme, kisionekane, kwa kukitandazia wingu lake.

10Alipima mviringo juu ya maji, uwe mpaka; ndipo, mwanga unapokutana nayo giza.[#Iy. 38:10-11; Fano. 8:27-29.]

11Nguzo za mbingu hutukutika kwa kutetemeka, akichafuka.

12Kwa uwezo wake huzistusha nazo bahari, kwa utambuzi wake huwaponda nao nondo waliomo baharini.

13Kwa kuzipuzia mbingu huzichangamsha, mkono wake humchoma naye joka kubwa, akikimbia.[#Yes. 27:1.]

14Tazameni! Huku ni kama pembeni tu kwa njia zake, hayo maneno yake, tunayoyasikia, ni manong'ono tu, lakini hizo nguvu za ngurumo zenyewe yuko nani atakayezitambua?

Jibu la mwisho la Iyobu: Waovu hawana budi kuangamia.

Iyobu akaendelea kutoa mifano akisema:

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania