The chat will start when you send the first message.
1Kisha akawaambia wanafunzi wake: Makwazo hayana budi kuja, lakini anayeyaleta atapatwa na mambo.
2Akitundikwa shingoni pake jiwe kubwa la kusagia, kisha atumbukizwe baharini, inamfaa kuliko kukwaza mmoja tu aliye mwenzao hawa wadogo.[#Mat. 18:6-7.]
3Jiangalieni! Ndugu yako akikukosea, umtishe! Naye akijuta, umwondolee![#Mat. 18:15.]
4Ijapo, akukosee mara saba siku moja na kukurudia mara saba na kusema: Nimejuta, sharti umwondolee![#Mat. 18:21-22.]
5Mitume wakamwambia Bwana: Tuongezee nguvu za kumtegemea Mungu![#Mar. 9:24.]
6Bwana akasema: Cheo chenu cha kumtegemea Mungu kikiwa kidogo kama kipunje cha mbegu, mtauambia mkuyu huu: Ng'oka hapo, ulipo, ujipande baharini! nao utawatii.[#Mat. 17:20; 21:21.]
7Kwenu yuko mwenye mtumwa wa kulima au wa kuchunga atakayemwambia huyo, akirudi toka shamba: Sasa hivi njoo, ukae chakulani?
8Hatamwambia: Andalia chakula, nitakachokila, ujifunge nguo, unitumikie, mpaka nitakapokwisha kula na kunywa! Kisha nawe ule, unywe?
9Je? Atamwambia mtumwa asante, kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa?
10Vivyo nanyi matakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa semeni: Sisi tu watumwa wasiofaa, tumefanya tu yaliyotupasa kuyafanya!
11*Ikawa, alipokwenda Yerusalemu, akashika njia ya kupita katikati ya Samaria na Galilea.[#Luk. 9:51; 13:22.]
12Alipoingia kijijini akakutana na waume kumi wenye ukoma waliokuwa wamesimama mbali,[#3 Mose 13:45-46.]
13wakapaza sauti wakisema: Bwana Yesu, tuhurumie!
14Alipowaona akawaambia: Nendeni kujionyesha kwa watambikaji! Ikawa, walipokwenda wakatakaswa.[#Luk. 5:14; 3 Mose 14:2-3.]
15Lakini mmoja wao alipoona, ya kuwa amepona, akarudi akimtukuza Mungu kwa sauti kuu.
16Akamwangukia kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria.
17Yesu akajibu akisema: Sio kumi waliotakaswa? Wale tisa wako wapi?
18Hawakuonekana wengine waliorudi, wamtukuze Mungu, pasipo huyu mgeni?
19Akamwambia: Inuka, uende zako! Kunitegemea kwako kumekuponya.*[#Luk. 7:50.]
20*Alipoulizwa na Mafariseo: Ufalme wa Mungu unakuja lini? akawajibu akisema: Ufalme wa Mungu unapokuja, watu hawatauona kwa macho,[#Mat. 12:28; Yoh. 18:36; Rom. 14:17.]
21wala hawatasema: Tazama, up hapa! au: Uko huko! Kwani ufalme wa Mungu umo ndani yenu.[#Mat. 24:23.]
22Kisha akawaambia wanafunzi: Siku zitakuja, mtakapotunukia kuiona siku moja tu ya siku za Mwana wa mtu, msiione.
23Nanyi watu watakapowaambia: Tazameni huko! Tazameni hapa! msiende huko, wala msiwafuate![#Luk. 21:8.]
24Kwani kama umeme unavyomulika mbinguni toka pembe hii mpaka pembe ile na kuviangaza vilivyoko chini ya mbingu, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa mtu, siku yake itakapofika.[#Mat. 24:26-27.]
25Lakini kwanza imempasa kuteswa mengi na kukataliwa nao wa kizazi hiki.[#Luk. 9:22.]
26Navyo vilivyokuwa siku za Noa, ndivyo vitakavyokuwa hata siku zile za Mwana wa mtu.[#Mat. 24:37-39.]
27Walikuwa wakila, hata wakinywa, walikuwa wakioa, hata wakiozwa mpaka siku, Noa alipoingia katika chombo kikubwa, yakaja mafuriko makubwa ya maji, yakawaangamiza wote.[#1 Mose 7:7-23.]
28Ndivyo, vilivyokuwa hata siku za Loti: walikuwa wakila, hata wakinywa, wakinunua, hata wakiuza, wakipanda, hata wakijenga.[#1 Mose 19:15,24-25.]
29Lakini siku, Loti alipotoka Sodomu, ndipo, moto uliochanganyika na mawe ya kiberitiberiti ulipotoka mbinguni kama mvua, ukawaangamiza wote.
30Vivyo hivyo vitakuwa siku ile, Mwana wa mtu atakapofunuliwa.*
31Siku ile mtu atakayekuwapo nyumbani juu, vitu vyake vikiwa nyumbani, asiingie kuvichukua! Vivyo hivyo naye atakayekuwako shambani asivirudie vilivyoko nyuma![#Mat. 24:17-18.]
32Mkumbukeni mkewe Loti![#1 Mose 19:26.]
33Atakayetafuta kuiponya roho yake ataiangamiza; naye atakayeiangamiza ataiponya, iwepo.[#Luk. 9:24.]
34Nawaambiani: Usiku ule watu wawili watakaolalia kitanda kimoja, mmoja atapokewa, mwenzake ataachwa.
35Wake wawili watakaokuwa wakisaga pamoja, mmoja atapokewa, mwenzake ataachwa.[#Mat. 24:40-41.]
36Wawili watakaokuwako shambani, mmoja atapokewa, mwenzake ataachwa.
37Walipojibu na kumwuliza: Wapi, Bwana? akawaambia: Penye nyamafu ndipo, nao tai watakapokusanyikia.[#Mat. 24:28.]