The chat will start when you send the first message.
1Je? Unajua wakati, minde wanapozalia, au umeangalia, majike ya kulungu wanapopatia mimba?
2Miezi yao ya kuwa wenye mimba umekwisha kuihesabu? Tena unajua wakati, wanapozalia?
3Huchutama, kisha huwazaa watoto wao, huko ndiko kuukomesha uchungu wao.
4Watoto wao hupata nguvu kwa kukua penye mapori matupu; wakijiendea na kutoka kwao hawarudi tena.
5Ni nani aliyewatuma punda milia kujiendea tu? au ni nani aliyeyafungua mafungo yao vihongwe?
6Si mimi niliyewapa nyika kuwa nyumba zao nalo jangwa la chumvi kuwa makao yao?
7Wao huyacheka makelele yaliyomo mijini, maana hawazisikii tena sauti za ukorofi za wasimamizi.
8Milimani ndiko, wanakojionea malisho yao, vijani vibichi vyote huvifuatafuata.
9Je? Nyati atapendezwa akikutumikia? Atatafuta kilalo cha kuwamo zizini mwako?
10Je? Unaweza kumfunga nyati kwa kamba, akulimie matuta, akikufuata na kulivuta jembe mabondeni pako?
11Kwa kuwa nguvu zake ni nyingi, unaweza kumwegemea, umwachie kazi zako za shambani?
12Atayapeleka mazao yako nyumbani, ukimtegemea hivyo? Au yaliyomo chanjani mwako atayakusanya vema?
13Mabawa ya mbuni huchezacheza, lakini je? Hayo mabawa na manyoya yake yako na upole?
14Kwani mayai yake huyaacha hapo mchangani, huo mchanga uyaangue kwa joto lake;
15husahau, ya kama labda mguu utapapita utakaoyakanyaga, au nyama wa porini atayapondaponda.
16Watoto wake huwakuza kwa ukali, kama sio wake, haogopi kwamba: Labda hautafaa huo utunzaji wake.
17Kwani Mungu humsahaulisha werevu wa kweli, wala hakumgawia utambuzi wo wote.
18Lakini anapoyapigapiga mabawa yake, aondoke, humcheka naye farasi pamoja naye ampandaye.
19Je? Ni wewe uliyempa farasi nguvu zake kubwa? Je? Ni wewe uliyemvika singa za shingoni?
20Je? Ni wewe unayemtuma, aogopeshe watu akiruka kwa mara moja kama nzige na kufoka sana?
21Huparapara bondeni akizifurahia nguvu zake, hutoka kwenda kukutana nao washikao mata.
22Hucheka waoga, maana hastuki, wala penye panga harudi nyuma.
23Podo hupiga kelele juu yake, nayo mikuki imetukayo pamoja na chembe za mishale.
24Akichafuka kwa ukali humeza nchi, baragumu likilia, hasimami,
25ila kila anapolisikia baragumu husema: Haya! Toka mbali hunusa, mapigano yaliko, akiyasikia matangazo ya wakuu na makelele ya vikosi.
26Je? Ni kwa utambuzi wako kipanga akiruka angani na kuyanyosha mabawa yake kwenda kusini?
27Au ni kwa agizo lako, tai akipaa juu sana na kujitengenezea kiota cha mahali palipo juu?
28Hutua penye miamba, apate kulala magengeni juu; ngome yake ilipo, ndipo papo hapo.
29Toka huko juu huchungulia akitafuta chakula, macho yake huyaona nayo yaliyoko mbali.
30Makinda yake hufyonza damu, napo panapo nyamafu yupo hapo.[#Hab. 1:8; Mat. 24:28.]
Bwana akamjibu Iyobu akisema: