Yosua 12

Yosua 12

Wafalme thelathini na mmoja walioshindwa na Waisiraeli.

1Hawa ndio wafalme wa nchi hii, wana wa Israeli waliowapiga, walipoichukua nchi yao, iwe yao wenyewe ng'ambo ya huko ya Yordani upande wa maawioni kwa jua toka mto wa Arnoni mpaka milimani kwa Hermoni, nayo nyika hiyo yote iliyoko upande wa maawioni kwa jua:

2Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekaa Hesiboni na kutawala toka Aroeri ulioko kwenye mto wa Arnoni kuanzia mle mtoni katikati kufikia nusu ya Gileadi mpaka mto wa Yaboko, mpaka wa wana wa Amoni uliko.[#4 Mose 21:24.]

3Aliitawala nayo nyika kufikia upande wa maawioni kwa jua wa bahari ya Kineroti mpaka upande wa maawioni kwa jua wa bahari ya nyikani, ndiyo Bahari ya Chumvi, ukifuata njia ya kwenda Beti-Yesimoti, tena kusini chini ya matelemko ya Pisiga.

4Tena mipaka ya Ogi, mfalme wa Basani, aliyekuwa wa masao ya wale Majitu; naye alikuwa anakaa Astaroti na Edirei;[#4 Mose 21:33; 5 Mose 3:11.]

5aliitawala milima ya Hermoni na Salka na Basani yote mpaka kwenye mipaka ya Wagesuri na ya Wamakati na nusu ya Gileadi mpaka kwenye mipaka ya Sihoni, mfalme wa Hesiboni.

6Mose, mtumishi wa Bwana, na wana wa Isiraeli waliwapiga, nazo nchi zao Mose, mtumishi wa Bwana, akazigawia wao wa Rubeni na wa Gadi nao walio nusu ya shina la Manase, ziwe nchi zao.[#4 Mose 32:33.]

7Nao hawa ndio wafalme, Yosua na wana wa Isiraeli waliowapiga ng'ambo ya huku ya Yordani inayoelekea baharini toka Baali-Gadi ulioko katika bonde la Libanoni mpaka kwenye ile milima mitupu inayoendelea hata Seiri; nchi hiyo Yosua akaigawia mashina ya Waisiraeli, iwe yao wenyewe, kama walivyogawanyika,

8wakae milimani na katika nchi ya tambarare na nyikani, hata kwenye matelemko na mbuga, nako kusini kwao Wahiti na Waamori na Wakanaani na Waperizi na Wahiwi na Wayebusi:[#Yos. 11:3.]

9Mfalme wa Yeriko mmoja, mfalme wa Ai ulioko upande wa Beteli mmoja,[#Yos. 6:2; 8:29.]

10mfalme wa Yerusalemu mmoja, mfalme wa Heburoni mmoja,[#Yos. 10:1,3.]

11mfalme wa Yarmuti mmoja, mfalme wa Lakisi mmoja,

12mfalme wa Egloni mmoja, mfalme wa Gezeri mmoja,[#Yos. 10:3,26,33,39; Amu. 1:11.]

13mfalme wa Debiri mmoja, mfalme wa Gederi mmoja,

14mfalme wa Horma mmoja, mfalme wa Aradi mmoja,[#Amu. 1:17; 4 Mose 21:1.]

15mfalme wa Libuna mmoja, mfalme wa Adulamu mmoja,[#Yos. 10:29-30.]

16mfalme wa Makeda mmoja, mfalme wa Beteli mmoja,[#Yos. 10:28.]

17mfalme wa Tapua mmoja, mfalme wa Heferi mmoja,

18mfalme wa Afeki mmoja, mfalme wa Saroni mmoja,[#Yos. 15:53; 1 Sam. 4:1.]

19mfalme wa Madoni mmoja, mfalme wa Hasori mmoja,[#Yos. 11:1,10.]

20mfalme wa Simuroni-Meroni mmoja, mfalme wa Akisafu mmoja,[#Yos. 11:1.]

21mfalme wa Taanaki mmoja, mfalme wa Megido mmoja,

22mfalme wa Kedesi mmoja, mfalme wa Yokinamu wa Karmeli mmoja,

23mfalme wa Dori milimani kwa Dori mmoja, mfalme wa makabila ya Gilgali mmoja,[#Yos. 11:2.]

24mfalme wa Tirsa mmoja, wafalme hawa wote ni 31.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania