The chat will start when you send the first message.
1Msiumbue mtu, msije mkaumbuliwa![#Rom. 2:1; 14:4; 1 Kor. 4:5.]
2Kwani kama mnavyowaumbua wengine, ndivyo, mtakavyoumbuliwa wenyewe. Kipimo, mnachopimia wengine, ndicho, mtakachopimiwa nanyi.[#Mar. 4:24.]
3Nawe unakitazamiani kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako, lakini gogo lililomo jichoni mwako wewe hulioni?
4Au utamwambiaje ndugu yako: Ngoja, nikitoe kibanzi katika jicho lako, wewe mwenyewe ukiwa unalo gogo zima jichoni mwako?
5Mjanja, kwanza litoe gogo katika jicho lako! Kisha utazame vema, ndivyo upate kukitoa kibanzi katika jicho la ndugu yako!
6Kilichotakata msiwape mbwa, wala msiwatupie nguruwe ushanga wenu wa lulu, wasije wakaukanyaga kwa miguu yao na kuwageukia na kuwararua ninyi.[#Mat. 10:11,14-15; Luk. 23:9; 2 Petr. 2:12-22.]
7Ombeni! ndipo, mtakapopewa. Tafuteni! ndipo, mtakapoona. Pigeni hodi! ndipo, mtakapofunguliwa mlango.[#Yer. 29:13-14; Mar. 11:24; Luk. 11:5-13; Yoh. 14:13.]
8Kwani kila anayeomba hupewa, naye anayetafuta huona, naye anayepiga hodi hufunguliwa mlango.
9Au kwenu yuko mtu, mwanawe anapomwomba mkate, ampe jiwe?
10Au anapomwomba samaki, ampe nyoka?
11Basi, ninyi mlio wabaya mkijua kuwapa watoto wenu vipaji vyema, Baba yenu alioko mbinguni asizidi kuwapa mema wanaomwomba?[#Yak. 1:17.]
12Yo yote, mnayotaka, watu wawafanyie ninyi, nanyi mwafanyie yaleyale! Kwani hayo ndiyo Maonyo na Wafumbuaji.[#Mat. 22:39-40; Luk. 6:31; Rom. 13:8-10.]
13*Uingieni mlango ulio mfinyu! Kwani liko lango lililo pana, nayo njia yake ni kubwa; ndiyo inayokwenda penye kuangamizwa, nao wanaoingia mle ni wengi.[#Luk. 13:24; Fil. 3:12.]
14Tena uko mlango ulio mfinyu, nayo njia yake inasonga; ndiyo inayokwenda penye uzima, lakini wanaoiona ni wachache.[#Mat. 19:24; Tume. 14:22.]
15Jilindeni kwa ajili ya wafumbuaji wa uwongo! Wanawajia wamevaa kama kondoo, lakini mioyoni ni mbwa wa mwitu wenye ukali.[#Mat. 24:4-5,11,24; Tume. 20:29; 2 Kor. 11:13-15.]
16Kwa matunda yao mtawatambua. Je? Huchuma zabibu miibani? Au huchuma kuyu mikongeni?[#Gal. 5:19-22; Yak. 3:12.]
17Hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; lakini mti mwovu huzaa matunda mabaya.[#Mat. 12:33.]
18Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu hauwezi kuzaa matunda mazuri
19Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa, utupwe motoni.[#Mat. 3:10; Yoh. 15:2-6.]
20Kwa hiyo mtawatambua kwa matunda yao.[#Rom. 2:13; Yak. 1:22,25; 2:14.]
21Miongoni mwao wanaoniita: Bwana! Bwana! sio wote wakaoingia katika ufalme wa mbingu, ni wao tu wanaoyafanyiza, Baba yangu alioko mbinguni ayatakayo.
22Siku ile wengi wataniuliza: Bwana, sisi hatukufumbua kwa Jina lako? Hatukufukuza pepo kwa Jina lako? Hatukufanya mengi yenye nguvu kwa Jina lako?[#Luk. 13:25-27; 1 Kor. 13:1-2.]
23Ndipo, nitakapowaambia waziwazi: Sijawatambua ninyi kabisa. Ondokeni kwangu, mliofanya maovu!*[#Mat. 25:41; 2 Tim. 2:19; Sh. 6:9.]
24*Basi, kila mtu anayeyasikia haya maneno yangu na kuyafanyiza atafanana na mtu mwenye akili aliyeijenga nyumba yake mwambani.[#Mat. 7:21.]
25Mvua kubwa ikanyesha, mito ikajaa, pepo zikavuma, vyote vikaipiga ile nyumba, lakini haikuanguka, kwani misingi yake ilikuwa imejengwa mwambani.
26Lakini kila mtu anayeyasikia haya maneno yangu asipoyafanyiza atafanana na mtu mpumbavu aliyeijenga nyumba yake mchangani.
27Mvua kubwa ikanyesha, mito ikajaa, pepo zikavuma vyote vikaipiga ile nyumba, basi, ikaanguka, anguko lake likawa kubwa.[#Ez. 13:10-11.]
28Ikawa, Yesu alipokwisha kuyasema maneno haya, makundi ya watu walishangazwa na mafundisho yake.[#Mar. 1:22; Luk. 4:32.]
29Kwani alikuwa akiwafundisha kama wenye nguvu, si kama waandishi wao.*[#Yoh. 7:16,46.]