The chat will start when you send the first message.
1Yesu alipokwisha kuwaagiza haya wanafunzi wake kumi na wawili akaondoka, alikokuwa, akaenda kufundisha watu na kuwapigia ile mbiu katika miji yao.
2*Lakini Yohana alipozisikia mle kifungoni kazi zake Kristo akatuma wanafunzi wake wawili,[#Mat. 14:3-4.]
3akamwuliza: Wewe ndiwe mwenye kuja, au tungoje mwingine?[#Mat. 3:11; Mal. 3:1.]
4Yesu akajibu akiwaambia: Rudini, mmsimulie Yohana, mliyoyasikia nayo mliyoyaona:
5vipofu wanaona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanapigiwa mbiu njema.[#Yes. 35:5-6; 61:1.]
6Tena mwenye shangwe ndiye asiyejikwaa kwangu.[#Mat. 13:57; 26:31.]
7Wao walipokwenda zao, Yesu akaanza kusema na yale makundi ya watu mambo ya Yohana: Mlipotoka kwenda nyikani mlikwenda kutazama nini? Mlikwenda kutazama utete unaotikiswa na upepo?[#Mat. 3:1,5.]
8Au mlitoka kutazama nini? Mlikwenda kutazama mtu aliyevaa mavazi mororo? Tazameni, wanaovaa mavazi mororo wamo nyumbani mwa wafalme.
9Au mlitoka kutazama nini? Mlitaka kuona mfumbuaji? Kweli, nawaambiani: Ni mkuu kuliko mfumbuaji.[#Luk. 1:76.]
10Huyo ndiye aliyeandikiwa:
Utaniona mimi, nikimtuma mjumbe wangu,
akutangulie, aitengeneze njia yako mbele yako.*
11Kweli nawaambiani: Miongoni mwao wote walizaliwa na wanawake hajaonekana aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Lakini aliye mdogo katika ufalme wa mbingu ni mkuu kuliko yeye.[#Mat. 13:17.]
12Tangu siku za Yohana Mbatizaji mpaka leo ufalme wa mbingu huendewa kwa nguvu, nao wenye nguvu lhuupoka.[#Luk. 16:16; 13:24.]
13Kwani Wafuambuaji wote nayo Maonyo waliufumbua, mpaka Yohana akitokea.
14Tena kama mnataka kuitikia: Yeye ndiye Elia atakayekuja.[#Mat. 17:10-13; Mal. 4:5.]
15Mwenye masikio yanayosikia na asikie!
16*Lakini wao wa kizazi hiki niwafananishe na nini? Wamefanana na watoto wanaokaa sokoni na kuwaita wenzi wao wakisema:
17Tumewapigia filimbi, nanyi hamkucheza; tena tumewaombelezea, nanyi hamkulia.[#Fano. 29:9.]
18Kwani Yohana alikuja, hakula, wala hakunywaakala, wakasema: Ana pepo.[#Mat. 3:4.]
19Mwana wa mtu alikuja, akala, akanywa, wakasema: Tazameni mtu huyu mlaji na mnyuwaji wa mvinyo, mpenda watoza kodi na wakosaji! Lakini werevu hutokezwa na matendo yake kuwa wa kweli.[#Mat. 9:14-15.]
20Ndipo Yesu alipoanza kuikaripia miji, yalimofanyika ya nguvu yake mengi, kwa maana haikujuta.
21Akasema: Yatakupata, wewe Korasini! Yatakupata, wewe Beti-Saida! Kwani ya nguvu yaliyofanyika kwenu, kama yangalifanyika Tiro na Sidoni, wangalijuta kale na kujivika magunia na kujikalisha majivuni.[#Yona 3:6.]
22Lakini nawaambiani: Siku ya hukumu miji ya Tiro na Sidoni itapata machungu yaliyo madogo kuliko yenu.
23Nawe Kapernaumu, hukupazwa mpaka mbinguni? Utatumbukia mpaka kuzimuni, kwani ya nguvu yaliyofanyika kwako, kama yangalifanyika Sodomu, ungalikuwako mpaka leo.[#Mat. 4:13; 8:5; 9:1.]
24Lakini nawaambiani: Siku ile ya hukumu nchi ya Sodomu itapata machungu yaliyo madogo kuliko yako.*[#Mat. 10:15.]
25*Siku zile Yesu akasema kwamba: Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwani hayo umewaficha werevu na watambuzi, ukawafunulia wachanga.[#1 Kor. 1:26-29.]
26Ndio, Baba, kwani hivyo ndivyo, ulivyopendezwa navyo.
27Vyote nimepewa na Baba yangu. Hakuna anayemtambua Mwana pasipo Baba; wala hakuna anayemtambua Baba pasipo mwana na kila, Mwana atakayemfunulia.[#Mat. 28:18; Yoh. 3:35; 17:2; Fil. 2:9.]
28Njoni kwangu nyote, wenye kusumbuka na wenye kulemewa na mizigo! Mimi nitawatuliza.[#Mat. 12:20; Yer. 31:25.]
29Twaeni kata yangu, mjifunze kwangu! Kwani ndimi mpole na mnyenyekevu moyoni. Kwa hivyo mtaipatia mioyo yenu kituo;[#Yer. 6:16.]
30kwani kata yangu ni njema, nao mzigo wangu ni mwepesi.*[#Mar. 7:3-9; Luk. 11:46; 1 Yoh. 5:3.]