3 Mose 17

3 Mose 17

Mahali pa kutambikia.

1Bwana akamwambia Mose kwamba:

2Sema na Haroni na wana wote wa Isiraeli, uwaambie: Hili ni neno, aliloliagiza Bwana kwamba:

3Mtu ye yote wa mlango wa Isiraeli atkayechinja ng'ombe au kondoo au mbuzi makambini au atakayemchinja nje ya makambi,

4asimpeleke pa kuliingilia Hema la Mkutano, amtolee Bwana toleo la tambiko mbele ya Kao lake Bwana, mtu huyu na awaziwe kuwa mwenye manza za damu: kwa kuwa alimwaga damu, sharti ang'olewe mtu huyu katikati yao walio ukoo wake.[#Yes. 66:3.]

5Ni kwamba: ng'ombe zao za tambiko, wanazozichinja maporini, wana wa Isiraeli sharti wampelekee Bwana hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano na kumpa mtambikaji, ndipo wazichinje kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani za Bwana.

6Nazo damu mtambikaji na azinyunyize juu ya meza ya kumtambikia Bwana hapo pa kuliingilia Hema la Mkutano, nayo mafuta na ayateketeze kuwa moshi wenye mnuko wa kumpendeza Bwana.

7Ng'ombe zenu za tambiko msizitolee tena mashetani, mnaowwafuata kufanya ugoni nao. Haya sharti yawe kwao maongozi ya kale na kale ya kuongoza vizazi na vizazi vya kwao.[#5 Mose 32:17.]

8Tena uwaambie: Mtu ye yote wa mlango wa Isiralei, hata mgeni atakayekaa kwao, atakayetoa ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima au ng'ombe nyingine ya tambiko,

9asipoipeleka pa kuliingilia Hema la Mkutano kuiteketeza hapo, iwe ng'ombe ya tambiko ya Bwana, mtu huyu sharti ang'olewe kwao walio wa ukoo wake.[#5 Mose 12:14.]

Mwiko wa damu na wa kibudu.

10Mtu ye yote wa mlango wa Isiraeli, hata mgeni atakayekaa kwao, atakayekula damu yo yote, mtu huyu atakayekula damu nitamkazia macho yangu, nimng'oe katikati yao walio ukoo wake.[#3 Mose 3:17.]

11Kwani roho ya mwili imo katika damu, nami niliwapa damu, mzipeleke mezani pa kutambikia, ziwapatie upozi ninyi wenyewe, kwani damu humpatia mtu upozi, kwa kuwa roho imo.[#Ebr. 9:22.]

12Kwa hiyo nimewaambia wana wa Isiraeli: Atakayekaa kwenu asile damu, wala mgeni atakayekaa kwenu asile damu!

13Mtu ye yote aliye wa wana wa Isiraeli naye mgeni atakayekaa kwao, akiwinda nyama au ndege anayelika, sharti aimwage damu yake na kuifunika kwa mchanga.

14Kwani roho ya kila mwenye mwili ni damu yake, maana humu ndimo, roho yake ilimo; kwa hiyo nimewaambia wana wa Isiraeli: Msile damu zao wo wote walio wenye miili! Kwani roho ya kila mwenye mwili ni damu yake, naye kila atakayeila sharti ang'olewe.[#1 Mose 9:4.]

15Tena kila atakayekula kibudu au nyama aliyeraruliwa na nyama mwingine, kama ni mwenyeji au kama ni mgeni, sharti azifue nguo zake na koga majini, naye atakuwa mwenye uchafu mpaka jioni, kisha atakuwa ametakata.[#3 Mose 11:40.]

16Lakini asipozifua nguo zake, wala asipouogesha mwili wake majini, atakuwa amekora manza zitakazomkalia.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania