Yona 3

Yona 3

Waniniwe wanajutishwa na Yona.

1Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili kwamba:[#Yona 1:2.]

2Ondoka, uende katika mji ule mkubwa wa Niniwe, uutangazie utume, nitakaokuambia!

3Ndipo, Yona alipoondoka, akaenda Niniwe, kama Bwana alivyomwagiza. Niniwe ulikuwa mji mkubwa machoni pa Mungu; kuupita kati ulikuwa mwendo wa siku tatu.[#Yona 4:11.]

4Yona akaanza kuingia mjini mwendo wa siku moja, akapiga mbiu kwamba: Zingaliko siku 40; zitakapopita, mji wa Niniwe utabomolewa.

5Ndipo, watu wa Niniwe walipomtegemea Mungu, wakatangaza, watu wafunge mfungo, wakavaa magunia wote, wakubwa mpaka wadogo.[#Mat. 12:41.]

6Habari ya mambo hayo ikafika hata kwa mfalme wa Niniwe, naye akaondoka katika kiti chake cha kifalme, akalivua vazi lake la kifalme, akavaa gunia, akajikalisha majivuni.

7Kisha akatangaza mbiu mle Niniwe ya kwamba: Kwa amri ya mfalme na ya wakuu wake yanaagizwa haya: Watu na nyama, kama ni ng'ombe au kondoo, wasionje kitu cho chote, wasile, wala maji tu wasinywe!

8Ila wajivike magunia, watu nao nyama, wakaze kumlilia Mungu! Kisha kila mtu arudi katika njia yake mbaya na kuyaacha makorofi yaliyomo mikononi mwake!

9Labda ndivyo, Mungu atakavyogeuza moyo, ayaache makali yake yenye moto, tusiangamie.[#Yoe. 2:14.]

10Mungu alipoyaona matendo yao, ya kuwa wamerudi katika njia zao mbaya, ndipo, Mungu alipogeuza moyo, akaacha kuyafanya yale mabaya, aliyoyasema, ya kuwa atawafanyizia; hakuyafanya.[#Yer. 18:7-8.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania