The chat will start when you send the first message.
1Shina la wana wa Yuda kura ikalipata nchi za kuzigawanyia koo zao kwenye mpaka wa Edomu; mpaka wao wa kusini uliipita nyika ya Sini iliyokuwa mwisho wa upande wa kusini.[#4 Mose 34:3-5.]
2Huo mpaka wao wa upande wa kusini ulianzia mwishoni kwa Bahari ya Chumvi kwenye pembe yake ielekeayo kusini.
3Kutoka kule kusini ulipita hapo pa kukwelea Akarabimu, ulipitia Sini, ulipanda tena upande wa kusini wa Kadesi-Barnea, ulipita Hesironi na kupanda tena Adari, ulizungukia Karka,
4ulifika Asimoni, kisha ulitokea kwenye mto wa Misri, mwisho ulitokea baharini. Huu ndio mpaka wenu wa kusini.
5Mpaka wa upande wa maawioni kwa jua ni Bahari ya Chumvi kuufikia mwisho wa Yordani. Nao mpaka wa upande wa kaskazini ulianzia hapo pembeni kwa bahari kwenye mwisho wa Yordani.
6Kutoka huko mpaka ulipanda Beti-Hogla, ulipitia Beti-Araba upande wake wa kaskazini, kisha mpaka uliupanda mwamba wa Bohani, mwana wa Rubeni.[#Yos. 18:17.]
7Kutoka Bondeni kwa Akori mpaka ulipanda Debiri, uligeukia kaskazini kufika Gilgali unaoelekea hapo pa kukwelea Adumimu ulioko kusini kwenye kijito; kisha mpaka ulipita penye maji ya Eni-Semesi na kutokea Eni-Rogeli (Chemchemi ya Wafua nguo).[#2 Sam. 17:17.]
8Kisha mpaka ulipanda katika bonde la Mwana wa Hinomu kufika kando kwao Wayebusi upande wao wa kusini, ni huko Yerusalemu; kisha mpaka ulipanda kufika juu ya mlima ulioko mbele ya Bonde la Hinomu upande wa baharini mwishoni kwa Bonde la Majitu upande wake wa kaskazini.[#2 Mambo 28:3.]
9Toka juu ya mlima huo mpaka uliendelea, ufike kwenye chemchemi ya maji ya Nefutoa, utokee kwenye miji ya mlima wa Efuroni; uliendelea tena kufika Bala, ndio Kiriati-Yearimu.[#Yos. 15:60.]
10Huko Bala mpaka uligeukia tena upande wa baharini kuufikia mlima wa Seiri, tena ulipita kando ya mlima wa Yearimu upande wake wa kaskazini, ndio Kesaloni; toka huko ulishuka Beti-Semesi, ufike Timuna.
11Toka huko mpaka uliendelea kando ya Ekroni upande wa kaskazini, kisha uliendelea kufika Sikroni, uliupita mlima wa Bala, utokee Yabuneli, nao mwisho wake mpaka ulikuwa hapo, ulipotokea baharini.
12Nao mpaka wa upande wa baharini ulikuwa Bahari Kubwa na nchi yake ya pwani. Hii ilikuwa mipaka ya kuzizunguka nchi za wana wa Yuda za kuzigawanyia koo zao.
(13-19: Amu. 1:10-15.)13Kalebu, mwana wa Yefune, akampa fungu katikati ya wana wa Yuda, liwe lake kwa hivyo, Bwana alivyomwambia Yosua; ni mji wa Arba, baba yao Waanaki, ndio Heburoni.[#Yos. 14:6-15.]
14Huko Kalebu akafukuza wana watatu wa Anaki, Sesai na Ahimani na Talmai, waliozaliwa na Anaki.
15Toka huko akawaendea wenyeji wa Debiri, nalo jina la Debiri lilikuwa kale Kiriati-Seferi.
16Hapo Kalebu akasema: Atakayeupiga Kiriati-Seferi na kuuteka nitampa mtoto wangu Akisa kuwa mkewe.
17Otinieli, mwana wa Kenazi, ndugu yake Kalebu, alipouteka, akampa mtoto wake Akisa kuwa mkewe.
18Ikawa, huyu alipofikia kwake akamhimiza mumewe kuomba shamba kwa baba yake Kalebu; basi, Akisa aliposhuka katika punda, Kalebu akamwuliza: Unataka nini?
19Naye akamwambia: Nipe tunzo la kunibariki! Kwa kuwa umenipeleka katika nchi ya kusini, nipe nazo mboji za maji! Ndipo, alipompa zile mboji zilizokuwa upande wa juu, nazo zilizokuwa upande wa chini.
20Hizi ndizo nchi za shina la wana wa Yuda za kuzigawanyia koo zao, ziwe mafungu yao:
21kwenye mwisho wa nchi ya shina la wana wa Yuda kuuelekea mpaka wa Edomu upande wa kusini kulikuwa na miji hii: Kabuseli na Ederi na Yaguri,
22na Kina na Dimona na Adada,
23na Kedesi na Hasori na Itinani,
24Zifu na Telemu na Baloti,
25na Hasori-Hadata na Kerioti-Hesironi, ndio Hasori.
26Amamu na Sema na Molada,
27na Hasari-Gada na Hesimoni na Beti-Peleti,
28na Hasari-Suali na Beri-Seba na Biziotia,
29Bala na Iyimu na Esemu,
30na Eltoladi na Kesili na Horma,
31na Siklagi na Madimana na Sanisana,
32Lebaoti na Silihimu na Aini na Rimoni; miji hii yote pamoja ni 29 pamoja na mitaa yao.
33Katika nchi ya tambarare: Estaoli na Sora na Asina,
34na Zanoa na Eni-Ganimu, Tapua na Enamu,[#Amu. 13:25; 16:31.]
35Yarmuti na Adulamu, Soko na Azeka,
36na Saraimu na Aditaimu na Gedera na Gederotaimu; ni miji 14, pamoja na mitaa yao.
37Senani na Hadaa na Migidali-Gadi,
38na Dilani na Misipe na Yokiteli,
39Lakisi na Boskati na Egloni,
40na Kaboni na Lamasi na Kitilisi,
41na Gederoti, Beti-Dagoni na Nama na Makeda; ni miji 16 pamoja na mitaa yao.
42Libuna na Eteri na Asani,
43Ifuta na Asina na Nesibu,
44na Keila na Akizibu na Maresa; ni miji 9 pamoja na mitaa yao.
45Ekroni na vijiji vyake na mitaa yake.
46Toka Ekroni upande wa baharini miji yote iliyoko kando ya Asdodi pamoja na mitaa yao.[#1 Sam. 5:10.]
47Asdodi na vijiji vyake na mitaa yake, Gaza pamoja na vijiji vyake na mitaa yake mpaka kwenye mto wa Misri, nao mpaka wake ni Bahari Kubwa.[#1 Sam. 5:1; Amu. 1:18; 4 Mose 34:6.]
48Tena milimani: Samiri na Yatiri na Soko,
49na Dana na Kiriati-Sana, ndio Debiri,
50na Anabu na Estemo na Animu,
51na Goseni na Holoni na Gilo; ni miji 11 pamoja na mitaa yao.
52Arabu na Duma na Esani,
53Yanumu na Beti-Tapua na Afeka,
54na Humuta na Kiriati-Arba, ndio Heburoni, na Siori; ni miji 9 pamoja na mitaa yao.
55Maoni, Karmeli na Zifu na Yuta,
56na Izireeli na Yokidamu na Zanoa,
57Kaini, Gibea na Timuna; ni miji 10 pamoja na mitaa yao.
58Halihuli, Beti-Suri na Gedori,
59na Marati na Beti-Anoti na Eltekoni; ni miji 6 pamoja na mitaa yao.
60Kiriati-Baali, ndio Kiriati-Yearimu, na Raba; ni miji 2 pamoja na mitaa yao.[#Yos. 9:17; 18:14.]
61Nyikani: Beti-Araba, Midini na Sekaka,
62na Nibusani na Mji wa Chumvi na Engedi ni miji 6 pamoja na mitaa yao.
63Lakini Wayebusi, ndio wenyeji wa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwafukuza; kwa hiyo Wayebusi wakakaa pamoja na wana wa Yuda mle Yerusalemu mpaka siku hii ya leo.[#Yos. 18:28; 2 Sam. 5:6.]