The chat will start when you send the first message.
1Nayo haya ndiyo maongozi ya ng'ombe za tambiko za upozi: ni takatifu zenyewe.[#3 Mose 5:1-6; 3 Mose 1:3,5.]
2Mahali hapo, wanapozichinja ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima, papo hapo na wazichinje nazo ng'ombe za tambiko za upozi, nazo damu zao na azinunyize pande zote juu ya meza ya kutambikia.
3Nayo mafuta yote ayatoe humo, ayapeleke: mkia na mafuta yanayoufunika utumbo,
4nayo mafigo yote mawili pamoja na mafuta yanayoshikamana nayo penye nyama za viuno na kipande cha ini kilicho pamoja na mafigo; basi, haya yote na ayaondoe.[#3 Mose 3:9-10.]
5Kisha mtambikaji na ayachome moto mezani pa kutambikia kuwa moto wa Bwana. Hii ndiyo ng'ombe ya tambiko ya upozi.
6Watambikaji wote walio wa kiume na wazile nyama zake; nazo ziliwe mahali patakatifu, maana nazo ni takatifu zenyewe.
7Mambo ya ng'ombe za tambiko za weuo yalivyo, ndivyo, nayo ya ng'ombe za tambiko za upozi yalivyo, maongozi yao ni yayo hayo: nyama zitakuwa zake mtambikaji yule aliyempatia upozi mwenye ng'ombe.
8Naye mtambikaji akipeleka ng'ombe ya tambiko ya mtu ya kuteketezwa nzima, ngozi ya hiyo ng'ombe ya tambiko ya kuteketezwa nzima itakuwa yake mtambikaji yule aliyeipeleka.[#3 Mose 1:6.]
9Navyo vilaji vyote vya tambiko vinavyookwa jikoni, navyo vyote vilivyotengenezwa chunguni au kangoni vitakuwa vyake mtambikaji yule aliyevipeleka.[#3 Mose 2:4-5,7.]
10Navyo vilaji vyote vya tambiko vilivyochanganywa na mafuta navyo vilivyo vikavu vitakuwa vyao wana wote wa Haroni, wavitumie kila mtu na ndugu yake.
11Haya ndiyo maongozi ya ng'ombe za tambiko za shukrani, mtu atakazomtolea Bwana:[#3 Mose 3.]
12Mtu akiitoa kuwa ya sifa, na aitoe hiyo ng'ombe ya tambiko ya sifa pamoja na vikate visivyochachwa, vilivyochanganywa na mafuta, na unga mwembamba wa vitumbua wa kutengeneza vikate vilivyochanganywa na mafuta.[#3 Mose 22:29.]
13Hili toleo lake alipeleke pamoja na mikate ilivyochachwa na pamoja na ng'ombe yake ya tambiko ya shukrani, atakayoitoa kuwa ya sifa.
14Katika hayo matoleo yote na atoe moja la kumnyanyulia Bwana; nalo ni lake mtambikaji yule atakayeinyunyiza damu ya ng'ombe ya tambiko ya shukrani.
15Nazo nyama za hiyo ng'ombe ya tambiko ya shukrani iliyo ya sifa na ziliwe siku hiyo ya kutolewa kwake, wasiziweke mpaka kesho.[#3 Mose 19:6; 22:30.]
16Akiitoa hiyo ng'ombe yake ya tambiko kwa ajili ya kiapo au kwa mapenzi yake mwenyewe, nyama zake hiyo ng'ombe ya tambiko na ziliwe siku hiyo ya kutolewa kwake, hata kesho yake masao yake yatalika.
17Lakini nyama za hiyo ng'ombe ya tambiko zitakazosazwa mpaka siku ya tatu sharti ziteketezwe kwa moto.
18Kama nyama za ng'ombe yake ya tambiko ya shukrani zingeliwa siku ya tatu, mwenye kuitoa asingependeza, wala asingewaziwa kuwa mwenye kuitoa, ila zitakuwa machukizo tu, naye kila mtu atakayezila atakuwa amekora manza.
