Yosua 1

Yosua 1

Yosua anatiwa nguvu na Mungu.

1Mose, mtumishi wa Bwana, alipokwisha kufa, ndipo, Bwana alipomwambia Yosua, mwana wa Nuni, mtumishi wake Mose, kwamba:

2Mtumishi wangu Mose amekwisha kufa; sasa ondoka, uuvuke huu Yordani, wewe na watu wote wa ukoo huu, mwiingie nchi hiyo, mimi nitakayowapa wana wa Isiraeli.[#5 Mose 34:5.]

3Kila mahali, nyayo za miguu yenu zitakapopakanyaga, nitawapa ninyi, kama nilivyomwambia Mose.[#5 Mose 11:24.]

4Kutoka nyikani na huko Libanoni mpaka kwenye lile jito kubwa, lile jito la Furati, nchi yote nzima ya Wahiti, tena mpaka kwenye Bahari Kubwa iliyoko upande wa machweoni kwa jua; huko ndiko, mpaka wenu utakakokuwa.

5Siku zote, utakazokuwapo, hatakuwako mtu atakayesimama mbele yako. Kama nilivyokuwa na Mose, vivyo hivyo nitakuwa na wewe, sitakuepuka, wala sitakuacha.[#5 Mose 31:8; Ebr. 13:5.]

6Jipe moyo, upate nguvu! Kwani wewe utawapeleka watu hawa, waichukue nchi hiyo, niliyowaapia baba zenu kuwapa.[#5 Mose 3:28; 31:7,23.]

7Ni hii tu: Jipe moyo, upate nguvu sana za kuyaangalia na kuyafanya Maonyo yote, mtumishi wangu Mose aliyokuagiza! Usiyaache kupitia kuumeni wala kushotoni, upate kujua njia ya kweli po pote, utakapokwenda.[#5 Mose 5:32; 1 Fal. 2:3.]

8Kitabu cha Maonyo haya kisiondoke kinywani mwako, ila uyawaze moyoni mchana na usiku, upate kuyaangalia na kuyafanya yote yaliyoandikiwa humo, kwani ndivyo, utakavyofanikiwa katika njia zako kwa kuzijua zitakazokuwa za kweli.[#Sh. 1:2-3.]

9Sukukuagiza kujipa moyo, upate nguvu? Usiogope, wala usiingiwe na vituko! Kwani Bwana Mungu wako yuko pamoja na wewe po pote, utakapokwenda.

Watu wanaagana na Yosua kumtii.

10Yosua akawaagiza wenye amri ya watu kwamba:

11Piteni makambini po pote, mwaagize watu kwamba: Jitengenezeeni pamba za njiani! Kwani baada ya siku tatu mtauvuka huu Yordani kwenda kuichukua hiyo nchi, Bwana Mungu wenu atakayowapa ninyi, mwichukue, iwe yenu.

12Nao Warubeni na Wagadi na nusu ya watu wa shina la Manese Yosua akaanza kuwaambia kwamba:

13Likumbukeni lile neno, Mose, mtumishi wa Bwana, alilowaagiza kwamba: Bwana Mungu enu atawapatia kutulia na kuwapa ninyi nchi hii.[#4 Mose 32:20.]

14Wake na watoto na nyama wenu wa kufuga watakaa katika nchi hii, Mose aliyowapa ninyi ng'ambo hii ya Yordani; lakini ninyi nyote mlio mafundi wa vita wenye nguvu mtashika mata, mvuke na kuwatangulia ndugu zenu, mwasaidie.

15Tena hapo, Bwana atakapowapatia nao ndugu zenu kutulia kama ninyi, nao waichukue hiyo nchi, Bwana Mungu wenu watakavyowapa, iwe yao, ndipo, mtakaporudi katika nchi iliyo yenu wenyewe, mwichukue, iwe yenu kweli, ni hii, Mose, mtumishi wa Bwana, aliyowapa ninyi ng'ambo hii ya Yordani upande wa maawioni kwa jua.

16Wakamjibu Yosua kwamba: Yote, uliyotuagiza, tutayafanya, napo po pote, utakapotutuma, tutakwenda.

17Kama tulivyomsikia Mose katika mambo yote, hivyo tutakusikia hata wewe. Tunataka tu, Bwana Mungu wako awe na wewe, kama alivyokuwa na Mose.

18Kila mtu atakayekupingia, ukisema neno, asiyasikie maneno yako yote, utakayotuagiza, atauawa. Jipe moyo, upate nguvu![#Yos. 1:6.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania