The chat will start when you send the first message.
1Bwana akamwambia Mose kwamba:
2Sema na wana wa Isiraeli ukiwaambia: Sikukuu za Bwana, mtakazozitangaza kuwa za kukutania Patakatifu, hizo sikukuu zangu ndizo hizi:
3Kazi sharti zifanywe siku sita, lakini siku ya saba ni siku ya kupumzika kabisa ya kukutania Patakatifu; hapo isifanywe kazi yo yote, maana ndiyo siku ya mapumziko ya kumheshimu Bwana katika makao yenu yote.[#2 Mose 20:8-11.]
4Hizi ndizo sikukuu za Bwana za kukutania Patakatifu, nanyi sharti mzitangaze, siku zao zilizowekwa zitakapotimia:[#2 Mose 23:14-19.]
5Katika mwezi wa kwanza siku ya kumi na nne ya mwezi saa za jioni ni Pasaka ya Bwana.[#2 Mose 12.]
6Siku ya kumi na tano ya mwezi uo huo ni sikukuu ya Bwana ya Mikate isiyochachwa; ndipo mle siku saba mikate isiyochachwa.
7Siku ya kwanza na mkutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi,
8ila mmtolee Bwana siku saba ng'ombe za tambiko za kuteketezwa. Siku ya saba mkutanie tena Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi.
9Bwana akamwambia Mose kwamba:
10Sema na wana wa Isiraeli ukiwaambia: Mtakapoingia katika nchi hiyo, nitakayowapa, hapo mtakapoyavuna mavuno yake, mganda wa kwanza wa mavuno yenu sharti mwupeleke kwa mtambikaji.
11Naye aupitishe motoni huo mganda mbele ya Bwana, uwapendezeshe kwake. Kesho yake siku ya mapumziko ndipo mtambikaji aupitishe motoni.[#Mat. 28:1; 1 Kor. 15:20.]
12Tena siku hiyo ya kuupitisha mganda wenu motoni sharti mtengeneze mwana kondoo wa mwaka mmoja asiye na kilema kuwa ng'ombe ya tambiko ya Bwana ya kuteketezwa nzima
13pamoja na vilaji vyake vya tambiko: pishi moja ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta wa kumteketezea Bwana kuwa mnuko wa kumpendeza, tena kibaba kimoja cha mvinyo kuwa kinywaji chake cha tambiko.
14Msile mikate ya ngano mpya wala bisi wala chenga za masuke machanga mpaka siku hiyo, mtakapomtolea Mungu wenu vipaji hivyo vya tambiko. Maongozi haya na yawe ya kale na kale kwa vizazi vyenu po pote, mtakapokaa.
15Kuanzia kesho yake siku ya mapumziko, ni siku ile mlipoupeleka mganda wa kupitishwa motoni, mjihesabie majuma mazima saba, yatimie;[#2 Mose 23:16; 34:22; 4 Mose 28:26-31.]
16siku zao, mtakazozihesabu mpaka kesho yake siku ya mapumziko ya saba ni siku 50; zikitimia, ndipo mmtolee Bwana vilaji vipya vya tambiko.[#5 Mose 16:9-12.]
17Makaoni mwenu mtoe mikate miwili ya kupitishwa motoni iliyotengenezwa kwa pishi moja ya unga mwembamba, iliyookwa ilipokwisha kuchachuka, ipate kuwa malimbuko ya Bwana.
18Pamoja na hiyo mikate sharti mpeleke wana kondoo saba wa mwaka mmoja wasio na vilema na ndama mmoja dume na madume mawili ya kondoo, wawe ng'ombe za tambiko za Bwana za kuteketezwa nzima pamoja na vilaji na vinywaji vyao vya tambiko; vikichomwa moto viwe mnuko mzuri wa kumpendeza Bwana.
19Kisha sharti mtengeneze dume moja la mbuzi kuwa ng'ombe ya tambiko ya weuo na wana kondoo wawili wa mwaka mmoja kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani.
20Kisha mtambikaji awapitishe motoni pamoja na hiyo mikate ya malimbuko kuwa kipaji cha kupitishwa motoni mbele ya Bwana pamoja na hawa wana kondoo wawili; kwa kuwa hawa ni watakatifu wa Bwana, watakuwa mali za watambikaji.
21Siku hiyo sharti mtangaze, watu wenu wakutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi. Maongozi haya na yawe ya kale na kale kwa vizazi vyenu po pote, mtakapokaa.