19Nazo nyama zilizogusana nacho cho chote kilicho kichafu zisiliwe, ila ziteketezwe kwa moto. Nyama nyingine za tambiko kila atakataye atazila hizo nyama.
20Lakini kila mtu atakayekula nyama za ng'ombe ya tambiko ya shukrani zilizo zake Bwana, akiwa mwenye uchafu, basi, roho yake huyo mtu na ing'olewe, atoweke kwenye watu wa kabila lake.
21Tena mtu akigusa cho chote chenye uchafu, kama ni mtu aliye na uchafu wake au nyama chafu au tapisho lo lote linalochafua, naye akila nyama za ng'ombe ya tambiko ya shukrani zilizo zake Bwana, basi, roho yake huyo mtu na ing'olewe, atoweke kwenye watu wa kabila lake.
22Bwana akamwambia Mose kwamba:
23Waambie wana wa Isiraeli kwamba: Mafuta yote ya ng'ombe na ya kondoo na ya mbuzi msiyale![#3 Mose 3:17.]
24Tena mafuta ya nyama aliyekufa kibudu nayo mafuta ya nyama aliyeraruliwa na nyama mwingine mtayatumia ya kazi yo yote, lakini kula msiyale![#2 Mose 22:31.]
25Kwani kila atakayekula mafuta ya nyama, watu wanayomtolea Bwana kuchomwa motoni, basi, roho yake huyo mtu aliyeyala na ing'olewe, atoweke kwenye watu wa kabila lake.
26Nazo damu zote pia msizile mahali po pote, mtakapokaa, wala za ndege wala za nyuma.[#3 Mose 3:17.]
27Kila mtu atakayekula damu zo zote roho yake na ing'olewe, atoweke kwenye watu wa kabila lake.
28Bwana akamwambia Mose:
29Waambie wana wa Isiraeli kwamba: Atakayemtolea Bwana ng'ombe yake ya tambiko ya shukrani sharti ampelekee Bwana toleo lake, alilolitoa katika hiyo ng'ombe yake ya tambiko ya shukrani.
30Mikono yake mwenyewe na iyapeleke yatakayochomwa kwa moto wa Bwana, ni mafuta pamoja na kidari; akiyapeleka haya, kidari na wakipitishe motoni mbele ya Bwana, kiwe kipaji cha tambiko cha kupitishwa motoni.[#2 Mose 29:24.]
31Kisha mtambikaji na ayachome moto yale mafuta mezani pa kutambikia, lakini kidari kitakuwa chao Haroni na wanawe.
32Nayo mapaja ya kuume ya ng'ombe zenu za tambiko za shukrani sharti mwape watambikaji kuwa vipaji vya tambiko vya kunyanyuliwa.[#3 Mose 9:21.]
33Atakayetoa damu za ng'ombe za tambiko za shukrani pamoja na mafuta yao miongoni mwa wana wa Haroni, basi, lile paja la kuume ni fungu lake yeye, atakalolipata.
34Kwani vidari vya kupitishwa motoni na mapaja ya kunyanyuliwa ninayachukua kwa wana wa Isiraeli katika ng'ombe zao za tambiko za shukrani, nimpe mtambikaji Haroni na wanawe kuwa haki yao ya kale na kale kwao wana wa Isiraeli.
35Haya ndiyo, Haroni na wanawe watakayoyapata kwenye mioto ya Bwana kwa hivyo, walivyopakwa mafuta; Bwana aliwagawia haya siku ile, alipowatoa kuwa watambikaji wake.
36Siku ile, Bwana alipowapaka mafuta, aliwaagiza wana wa Isiraeli, wawape haya, nayo ni haki ya kale na kale ya vizazi vyao.
37Haya ndiyo malinganyo ya kutumia ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na vilaji vya tambiko na ng'ombe za tambiko za weuo na za upozi na za kujazwa gao nazo ng'ombe za tambiko za shukrani.[#3 Mose 6:20.]
38Ndiyo, Bwana aliyomwagiza Mose mlimani kwa Sinai siku ile, alipowaagiza wana wa Isiraeli kumtolea Bwana matoleo yao katika nyika ya Sinai.