The chat will start when you send the first message.
1Wakamkusanyikia Mafariseo na wengine waliokuwa waandishi waliotoka Yerusalemu.
2Wakaona wanafunzi wake, wanavyokula vyakula kwa mikono hivyo ilivyo, maana haikunawiwa.[#Luk. 11:38.]
3Kwani Mafariseo na Wayuda wote hawali, wasiponawa mikono na kuikamua; huku ni kuyashika mazoezo ya wakale.
4Navyo vya sokoni hawavili, wasipoviosha kwanza; nayo mambo mengine mengi yako, waliyoyapokea kuyashika, kama kuosha vinyweo na mitungi na vyungu na vitanda.
5Mafariseo na waandishi walipomwuliza: Kwa sababu gani wanafunzi wako hawaendi na kuyafuata mazoezo ya wakale, ila hula chakula kwa mikono hivyo ilivyo?
6akawaambia: Yesaya aliyafumbua vizuri hayo mambo yenu, ninyi wajanja, kama yalivyoandikwa kwamba:
Ukoo huu huniheshimu kwa midomo tu,
lakini mioyo yao inanikalia mbali.
7Hivyo hunicha bure,
kwani hufundisha mafundisho yaliyo maagizo ya watu tu.
8Mnaliacha agizo lake Mungu, myashike mazoezo ya watu.
9Akawaambia: Vizuri vyenu ni kulitengua agizo lake Mungu, mpate kuyaangalia mazoezo ya wakale wenu.
10Kwani Mose alisema: Mheshimu baba yako na mama yako! na tena: Atakayemwapiza baba au mama sharti afe kwa kuuawa![#2 Mose 20:12; 21:17; 5 Mose 5:16.]
11Lakini ninyi husema: Mtu akimwambia baba au mama: Korbani, ni kwamba: Mali, unazozitaka, nikusaidie nazo, amepewa Mungu, basi, ni vema.
12Hivyo mnamzuia mtu huyo, asimpatie baba wala mama kitu;
13hivyo mnalitangua Neno la Mungu kwa ajili ya mazoezo, mliyozoezwa na wakale wenu. Tena mnafanya mengi yanayofanana na hayo.
14Akaliita tena kundi la watu, akawaambia: Nisikilizeni nyote, mjue maana!
15Hakuna kitu kilichoko nje ya mtu kinachoweza kumtia uchafu kikiingia ndani yake; ila yanayomtoka mtu ndiyo yanayomtia uchafu.[#Tume. 10:14-15.]
16Kama yuko mwenye masikio yanayosikia na asikie!
17Kisha alipoondoka penye watu na kuingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza mfano ule.
18Akawaambia: Kumbe nanyi hamjaerevuka hata leo! Hamjui, kila kitu kilichoko nje kikiingia ndani ya mtu hakiwezi kumtia uchafu?
19Kwa kuwa hakimwingii moyoni, ila tumboni tu, kikatoka chooni; ndivyo, alivyotengua miiko yote ya vyakula.
20Akasema: Linalomtoka mtu hilo ndilo linalomtia mtu uchafu.
21Kwani ndani mioyoni mwa watu hutoka mawazo mabaya: ugoni, wizi, uuaji,
22uzinzi, choyo, ubaya, unyengaji, uasherati, kijicho, matusi, majivuno, upuzi.
23Mabaya haya yote hutoka ndani, tena ndiyo yanayomtia mtu uchafu.
24Alipoondoka pale, akaenda mipakani kwa Tiro, akaingia nyumbani, maana alitaka, asijulikane na mtu, lakini hakuweza kufichika.
25Kwani papo hapo mwanamke alisikia, ya kuwa yuko. Kwa kuwa na mtoto mwenye pepo mchafu akaja, akamwangukia miguuni pake;
26naye yule mwanamke alikuwa Mgriki, kabila lake ni Msirofoniki. Alipomwomba, amfukuze pepo, amtoke binti yake,
27akamwambia: Uache, kwanza watoto washibe, kwani haifai kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia vijibwa!
28Lakini akamjibu akisema: Ndio, Bwana, lakini nao vijibwa hula chini ya meza makombo ya vitoto.
29Ndipo, alipomwambia: Kwa ajili ya neno hili enenda, pepo amemtoka binti yako!
30Akaondoka, akaenda nyumbani mwake, akamkuta kitoto, amelala kitandani, naye pepo alikuwa amekwisha kumtoka.
31*Alipotoka tena mipakani kwa Tiro akapita Sidoni, akafika kwenye bahari ya Galilea katikati ya mipaka ya ile Miji Kumi.[#Mat. 15:29-31.]
32Wakamletea mtu aliyekuwa kiziwi na bubu, wakambembeleza, ambandikie mkono.[#Mar. 5:23.]
33Akamwondoa katika kundi la watu, wawe peke yao, akaweka vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi.[#Mar. 8:23.]
34Kisha akatazama juu mbinguni, akapiga kite, akamwambia: Efata! ni kwamba: Fumbuka![#Mar. 6:41; Yoh. 11:41.]
35Ndipo, masikio yake yalipofumbuka, nayo mafungo ya ulimi wake yakalegea papo hapo, akasema vema.
36Akawaagiza, wasimwambie mtu. Lakini ijapo awaagize hivyo, wale walizidi kuyatangaza po pote.[#Mar. 1:43-44.]
37Watu wakashangaa mno, wakasema: Ametenda vyote vizuri; viziwi anawafanya, wasikie, nao mabubu, waseme.*