The chat will start when you send the first message.
1Kisha Yesu akasema na watu waliokutanika na wanafunzi wake,
2kwamba: Kitini pa Mose wamekaa waandishi na Mafariseo.
3Yo yote, watakayowaambia, yafanyeni na kuyashika! Lakini kama wafanyavyo, msiyafuate! Kwani kusema wanasema, lakini hawayafanyi.[#Mal. 2:7-8; Rom. 3:21-23.]
4Huwafungia watu mizigo mizito isiyochukulika wakiwawekea mabegani, lakini wenyewe hawataki kuigusa hata kwa kidole chao kimoja tu.[#Tume. 15:10.]
5Matendo yao yote huyafanyia kutazamwa na watu. Hukuza makaratasi ya kuombea, huviongeza navyo vishada vya nguo zao, viwe vinene.[#Mat. 6:1; 2 Mose 13:9; 4 Mose 15:38-39; 5 Mose 6:8.]
6Wakialikwa chakulani hupenda kukaa penye wakuu, namo nyumbani mwa kuombea hupenda viti vya mbele.[#Luk. 14:7.]
7Hupenda kuamkiwa na watu sokoni na kuitwa mfunzi mkuu.
8Lakini ninyi msitake kuitwa mfunzi mkuu! Kwani mfunzi wenu ni mmoja, ndiye Kristo, nanyi nyote ni ndugu.
9Tena nchini msimwite mtu baba yenu! Kwani baba yenu ni mmoja, ni wa mbinguni.
10Wala msitake kuitwa kiongozi! Kwani kiongozi wenu ni mmoja, ni Kristo.
11Lakini kwenu aliye mkubwa na awatumikie ninyi![#Mat. 20:26-27.]
12Kwani atakayejikweza mwenyewe atanyenyekezwa; naye atakayejinyenyekeza mwenyewe atakwezwa.[#Iy. 22:29; Fano. 29:23; Ez. 21:26; Luk. 14:11; 18:14; 1 Petr. 5:5.]
13Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani mnawafungia watu mlango wa ufalme wa mbingu. Ninyi hamwingii, nao wanaotaka kuingia hamwaachi, waingie.
14Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani mnazila nyumba za wajane mkijitendekeza, kama mnakaza kuwaombea. Kwa hiyo mapatilizo yenu yatakuwa kuliko ya wengine.[#Ez. 22:25.]
15Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani mnazunguka baharini na katika nchi kavu, mpate mfuasi mmoja tu; kisha hapo akipatikana, mnamgeuza kuwa wa kutumbukizwa motoni kuwapita ninyi kabisa.
16Yatawapata ninyi viongozi vipofu mnaosema: Mtu atakapoapa na kulitaja Jumba la Mungu, si kitu; lakini mtu atakapoapa na kuitaja dhahabu ya Jumba la Mungu amejifunga![#Mat. 5:34-37; 15:14.]
17Wajinga na vipofu ninyi! Iliyo kubwa ni nini? Dhahabu au Jumba la Mungu linaloitakasa dhahabu?
18Tena mnasema: Mtu atakapoapa na kuitaja meza ya Bwana, si kitu; lakini atakapoapa na kukitaja kipaji kilichoko juu yake amejifunga!
19Vipofu ninyi! Iliyo kubwa ni nini? Kipaji au meza ya Bwana inayokitakasa kipaji?[#2 Mose 29:37.]
20Mtu anayeapa na kuitaja meza ya Bwana huapa na kuitaja hiyo meza pamoja navyo vyote vilivyopo pake.
21Tena mtu anayeapa na kulitaja Jumba la Mungu huapa na kulitaja hilo Jumba pamoja naye yule anayekaa humo.
22Tena mtu anayeapa na kuitaja mbingu huapa na kukitaja kiti cha kifalme cha Mungu pamoja na yeye anayekikalia.[#Mat. 5:34.]
23Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani fungu la kumi mnalitolea hata mchicha na nyanya na pilipili, lakini yaliyo magumu katika Maonyo mmeyaacha, yale ya hukumu na ya huruma na ya mategemeo. Haya yawapasa kuyashika pasipo kuyaacha yale.[#3 Mose 27:30; Mika 6:8.]
24Viongozi vipofu ninyi, mbu mnawatema, lakini ngamia mnawameza!
25Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani vinyweo na vyano mnaviosha nje, lakini ndani vimejaa mapokonyo na mapujufu.[#Mar. 7:4-13.]
26Fariseo kipofu, kwanza osha ndani yake kinyweo na chano, vipate kuwa safi hata nje![#Yoh. 9:40; Tit. 1:15.]
27Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani mmefanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, nayo huonekana nje kuwa mazuri, lakini ndani hujaa mifupa ya wafu na uchafu wote.[#Tume. 23:3.]
28Vivyo hivyo nanyi nje mnaonekana kwa watu kuwa waongofu, lakini ndani yenu imejaa ujanja na upotovu.[#Luk. 16:15.]
29Yatawapata ninyi waandishi na Mafariseo mlio wajanja, kwani mnayajenga makaburi ya wafumbuaji, tena mnayapamba makumbusho ya waongofu
30na kusema: Sisi kama tungalikuwapo siku za baba zetu, basi, hatungalifanya nao bia ya kuwaua wafumbuaji.
31Hivyo mnajishuhudia wenyewe, ya kuwa m-wana wao waliowaua wafumbuaji.[#Tume. 7:52.]
32Nanyi kijazeni kipimo cha baba zenu!
33M nyoka, m wana wa chatu! Mtaikimbiaje hukumu ya kutumbukizwa shimoni mwa moto?[#Mat. 3:7.]
34*Kwa sababu hii tazameni, mimi natuma kwenu wafumbuaji na werevu wa kweli na waandishi; wengine wao mtawaua na kuwawamba misalabani, wengine wao mtawapiga katika nyumba zenu za kuombea, kisha mtawafukuza mji kwa mji;[#Mat. 10:23; 13:52; 1 Tes. 2:15.]
35hivyo zitawajia damu zote za waongofu zilizomwagwa nchini, kuanzia damu ya Abeli aliyekuwa mwongofu mpaka kuifikia damu ya Zakaria, mwana wa Berekia, mliyemwua katikati ya Jumba la Mungu na meza ya Bwana.[#1 Mose 4:8; 2 Mambo 24:20-21.]
36Kweli nawaambiani: hayo yote yatawajia wao wa kizazi hiki.
37Yerusalemu, Yerusalemu, unawaua wafumbuaji, ukawapiga mawe walitumwa kwako! Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako, kama kuku anavyovikusanya vifaranga vyake mabawani! Lakini hamkutaka![#Luk. 13:34-35; Tume. 7:59; 1 Tes. 2:15.]
38Mtaona, Nyumba yenu ikiachwa, iwe peke yake![#1 Fal. 9:7-8; Yer. 12:7; 22:5.]
39Kwani nawaambiani: Tangu sasa hamtaniona tena, mpaka mtakaposema: Na atukuzwe ajaye kwa Jina la Bwana!*[#Mat. 21:9; 26:64; Sh. 118:26; Rom. 11:26.]