Yosua 21

Yosua 21

Miji 48 ya watambikaji na ya Walawi.

1Kisha wakuu wa milango ya Walawi wakamjia mtambikaji Elazari na Yosua, mwana wa Nuni, na wakuu wa milango ya mashina ya wana wa Isiraeli,[#Yos. 14:1.]

2wakawaambia huko Silo katika nchi ya Kanaani kwamba: Bwana aliagiza kinywani mwa Mose kutupa sisi miji ya kukaa pamoja na malisho yao ya nyama wetu wa kufuga.[#4 Mose 35:2-8.]

3Kwa hiyo wana wa Isiraeli wakawatolea Walawi kwa kuagizwa na Bwana katika mafungu yao miji hii pamoja na malisho yao:

(4-42: 1 Mambo 6:39-66.)

4Koo za Wakehati zilipopigiwa kura, wana wa mtambikaji Haroni waliokuwa katika hawa Walawi walipata miji 13 kwa shina la Yuda na kwa shina la Simeoni na kwa shina la Benyamini.

5Nao wana wa Kehati waliosalia walipopigiwa kura walipata miji 10 kwa koo za shina la Efuraimu na kwa shina la Dani na kwa nusu ya shina la Manase.

6Nao wana wa Gersoni walipopigiwa kura walipata miji 13 kwa koo za shina la Isakari na kwa shina la Aseri na kwa shina la Nafutali na kwa nusu ya shina la Manase kule Basani.

7Nao wana wa Merari walipata miji 12 ya kuzigawanyia koo zao kwa shina la Rubeni na kwa shina la Gadi na kwa shina la Zebuluni.

8Miji hii ndiyo, wana wa Isiraeli waliyowapa Walawi pamoja na malisho yao kwa kuwapigia kura, kama Bwana alivyoviagiza kinywani mwa Mose.

9Kwa shina la wana wa Yuda na kwa shina la wana wa Simeoni waliwapa Walawi miji hii, waliyoita kwa majina yao.

10Wana wa Haroni walipigiwa kura ya kwanza ya koo za Kehati katika wana wa Lawi.

11Wakawapa Kiriati wa Arba aliyekuwa baba yake Anaki, ndio Heburoni ulioko milimani kwa Yuda pamoja na malisho yake yaliyouzunguka.[#Yos. 20:7.]

12Lakini mashamba yake pamoja na mitaa yake walikuwa wamempa Kalebu, mwana wa Yefune, yawe mali zake za kuzishika.[#Yos. 14:14; 15:13.]

13Lakini wana wa mtambikaji Haroni waliwapa huo mji wa Heburoni, uliokuwa wa kukimbilia wauaji, pamoja na malisho yake, tena Libuna pamoja na malisho yake,

14na Yatiri pamoja na malisho yake na Estemoa pamoja na malisho yake,

15na Holoni pamoja na malisho yake na Debiri pamoja na malisho yake,

16na Aini pamoja na malisho yake na Yuta pamoja na malisho yake, Beti-Semesi pamoja na malisho yake, ndio miji 9 kwa mashina haya mawili.[#1 Sam. 6:12,15.]

17Tena kwa shina la Benyamini: Gibeoni pamoja na malisho yake na Geba pamoja na malisho yake,

18na Anatoti pamoja na malisho yake na Almoni pamoja na malisho yake, ndio miji 4.[#Yer. 1:1.]

19Miji yote ya wana wa Haroni waliokuwa watambikaji ilikuwa miji 13 pamoja na malisho yao.

20Nazo koo za wana wa Kehati waliokuwa Walawi, ndio wana wa Kehati waliosalia, walipopigiwa kura yao walipata miji kwa shina la Efuraimu.

21Wakawapa Sikemu uliokuwa wa kukimbilia wauaji pamoja na malisho yake milimani kwa Efuraimu na Gezeri pamoja na malisho yake,[#Yos. 20:7.]

22na Kibusaimu pamoja na malisho yake na Beti-Horoni pamoja na malisho yake, ndio miji 4.

23Tena kwa shina la Dani: Elteke pamoja na malisho yake na Gibetoni pamoja na malisho yake,

24na Ayaloni pamoja na malisho yake na Gati-Rimoni pamoja na malisho yake, ndio miji 4.

25Tena kwa nusu ya shina la Manase: Taanaki pamoja na malisho yake na Gati-Rimoni pamoja na malisho yake, ndio miji 2.

26Miji yote ilikuwa 10 pamoja na malisho yao ya kuzigawanyia koo za wana wa Kehati waliosalia.

27Nao wana wa Gersoni waliokuwa miongoni mwa koo za Walawi walipata kwa nusu ya shina la Manase mji wa Golani huko Basani uliokuwa wa kukimbilia wauaji pamoja na malisho yake na Bestera pamoja na malisho yake, ndio miji 2.[#Yos. 20:8.]

28Tena kwa shina la Isakari Kisioni pamoja na malisho yake na Daberati pamoja na malisho yake,

29Yarmuti pamoja na malisho yake na Eni-Ganimu pamoja na malisho yake, ndio miji 4.

30Tena kwa shina la Aseri: Misali pamoja na malisho yake na Abudoni pamoja na malisho yake,

31Helkati pamoja na malisho yake na Rehobu pamoja na malisho yake, ndio miji 4.

32Tena kwa shina la Nafutali: mji wa Kedesi uliokuwa wa kukimbilia wauaji kule Galili pamoja na malisho yake na Hamoti-Dori pamoja na malisho yake na Kartani pamoja na malisho yake, ndio miji 3.[#Yos. 20:7.]

33Miji yote, Wagersoni waliyozipatia koo zao, ilikuwa miji 13 pamoja na malisho yao.

34Nazo koo za wana wa Merari, ndio Walawi waliosalia, walipata kwa shina la Zebuluni: Yokinamu pamoja na malisho yake, Karta pamoja na malisho yake,

35Dimuna pamoja na malisho yake, Nahalali pamoja na malisho yake, ndio miji 4.

36Tena kwa shina la Rubeni: Beseri pamoja na malisho yake na Yasa pamoja na malisho yake.[#Yos. 20:8.]

37Kedemoti pamoja na malisho yake na Mefati pamoja na malisho yake, ndio miji 4.

38Tena kwa shina la Gadi: mji wa Rama wa Gileadi, uliokuwa wa kukimbilia wauaji, pamoja na malisho yake na Mahanaimu pamoja na malisho yake,[#Yos. 20:8.]

39Hesiboni pamoja na malisho yake, Yazeri pamoja na malisho yake, yote ndio miji 4.

40Miji yote, wana wa Merari waliosalia miongoni mwa koo za Walawi waliyozipatia koo zao kwa kupigiwa kura, ilikuwa miji 12.

41Miji yote ya Walawi iliyokuwa katikati ya nchi zao wana wa Isiraeli ilikuwa miji 48 pamoja na malisho yao yaliyoizunguka;

42miji hii ilikuwa mji kwa mji pamoja na malisho; ndivyo, miji hiyo yote ilivyokuwa.

43Ndivyo, Bwana alivyowapa Waisiraeli nchi hii yote, aliyoapa kuwapa baba zao, wakaichukua, wakakaa humo.[#1 Mose 12:7.]

44Naye Bwana akawapatia utulivu pande zote pia, kama alivyowaapia baba zao, mtu asiweze kusimama mbele yao miongoni mwa adui zao wote, kwani adui zao wote Bwana aliwatia mikononi mwao.

45Yale mema yote, Bwana aliyowaagia wao wa mlango wa Isiraeli, halikuwapotelea hata moja, yalikuwa yametimia yote pia.[#Yos. 23:14.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania