Yosua 20

Yosua 20

Miji sita ya kuponea kisasi cha kuuawa.

1Kisha Bwana akamwambia Yosua kwamba:[#4 Mose 35:6-29.]

2Waambie wana wa Isiraeli kwamba: Jipatieni ile miji ya kuikimbilia, niliyowaambia kinywani mwa Mose,

3mwuaji apate kuikimbilia, kama hakumpiga mwenziwe na kumwua kwa kusudi wala kwa kujua, mpate kuikimbilia na kumkimbia atakayeilipiza hiyo damu.

4Kama anakimbilia mmojawapo hiyo mji, asimame pa kuliingilia lango la mji na kusema masikioni pa wazee wa miji huo manza zake, alizozikora, kisha sharti wampokee mjini mwao na kumpa mahali pa kukaa kwao.

5Kama mwenye kuilipiza ile damu anamfuata upesi, wasimtoe yule mwuaji na kumtia mkononi mwake, kwa kuwa alimpiga mwenziwe pasipo kujua, wala hakumchukia tangu kale.

6Naye atakaa humo mjini, mpaka atakaposimamishwa mbele ya mkutano, apate kuhukumiwa, tena mpaka mtambikaji mkuu wa siku zile atakapokufa, kisha yule mwuaji atapata kurudi na kuingia mjini kwao na nyumbani mwao mlemle mjini, alimotoka na kukimbia.

7Ndipo, walipoeua Kedesi katika nchi ya Galili milimani kwa Nafutali na Sikemu milimani kwa Efuraimu na Kiriati-Arba, ndio Heburoni, milimani kwa Yuda.[#Yos. 15:13; 19:37.]

8Tena ng'ambo ya huko ya Yordani upande wa Yeriko wa Maawioni kwa jua wakatoa kwa shina la Rubeni mji wa Beseri ulioko nyikani juu mlimani panapokwenda sawa, tena Ramoti wa Gileadi kwa shina la Gadi na Golani wa Basani kwa shina la Manase.[#5 Mose 4:43.]

9Hii ndiyo miji iliyowekewa wana wote wa Isiraeli nao wageni waliokaa ugenini kwao ya kuikimbilia; mtu ye yote asiyemwua mwenziwe kwa kusudi asiuawe na mkono wake mwenye kuilipiza hiyo damu, mpaka asimamishwe mbele ya mkutano.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania