The chat will start when you send the first message.
1Akaanza kusema nao kwa mifano. Mtu alipanda mizabibu, akaizungusha ugo, akachimbua kamulio la kuzikamulia zabibu, ajenga dungu, akaipangisha wakulima, kisha akaenda katika nchi nyingine.[#Yes. 5:1-2.]
2Siku zilipotimia, akatuma mtumwa kwa wale wakulima, apewe na wakulima matunda ya mizabibu.
3Nao wakamkamata, wakampiga, wakamrudisha mikono mitupu.
4Akatuma tena kwao mtumwa mwingine, naye wakampiga na kumtia vidonda vya kichwani na kumtukana.
5Alipotuma tena mwingine, huyo naye wakamwua. Nao wengine wengi, wengine wakawapiga, wengine wakawaua.
6Alikuwa na mmoja tena, ndiye mwanawe mpendwa; huyo akamtuma kwao wa mwisho akisema: Watamcha mwanangu.
7Lakini wale wakulima wakasemezana wao kwa wao: Huyu ndiye kibwana, njoni, tumwue! Kisha nao urithi wake utakuwa wetu!
8Kwa hiyo wakamkamata, wakamwua, wakamtupa nje ya mizabibu.[#Ebr. 13:12.]
9Basi, mwenye mizabibu atafanya nini? Atakapokuja atawaangamiza wale wakulima, nayo mizabibu atawapa wengine.
10Hamjalisoma bado andiko hilo la kwamba:
Jiwe, walilolikataa waashi, hilihili limekuwa la pembeni?
11Hivyo vimefanywa na Bwana; nasi tukivitazama, ni vya
kustaajabu.
12Ndipo, walipotafuta kumkamata, lakini waliliogopa kundi la watu. Kwani walitambua, ya kuwa amewasemea wao wenyewe mfano huo. Lakini wakamwacha, wakaenda zao.
13Wakatuma kwake Mafariseo na watu wa Herode, wamtege kwa maneno yake.[#Mar. 3:6.]
14Wakaja, wakamwambia: Mfunzi, tumekujua, ya kuwa wewe ni mtu wa kweli, tena humwuliziulizi mtu ye yote, kwani hutazami nyuso za watu, nayo njia ya Mungu unaifundisha, ilivyo kweli.
15Iko ruhusa ya kumtolea Kaisari kodi au haiko? Tumpe au tusimpe? Kwa kuujua ujanja wao akawaambia: Mwanijaribiaje? Nileteeni shilingi, niitazame!
16Walipomletea, akawauliza: Chama hiki cha nani? Maandiko nayo ya nani? Wakamwambia: Ni yake Kaisari.
17Ndipo, Yesu alipowaambia: Yaliyo yake Kaisari mtoleeni Kaisari, naye Mungu yaliyo yake Mungu! Wakamstaajabu sana.[#Rom. 13:7.]
18Masadukeo wanaosema: Hakuna ufufuko walipokuja kwake wakamwuliza wakisema:
19Mfunzi, Mose alituandikia kama hivi: Mtu akifiwa na mkubwa wake aliyeacha mkewe, lakini hakuacha mwana, nduguye amchukue huyo mke, amzalie mkubwa wake mwana.[#1 Mose 38:8; 5 Mose 25:5-6.]
20Kulikuwa na waume saba walio ndugu. Wa kwanza akaoa mke, lakini alipokufa hakuacha mwana.
21Wa pili naye akamchukua, akafa, asiache mwana. Naye wa tatu vivi hivi.
22Nao wote saba hawakuacha mwana. Mwisho wao wote akafa naye mwanamke.
23Basi, katika ufufuko watakapofufuka, atakuwa mke wa yupi wa hao? Kwani wote saba walikuwa naye yule mwanamke.
24Yesu akawaambia: Mkipotelewa hivyo, maana hamyajui Maandiko wala nguvu ya Mungu?
25Kwani watakapofufuka katika wafu hawataoa, wala hawataolewa, ila watakuwa, kama malaika walivyo mbinguni.
26Lakini kwa ajili ya wafu, kwamba wafufuliwa, hamkusoma katika kitabu cha Mose, Mungu alivyomwambia hapo kichakani: Mimi ni Mungu wa Aburahamu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo?[#2 Mose 3:2,6; Mat. 8:11; Luk. 16:22.]
27Basi, Mungu siye wa wafu, ila wao walio hai. Ninyi mnapotelewa sana.
28Akamjia mwandishi mmoja aliyewasikia, walivyobishana; naye alijua, ya kuwa amewajibu vizuri. Huyo akamwuliza: Katika maagizo yote lililo la kwanza ni lipi?
29Yesu akajibu: La kwanza ndilo hili: Sikia, Isiraeli! Bwana Mungu wetu ni Bwana peke yake.[#5 Mose 6:4-5.]
30Nawe umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa mawazo yako yote na kwa nguvu yako yote![#Yoh. 15:12.]
31La pili ndilo hili: Umpende mwenzio, kama unavyojipenda mwenyewe! Agizo jingine lililo kubwa kuliko haya haliko.[#3 Mose 19:18.]
32Yule mwandishi akamwambia: Vema, mfunzi, umesema ya kweli: Mungu ni mmoja tu, hakuna mwingine ila yeye.[#5 Mose 4:35; 6:4.]
33Tena kumpenda yeye kwa moyo wote na kwa mawazo yote na kwa nguvu yote, na kumpenda mwenzio, kama unavyojipenda mwenyewe, hupita ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na vipaji vyote vya tambiko.[#1 Sam. 15:22.]
34Yesu alipomwona, ya kuwa amejibu yenye maana, akamwambia: Wewe hu mbali ya ufalme wa Mungu. Kisha hakuwako hata mmoja aliyejipa moyo wa kumwuliza neno tena.[#Tume. 26:27-29.]
35Yesu alipofundisha hapo Patakatifu akawauliza akisema: Waandishi husemaje, ya kuwa Kristo ni mwana wa Dawidi?
36Dawidi mwenyewe alisema kwa nguvu ya Roho Mtakatifu:
Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti kuumeni kwangu,
mpaka niwaweke adui zako chini miguuni pako!
37Basi, Dawidi mwenyewe akimwita Bwana, anakuwaje tena mwana wake?
Kwa kuwa watu wengi walipendezwa kumsikiliza,
38akasema na kuwafundisha: Jiangalieni kwa ajili ya waandishi wanaotaka kutembea wenye kanzu ndefu na kuamkiwa na watu sokoni!
39Namo nyumbani mwa kuombea hupenda viti vya mbele, hata wakialikwa chakulani hupenda kukaa penye wakuu.
40Huzila nyumba za wajane wakijitendekeza, kama wanakaza kuwaombea. Walio hivyo mapatilizo yao yatakuwa kuliko ya wengine.
41*Akakaa na kuielekea sanduku ya vipaji, akatazama, watu wanavyotia mapesa katika sanduku ya vipaji. Wenye mali wengi wakatia mengi.[#2 Fal. 12:9-10.]
42Akaja mwanamke mjane mmoja aliyekuwa mkiwa, akatia visenti viwili, pamoja ni hela moja.
43Ndipo, alipowaita wanafunzi wake, akawaambia: Kweli nawaambiani: Huyu mjane mkiwa ametia mengi kuliko wote waliotia mapesa humu sandukuni mwenye vipaji.
44Kwani wote walitoa mali katika mali zao nyingi, lakini huyu kwa ukiwa wake amevitoa vyote, alivyokuwa navyo, ndivyo vyote vilivyomlisha.*[#2 Kor. 8:12.]