The chat will start when you send the first message.
1Ndipo, Bwana alipomjia Iyobu akiwa mwenye upepo wa kuvuma na nguvu, akasema:[#Iy. 31:35.]
2Ni nani huyu ayatiaye giza matengenezo yangu akijisemea maneno yakosayo ujuzi?[#Iy. 34:35.]
3Haya! Jifunge viuno vyako kama mtu wa kiume! Kisha nitakuuliza, unijulishe mambo.[#Iy. 40:7.]
4Nilipoiweka misingi ya nchi, ulikuwa wapi? Kama unajua utambuzi, ieleze!
5Ni nani aliyeviweka vipimo vyake? Sema, kama unavijua! Au ni nani aliyeipima kwa kamba ya kupimia?[#Fano. 30:4.]
6Misingi yake ilikochimbiwa, ndiko wapi? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,
7zilipopiga shangwe nyota za mapema zote pamoja, nao wote waliokuwa wana wa Mungu walipopiga vigelegele?
8Ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, ilipotoka tumboni mwa nchi kwa kufurika?
9Nilipoipatia mawingu kuwa mavazi yake ka kungu jeusi kuwa nguo zake za kujitandia?
10Nilipoipinga kwa kuishurutisha kuyafuata maongozi yangu, napo nilipoiwekea makomeo na milango kuwa mipaka?[#Fano. 8:29.]
11Nilipoiambia: Ufike mpaka hapa, usipapite! Ndipo, mawimbi yako yenye majivuno yatakapokomea?[#Sh. 104:8-9.]
12Tangu hapo, siku zako zilipoanza, uliagiza, kuche, ukayajulisha mapambazuko mahali pao pa kutokea,
13yapate kuyashika mapeo ya nchi, waovu wafukuzwe, waitoke nchi?
14Hapo nchi hugeuka kama udongo, ukichorwa marembo, vyote vikijipanga kuwa kama mavazi yake mazuri mno.
15Lakini wanaonyimwa mwanga wao ndio waovu, nayo mikono iliyokunjuliwa kwa majivuno huvunjwa.
16Penye matokeo ya bahari ulipafika? Ukatembea humo ndani ya bahari mlimo na vilindi?
17Malango ya kifo yakafunguka mbele yako? Nayo malango ya kuzimu ukayaona?
18Ukapata kuutambua nao upana wa nchi? Kama unaujua wote, haya! Ueleze!
19Njia ya kwenda huko, mwanga unakokaa, iko wapi? napo mahali pake giza pako wapi?
20Unaweza kuisindikiza, uipeleke kwake? Njia za kwenda nyumbani kwake unazijua?
21Kweli unazijua! Kwani hapo ulikuwa umekwisha kuzaliwa, nayo hesabu ya siku zako ni kubwa!
22Penye vilimbiko vya theluji ulipafika? Navyo vilimbiko vya mvua ya mawe uliviona?
23Siku za masongano ndizo, nilizoviwekea, hata siku ya magombano nayo ya mapigano.[#Yos. 10:11.]
24Njia ya kwenda hapo, mwanga unapogawanyika, iko wapi? Upepo wa maawioni kwa jua unatoka wapi, uenee juu ya nchi?
25Ni nani azichimbiaye mvua mifereji, zikifurika? Tena ni nani, auelekezeaye umeme njia yake, ukinguruma?[#Iy. 28:26.]
26Ni nani ainyesheaye mvua hiyo nchi isiyokaa watu, nako kusikopatikana wana wa Adamu, kule nyikani?
27Ni nani atakayelishibisha jangwa napo palipo patupu kabisa, apachipuze na kuotesha majanijani?
28Je? Baba ya mvua yuko wapi? Ayazaaye matone ya umande ni nani?
29Tumboni mwa nani ndimo, barafu inamotoka? Tena ni nani auzaaye umande wa theluji, utoke mbinguni?[#Sh. 147:16.]
30Ni kazi ya nani, maji yakipata mafuniko kama ya mawe, nayo maji ya vilindi yakishikamana huko juu kwa kugandamanishwa?
31Je? Mafungo ya zile nyota saba za Kilimia unaweza kuyafunga? au kuyafungua mapingu yao zile nyota tatu za Choma, nikuchome?[#Iy. 9:9.]
32Je? Utazitoa nyota za Mviringo wa Nyama kila moja wakati wake? au zile za Gari na za watoto wake utaziongoza?
33Je? Maongozi ya mbinguni unayajua? au ni wewe unayezipa nchi hii, ziitawale?
34Je? Unaweza kuzipaza sauti zako, zifike mawinguni, uite mvua yenye maji mengi, ije kukufunika?
35Je? Unaweza kuutuma umeme, uende mahali fulani, kisha ukuambie: Mimi hapa! Nimerudi!
36Ni nani afanyaye yenye ujuzi kama hayo pasipo kujulikana? Au ni nani ayatambulishaye kwao wayachunguzao?
37Ni nani awezaye kuyahesabu mawingu, asipotelewe? Au ni nani awezaye kuvimwaga viriba vya mbinguni,[#1 Mose 7:11.]
38mavumbi yashikamane kuwa udongo wa chepechepe, nayo mengine yageuke kuwa matope yagandamanayo?
39Je? Unaweza kumpokonya simba mke nyama, aliyemrarua? Au unaweza kuikomesha njaa ya wana wa simba,
40wakiwa mapangoni mwao, waotame, au wakikaa mafichoni na kuvizia?[#Iy. 37:8.]
41Ni nani awapatiaye makunguru vilaji vyao, wana wao wakimlilia Mungu na kutangatanga kwa kukosa chakula?[#Sh. 147:9.]