22Mtakapovuna mavuno ya nchi yenu msikate napo pembeni penye mashamba yenu kupavunia napo, wala msiokoteze viokotezo vya mavuno yenu, ila mviache, viokotezwe na wakiwa na wageni. Mimi Bwana ni Mungu wenu.[#3 Mose 19:9.]
23Bwana akamwambia Mose kwamba:[#4 Mose 10:10; 29:1-6.]
24Waambie wana wa Isiraeli kwamba: Katika mwezi wa saba siku ya kwanza ya mwezi iwe kwenu siku ya mapumziko ya ukumbusho wa kupiga baragumu, mtakapokutania Patakatifu.
25Msifanye kazi yo yote ya utumishi, ila mmtolee Bwana ng'ombe za tambiko.
26Bwana akamwambia Mose kwamba:[#3 Mose 16.]
27Siku ya kumi ya huo mwezi wa saba ni siku ya Mapoza, napo ndipo mkutanie Patakatifu pamoja na kujitesa kwa kufunga na kumtolea Bwana ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa.
28Siku hiyo msifanye kabisa kazi yo yote, kwani ndio siku ya Mapoza ya kuwapatia ninyi upozi mbele ya Bwana Mungu wenu.
29Kila asiyejitesa mwenyewe kwa kufunga siku hiyohiyo atang'olewa kwao walio ukoo wake.
30Naye kila atakayefanya kazi yo yote siku hiyohiyo nitamwangamiza kabisa, atoweke katikati yao walio ukoo wake.
31Kwa hiyo msifanye kazi yo yote. Maongozi haya na yawe ya kale na kale kwa vizazi vyenu po pote, mtakapokaa.
32Iwe kwenu siku ya mapumziko ya kupumzika kabisa ya kujitesa kwa kufunga. Sharti mpumzike jioni ile siku ya tisa ya mwezi huo toka hapo jioni, ikiwa jioni tena, mpumzike kwa kuishika hiyo siku yenu ya mapumziko.
33Bwana akamwambia Mose kwamba:[#2 Mose 23:16; 34:22.]
34Waambie wana wa Isiraeli: Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni sikukuu ya Bwana ya Vibanda siku saba.[#4 Mose 29:12-39; 5 Mose 16:13-15.]
35Siku ya kwanza na mkutanie Patakatifu, msifanye kazi yo yote ya utumishi.
36Siku saba sharti mmtolee Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa; siku ya nane na mkutanie Patakatifu, mmtolee Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa, ni siku ya mkutano, kwa hiyo msifanye kazi yo yote ya utumishi.[#Yoh. 7:37.]
37Hizi ndizo sikukuu za Bwana, ndipo mtangaze, watu wakutanie Patakatifu kumtolea Bwana ng'ombe za tambiko za kuteketezwa: za kuteketezwa nzima pamoja na vilaji vya tambiko, tena ng'ombe za tambiko za kuchinjwa pamoja na vinywaji vya tambiko, kila moja siku yake, kama siku inavyopaswa.
38Lakini tena ziko siku za mapumziko za Bwana na vipaji, mnavyovitoa wenyewe, hata vipaji, mnavyovitoa kwa kuyalipa mliyoyaapa, na vipaji vinginevingine, mnavyomtolea Bwana kwa kupendezwa mioyoni.
39Siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakapokuwa mmekwisha kuyachuma mapato ya nchi, sharti mle sikukuu ya Bwna siku saba, siku ya kwanza ni ya mapumziko, nayo ya nane ni ya mapumziko.
40Tena siku ya kwanza na mjipatie matunda mazuri ya miti na makuti mabichi ya mitende na matawi ya miti ya maporini na ya mitoni, mmfurahie Bwana Mungu wenu siku saba.[#Neh. 8:14-16.]
41Siku hiyo iliyo sikukuu ya Bwana sharti mwile kila mwaka siku saba. Maongozi haya na yawe ya kale na kale kwa vizazi vyenu, mwile sikukuu hii siku saba.
42Na mkae vibandani siku saba, wote walio wenyeji kwao Waisiraeli na wakae vibandani.
43Ni kwa kwamba vizazi vyenu wajue, ya kuwa niliwakalisha vibandani nilipowatoa katika nchi ya Misri. Mimi Bwana ni Mungu wenu.
44Mose akawaambia wana wa Isiraeli hizo sikukuu za Bwana.