Iyobu 27

Iyobu 27

1Hivyo, Mungu alivyo Mwenye uzima, ijapo akatae kuniamulia,

2hivyo, Mwenyezi alivyoitia roho yangu machungu haya,

3siku zote, nitakapokuwa ninakokota roho bado, pumzi ya Mungu itakapokuwa ingalimo puani mwangu:

4midomo yangu haitasema neno lipotokalo, wala ulimi wangu hautaongopa.[#Sh. 34:14.]

5Ninyi sitawaitikia kale na kale mpaka nitakapozimia, sitakoma kuvieleza kwamba: Sikukosa.

6Neno hili ninalishika sana, sitaliacha kwamba: Mimi ni mwongofu, moyo wangu haunisutii moja tu miongoni mwao siku zangu.[#Tume. 24:16; 1 Kor. 4:4.]

7Mchukivu wangu na yampate yanayompata asiyemcha Mungu, naye aniinukiaye na yampate yaleyale yanayompata mpotovu.

8Kwani mwovu akijipatia mapato kwa kukorofisha watu, Mungu atakapoitaka roho yake kwake, yuko na kingojeo gani?[#Luk. 12:20.]

9Mungu atavisikia vilio vyake, masongano yatakapompata?

10Au atamfurahia Mwenyezi, amlilie Mungu kila, anapotaka?

11Nitawafundisha ninyi matendo yake mkono wa Mungu, Mwenyezi anayoyafanya, sitawaficha!

12Ninyi nyote yatazameni mliyoyaona! mbona mwajisemea tena maneno yaliyo bure kabisa?

13Hili ni fungu lake asiyemcha Mungu lililoko kwake Mungu, tena ni urithi, watakaoupata kwake Mwenyezi, wao wakorofi.

14Wanawe watakapokua watauawa na upanga, nao wajukuu wake hawatashiba vyakula.[#Iy. 21:19.]

15Watakaosalia kwake watazikwa kwa kuuawa na kipindupindu, nao wajane wao hawatawaombolezea.

16Ijapo, alimbike fedha kuwa nyingi kama mavumbi, ijapo, ajiwekee mavazi kuwa mengi kama mchanga,

17ijapo, ayaweke hivyo, atakayeyavaa ni mwongofu, nazo fedha watajigawanyia wao watakatao.[#Fano. 13:22.]

18Akijenga nyumba yake, huwa kama buibui, au kama dungu, wanalomjengea mlinzi.

19Anakwenda kulala mwenye mali, lakini ni mara ya mwisho, akifumbua macho, hakuna mali tena.

20Mastusho yanamfikia kama maji mengi, upepo wa chamchela unampokonya usiku.

21Upepo utokao maawioni kwa jua unamchukua, ajiendee, ukimwondoa kwa nguvu hapo pake, alipokuwa.

22Unampiga mishale yake pasipo kumhurumia, hata atake hili mojo tu: kukimbia, atoke mkononi mwake.

23Watu wanampigia makofi na kumzomea, akitoka hapo pake, alipokuwa.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania