The chat will start when you send the first message.
1Mlio werevu wa kweli, yasikieni ninayoyasema!
2Nitegeeni masikio yenu, mlio wajuzi!
3Kwani sikio huyajaribu yanayosemwa, ufizi nao huyaonja yanayoliwa.[#Iy. 12:11.]
4Yaliyo sawa ndiyo, tujichagulie, sote pamoja tuyajue yaliyo mema!
5Kwani Iyobu amesema: Mimi sikukosa, lakini Mungu ananinyima shauri lililo sawa.[#Iy. 27:2; 33:9.]
6Ingawa sikukosa, napewa uwongo, kidonda, mshale wake ulichonipiga, hakiponi, tena hakuna kiovu, nilichokifanya.[#Iy. 6:4; 9:15,20.]
7Mtu aliye kama Iyobu yuko wapi? Masimango ya kwake yakichuruzika kama maji ya kunywa,[#Iy. 15:16.]
8akifanya bia nao wafanyao maovu, akitembea na watu wasiomcha Mungu?[#Sh. 1:1.]
9Kwani amesema: Hakuna mafaa, mtu anayojipatia kwa kupendezana naye Mungu.[#Iy. 9:22.]
10Kwa hiyo nisikilizeni, ninyi waume mlio wenye akili! Mungu asiwaziwe kamwe ya kwamba: Hufanya maovu, wala Mwenyezi ya kwamba: Hufanya mapotovu!
11Ila humlipisha mtu matendo yake, aone yaupasayo mwenendo wake.[#Rom. 2:6.]
12Hii ni kweli, Mungu hafanyi maovu, wala Mwenyezi hayapotoi mashauri yaliyo sawa.[#Iy. 19:6.]
13Kuiangalia nchi hii alimwagiza nani? Au yuko nani aliyeuweka huu ulimwengu wote?
14Kama angeuelekeza moyo wake kuyaangalia yamfaliayo mwenyewe, au kama angeirudisha kwake roho na pumzi yake,
15wote wenye miili yenye nyama wangezimia kwa mara moja, nao watu wangerudi kuwa mavumbi tena.[#1 Mose 3:19; Sh. 104:29.]
16Kama uko na utambuzi, yasikilize haya! Itegee sauti ya maneno yangu masikio yako!
17Je? Achukizwaye na mashauri yaliyo sawa anaweza kutawala? Au mkuu aongokaye utamwazia kuwa mwovu?
18Utamwambia mfalme: Hufai kitu? au wakuu: M waovu?
19Naye Mungu hazipendelei nyuso za wakuu, wala hawatazami wenye nguvu kuliko wanyonge, kwani wote ni viumbe vya mikono yake.
20Punde si punde, mara watu hufa, usiku wa manane hupepesuka, kisha huenda zao, nao wenye nguvu huondolewa pasipo kushikwa mikono.
21Kwani macho yake huziangalia njia za watu, nyayo zao zinapokanyaga, hupaona pote.[#Iy. 31:4; Fano. 5:21.]
22Hapapatikani penye giza kabisa wala kivuli chenye weusi, wapate kujificha mlemle wafanyao maovu.[#Sh. 139:11-12.]
23Kwani Mungu hamwangalii mtu mara kwa mara akimtaka, aje kwake kukatwa shauri.
24Huvunja wenye nguvu pasipo kuwachunguzachunguza, akaweka wengine mahali pao.
25Kwani anazijua kazi zao, zilivyo kweli, akawakumba usiku, wapondwe.
26Kwa kuwa ni waovu, huwapiga mahali palipo na watu wanaovitazama.
27Ni kwa sababu waliacha kumfuata, nazo njia zake zote hawakuziangalia, wazishike.
28Huko ni kuwatwika vilio vyao wakorofikao, navyo vilio vya wanyonge, alivyovisikia.[#2 Mose 22:23.]
29Akiwanyamazisha hivyo, yuko nani atakayemwambia: Unafanya nini? Akiuficha uso wake, yuko nani awezaye kumwona? Njia yake ya kuwaendea wote ni hiyo moja, wao walio mataifa mazima naye mtu aliye peke yake.
30Huku ni kwamba: Mtu mpotovu asiwe mfalme, asigeuke kuwa tanzi la kutegea watu.
31Je? Mungu anaambiwa: Nalipishwa, lakini sikukosa?
32Kama yako, nisiyoyaona, nifundishe wewe! Kama nilifanya mapotovu, sitayafanya tena?[#Iy. 40:5.]
33Je? Kama inavyokupendeza wewe, ndivyo alipishe? Unavikataaje? Ni wewe upaswaye kuchagua malipo, siye yeye? Haya! Yaseme unayoyajua!
34Watu wenye akili wataniambia pamoja na waume walio werevu wa kweli wanaonisikia:
35Iyobu aliyoyasema siyo ya ujuzi, kweli maneno yake siyo ya mtu mwenye akili.[#Iy. 38:2.]
36Basi, kwa hiyo Iyobu na ajaribiwe kale na kale, kwani kama watu waovu wanavyojibu, ndivyo, anavyojibu naye.
37Kwani makosa yake anayaongeza na kufanya maovu, akitupigia makofi machoni petu, tena akimgombeza Mungu kwa kusema kwake.[#Iy. 34:5.]
Elihu akajibu tena akisema: