The chat will start when you send the first message.
1*Siku ya mapumziko ilipokwisha pita, ndipo, Maria Magadalene na Maria, mama yake Yakobo, na Salome waliponunua manukato, wapate kwenda kumpaka.
2Siku ya kwanza ya juma asubuhi na mapema wakajidamka, wakaenda kaburini, jua lilipochomoza.
3Wakasema wao kwa wao: Nani atatufingirishia lile jiwe, litoke mlangoni pa kaburi?
4Walipotazama wakaona, jiwe limekwisha fingirishwa; kwani lilikuwa kubwa mno.
5Walipoingia kaburini wakaona kijana, amekaa kuumeni, amejitanda nguo nyeupe, wakaingiwa na kituko.
6Naye akawaambia: Msistuke! Mnamtafuta Yesu wa Nasareti aliyewambwa msalabani, amefufuliwa, hayumo humu. Patazameni mahali, walipomweka!
7Lakini nendeni, mwaambie wanafunzi wake na Petero, ya kuwa anawatangulia ninyi kwenda Galilea! Huko ndiko, mtakakomwona, kama alivyowaambia.[#Mar. 14:28.]
8Wakatoka kaburini, wakakimbia, kwani walikuwa wameshikwa na utetemeko na ushangao. Kisha hawakumwambia mtu neno, kwani waliogopa.*
9Alipokwisha fufuka asubuhi na mapema siku ya kwanza ya juma, akamtokea kwanza Maria Magadalene, aliyemfukuzia pepo saba.[#Luk. 8:2; Yoh. 20:11-18.]
10Ndipo, alipokwenda, akawasimulia wale waliokuwa pamoja naye, walipoomboleza na kulia.
11Nao waliposikia, ya kuwa anaishi, ya kuwa yeye amemwona, hawakuitikia.
(12-13: Luk. 24:13-35.)12Kisha akawatokea wenzao wawili kwa sura nyingine, wakitembea kwenda shambani.
13Nao wakaenda, wakavisimulia wenzi wao wengine, lakini nao hawakuwaitikia.
(14-18: Luk. 24:36-49; Yoh. 20:19-23.)14*Mwisho akawatokea wale kumi na mmoja, walipokaa wakila. Akawakaripia, kwa sababu walikuwa wameshindwa na kumtegemea, na kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, kwani hawakuwaitikia wale waliomwona, ya kuwa amefufuka.[#1 Kor. 15:5.]
15Akawaagiza: Nendeni katika nchi zote za ulimwenguni, mwatangazie wote walioumbwa Utume mwema![#Mat. 28:18-20.]
16Anayemtegemea Mungu akibatizwa ataokoka, lakini asiyemtegemea atahukumiwa.[#Tume. 2:38.]
17Nao wamtegemeao vielekezo vitakavyowafuata ni hivi: kwa Jina langu watafukuza pepo, watasema kwa ndimi mpya,[#Tume. 2:4,11; 9:17; 10:46; 16:18.]
18watashika nyoka, hata wakinywa machawi, hayatawaua kabisa; watakapobandikia wagonjwa mikono, ndipo, watakapoponapona.[#Luk. 10:19; Tume. 28:3-6; Yak. 5:14-15.]
19Bwana Yesu alipokwisha kusema nao akachukuliwa na kupazwa mbinguni, akaketi kuumeni kwa Mungu.[#Sh. 110:1; Tume. 7:55; 1 Tim. 3:16.]
20Kisha wale wakatoka, wakapiga mbiu mahali po pote. Naye Bwana alifanya kazi pamoja nao akilitia Neno lake nguvu na kutenda vielekezo vilivyowafuata.*[#Ebr. 2:4.]