The chat will start when you send the first message.
1Hili ndilo neno la Bwana lililomjia Yoeli, mwana wa Petueli: Yasikieni haya, ninyi wazee!
Yasikilizeni, ninyi nyote mkaao katika nchi hii!
2Je? Kama hayo yamefanyika katika siku zenu
au katika siku za baba zenu?
3Yasimulieni haya wana wenu!
Nao wana wenu wayasimulie wana wao!
Nao wana wao wayasimulie uzao mwingine ujao!
4Panzi waliyoyasaza yameliwa na nzige,
nzige waliyoyasaza yameliwa na funutu,
funutu waliyoyasaza yameliwa na bumundu.
5Levukeni, ninyi walevi, kalieni!
Pigeni kelele, nyote mnywao mvinyo!
Ni kwa ajili ya mvinyo mbichi,
kwa kuwa zimekwisha kuondolewa vinywani mwenu!
6Kwani liko kabila, limepanda kuiingia nchi yangu,
ni lenye nguvu, tena halihesabiki,
meno yao kama meno ya simba, magego yao kama ya simba jike.
7Wameigeuza mizabibu yangu, iwe kama jangwa,
nayo mikuyu yangu, iwe mashina matupu,
wameyabandua maganda yao, wakayatupa chini,
matawi yao yakawa meupe kabisa.
8Ombolezeni kama mwanamwali aliyejivika gunia
kwa ajili ya bwana wa ujana wake!
9Vilaji na vinywaji vya tambiko vimekomeshwa,
visifike Nyumbani mwa Bwana;
kwa hiyo watambikaji wanasikitika, ndio wanaomtumikia Bwana.
10Mashamba yameangamizwa, nchi imesikitika,
kwani ngano zimeangamia, mvinyo mpya zimekupwa,
mafuta nayo yamefifizwa.
11Wakulima wametwezwa, watunza mizabibu wanalia,
kwa ajili ya ngano na ya mawele,
kwani ngano zimeangamia, mvinyo mpya zimekupwa,
mafuta nayo yamefifizwa.
Wakulima wametwezwa, watunza mizabibu wanalia,
kwa ajili ya ngano na ya mawele,
kwani mavuno ya mashamba yamepotea.
12Mizabibu imekauka, mikuyu imefifia,
mikomamanga na mitende na michungwa,
miti yote pia ya shambani imekauka,
kweli nazo furaha zimekaukiana, zimewapotelea watu.
13Vaeni nguo za matanga! Ombolezeni, ninyi watambikaji!
Pigeni kelele, mnaotumikia mezani pa kutambikia!
Njoni, mlale usiku kucha na kuvaa magunia,
mnaomtumikia Mungu wangu!
Kwani Nyumba ya Mungu wenu imenyimwa
vilaji na vinywaji vya tambiko!
14Eueni mfungo! Utangazeni mkutano!
Wakusanyeni wazee nao wote wanaokaa katika nchi hii,
waje Nyumbani mwa Bwana Mungu wenu, mmlalamikie Bwana!
15Semeni: Imetupata ile siku! Kweli siku ya Bwana iko
karibu!
Inakuja kama mwangamizo utokao kwake Mwenyezi!
16Je? Chakula hakikuondolewa machoni petu?
Nyumbani mwa Mungu wetu hamkuondoka furaha na shangwe?
17Mbegu zimenyauka chini ya madongo yao,
vilimbiko vimetoweka, vyanja vimebomolewa,
kwani ngano zimekauka!
18Sikilizeni! Nyama nao wanapiga kite!
Makundi ya ng'ombe yametatizwa, kwani hakuna malisho yao,
nayo makundi ya kondoo yanakosa.
19Wewe Bwana, ninakulilia, kwani moto umezila mbuga za
nyikani,
moto wenye miali umeichoma miti yote ya porini.
20Nao nyama wa porini wanakutwetea
kwani vijito vya maji vimekauka,
nao moto umezila mbuga za nyikani.