Iyobu 35

Iyobu 35

1Je? Hayo unayawaza kuwa shauri likupasalo,[#Iy. 32:2.]

2ukisema: Mimi ni mwenye wongofu kuliko Mungu?

3tena ukiuliza, kama huo wongofu utakupatia faida gani, tena ukisema: Nikiacha kukosa, inafaaje kuliko kukosa?[#Iy. 34:9.]

4Mimi nitakujibu wewe nao wenzako walioko kwako:

5Zitazame mbingu, upate kuona! Yaangalie mawingu yaliyoko huko juu kichwani pako!

6Yule unamtendea nini ukikosa? Mapotovu yako yakiwa mengi, unamfanyizia nini?[#Iy. 7:20.]

7Yule unampa nini usipokosa? Au liko, atakalolichukua mkononi mwako?[#Rom. 11:35.]

8Uovu wako utaweza kumwumiza mtu tu aliye kama wewe, nao wongofu wako utaweza kumfalia mwana wa Adamu.

9Kwa wingi wa mateso watu hulia, kwa kutolewa nguvu na wakuu hupiga makelele.

10Lakini hakuna aulizaye: Yuko wapi Mungu aliyeniumba? Siye anayeniimbisha hata usiku?[#Sh. 42:9; Tume. 16:25.]

11Atufundishaye kuliko nyama wa porini siye yeye? Tena siye yeye atuerevushaye kuliko ndege wa angani?

12Lakini asipojibu, wanapomlilia, ni kwa ajili ya majivuno yao walio wabaya.

13Vilio vya bure Mungu havisikii, aliye Mwenyezi haviangalii.[#Yoh. 9:31.]

14Ikiwa, unasema nawe, ya kama humwoni, hilo shauri liko kwake, wewe umngoje tu![#Iy. 23:8-9.]

15Makali yake yasipotokea hata sasa, huwaziwa kuwa hajui kabisa, mtu akikorofishwa.[#Mbiu. 8:11.]

16Naye Iyobu amekifunua kinywa chake, vikawa vya bure, amesema maneno mengi ya mambo, asiyoyajua.

Elihu anasema mara ya nne: Mungi ni mkuu peke yake.

Elihu akajibu tena akisema:

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania