The chat will start when you send the first message.
1*Siku ya mapumziko ilipokwisha, siku ya kwanza ya juma kulipokucha, wakaenda Maria Magdalena na yule Maria mwingine kulitazama kaburi.
2Mara kukawa na tetemeko kubwa la nchi. Kwani malaika wa Bwana alishuka toka mbinguni, akaja akalifingirisha lile jiwe, likatoka mlangoni, akalikalia.
3Sura yake ilikuwa kama umeme, nguo zake zikang'aa kama chokaa juani.[#Mat. 17:2; Tume. 1:10.]
4Walinzi wakaingiwa na woga, wakatetemeka, wakawa kama wafu.
5Malaika akawaambia wale wanawake akisema: Msiogope! Kwani ninajua, ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyewambwa msalabani.
6Hayumo humu, kwani amefufuliwa, kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali, Bwana alipokuwa amewekwa![#Mat. 12:40; 16:21; 17:23; 20:19; Tume. 2:36.]
7Nanyi nendeni upesi, mwaambie wanafunzi wake kwamba: Amefufuliwa katika wafu! Tazameni, anawatangulia ninyi kwenda Galilea. Huko ndiko, mtakakomwona. Tazameni, nimekwisha kuwaambia.[#Mat. 26:32.]
8Wakatoka upesi kaburini wakishikwa na woga, tena wakifurahi sana, wakaenda mbio kuwasimulia wanafunzi wake.
9Mara Yesu akakutana nao, akasema: Salamu kwenu! Nao wakamjia, wakamshika miguu yake, wakamwangukia.
10Ndipo, Yesu alipowaambia: Msiogope, nendeni, mwasimulie ndugu zangu, waende Galilea! Ndiko, watakakoniona.*[#Ebr. 2:11.]
11Walipokwenda zao, mara nao walinzi wakafika mjini mmoja mmoja, wakasimulia watambikaji wakuu yote yaliyokuwapo.[#Mat. 27:65.]
12Wakakusanyika pamoja na wazee, wakala njama, wakatoa fedha nyingi za kuwapa wale askari,
13wakawaambia: Semeni: Wanafunzi wake wamekuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala![#Mat. 27:64.]
14Neno hili likijulikana kwa mtawala nchi, sisi tutasema naye kwa werevu, ninyi msipate mahangaiko.
15Kwa hiyo wakazichukua zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Nalo neno hili linasimuliwa kwa Wayuda mpaka leo.
16*Wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilea, wakafika mlimani pale, Yesu alipowaagizia.[#Mat. 28:7.]
17Walipomwona wakamwangukia, lakini wengine waliingiwa na mashaka.
18Naye Yesu akawajia, akawaambia: Nimepewa nguvu zote mbinguni na nchini.[#Mat. 11:27; Dan. 7:14; Ef. 1:20-22.]
19Nendeni, mkawafundishe wao wa mataifa yote, wawe wanafunzi wangu, mkiwabatizia Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu[#Mar. 16:15-16.]
20na kuwafundisha, wayashike yote, niliyowaagiza! Tazameni, niko pamoja nanyi siku zote, mpaka dunia itakapokoma.*[#Mat. 18:20; 24:14; Yoh. 14:23; 2 Kor. 5:20.]