Nehemia 12

Nehemia 12

Majina ya watambikaji na ya Walawi.

1Hawa ndio watambikaji na Walawi waliorudi milimani kwao pamoja na Zerubabeli, mwana wa Saltieli, na Yesua: Seraya, Yeremia, Ezera,[#Ezr. 2:2.]

2Amaria, Maluki, Hatusi,

3Sekania, Rehumu, Meremoti,

4Ido, Ginetoi, Abia,[#Luk. 1:5.]

5Miyamini, Madia, Bilga,

6Semaya, Yoyaribu, Yedaya,

7Salu, Amoki, Hilkia, Yedaya; hawa walikuwa wakuu wa watambikaji na wa ndugu zao katika siku za Yesua.

8Walawi walikuwa: Yesua, Binui, Kadimieli, Serebia, Yuda, Matania; yeye na ndugu zake waliongoza nyimbo za kushukuru;[#Neh. 11:17.]

9ndugu zao Bakibukia na Uni wakasimama usoni pao, wawasaidie.

10Yesua akamzaa Yoyakimu, Yoyakimu akamzaa Eliasibu, Elaisibu akamzaa Yoyada,[#Neh. 12:26; 3:1,20.]

11Yoyada akamzaa Yonatani, Yonatani akamzaa Yadua.

12Watambikaji waliokuwa wakuu wa milango wiku za Yoyakimu ndio hawa: Meraya wa mlango wa Seraya, Hanania wa mlango wa Yeremia,

13Mesulamu wa mlango wa Ezera, Yohana wa mlango wa Amaria,

14Yonatani wa mlango wa Meluki, Yosefu wa mlango wa Sebania,

15Adina wa mlango wa Harimu, Helkai wa mlango wa Merayoti,

16Zakaria wa mlango wa Ido, Mesulamu wa mlango wa Ginetoni,

17Zikiri wa mlango wa Abia, Piltai wa mlango wa Minyamini na wa Moadia,

18Samua wa mlango wa Bilga, Yonatani wa mlango wa Semaya,

19Matinai wa mlango wa Yoyaribu, Uzi wa mlango wa Yedaya,

20Kalai wa mlango wa Salai, Eberi wa mlango wa Amoki,

21Hasabia wa mlango wa Hilkia, Netaneli wa mlango wa Yedaya.

22Walawi waliokuwa wakuu wa milango waliandikwa siku za Eliasibu, Yoyada na Yohana na Yadua; lakini watambikaji waliandikwa, Mpersia Dario aliposhika ufalme.[#Neh. 12:10-11.]

23Wana wa Lawi waliokuwa wakuu wa milango waliandikwa katika kitabu cha mambo ya siku za kale kufikisha siku za Yohana, mwana wa Eliasibu.

24Nao wakuu wa Walawi ni hawa: Hasabia, Serebia na Yesua, mwana wa Kadimieli, nao ndugu zao waliosimama usoni pao, wawasaidie kuimba mashangilio ya kushukuru, kama Dawidi aliyekuwa mtu wa Mungu alivyoagiza, wapokeane zamu kwa zamu.[#1 Mambo 25; 2 Mambo 29:25.]

25Matania na Bakibukia, Obadia, Mesulamu, Talmoni na Akubu walikuwa walinda malango, wakavilinda vilimbiko vilivyomo vyumbani penye malango.[#Neh. 11:17,19; 1 Mambo 26:15,17; 2 Mambo 8:14.]

26Hawa ndio waliokuwako siku za Yoyakimu, mwana wa Yesua, mwana wa Yosadaki, na siku za mtawala nchi Nehemia na za Ezera aliyekuwa mtambikaji na mwandishi.[#Neh. 5:14; 12:10; 1 Mambo 6:14-15; Ezr. 7:1-6.]

Boma la Yerusalemu linaeuliwa.

27Walipotaka kulieua boma la Yerusalemu wakawatafuta Walawi mahali pao po pote, wawapeleke Yerusalemu kufanya mweuo na furaha kwa kushukuru na kuimbia matoazi na mapango na mazeze.

28Wakakusanyika wana wao walio waimbaji wakitoka katika nchi iliyouzunguka Yerusalemu na viwanjani kwa Netofa

29na Beti-Gilgali na mashambani kwenye Geba na Azimaweti; kwani kwenye vile viwanja ndiko, waimbaji walikojijengea kuzunguka Yerusalemu.

30Watambikaji na Walawi walipokwisha kujitakasa, wakawatakasa watu na malango na boma.

31Kisha nikawapeleka wakuu wa Yuda bomani juu, nikasimama hapo na makundi mawili makubwa ya kushukuru, moja likaenda ukutani juu kufika penye lango la Jaani.[#Neh. 2:13; 3:13.]

32Nyuma yao wakafuata Hosaya na nusu ya wakuu wa Yuda:

33Azaria, Ezera na Mesulamu,

34Yuda na Benyamini na Semaya na Yeremia.

35Nao wana wa watambikaji wengine walikuwako wenye matarumbeta: Zakaria, mwana wa Yonatani, mwana wa Semaya, mwana wa Matania, mwana wa Mikaya, mwana wa Zakuri, mwana wa Asafu,

36na ndugu zake: Semaya na Azareli, Milalai, Gilalai, Maai, Netaneli na Yuda na Hanani wakishika vyombo vya kuimbia vya Dawidi aliyekuwa mtu wa Mungu, naye mwandishi Ezera akawatangulia.

37Wakaja kulifikia lango la Jicho la Maji, wakaenda moja kwa moja wakaipanda ngazi ya mji wa Dawidi, wakaendelea kupanda, hata wakafika ukutani juu penye nyumba ya Dawidi mpaka kwenye lango la Maji lililoko upande wa maawioni kwa jua.[#Neh. 3:26.]

38Lakini kundi la pili la kushukuru likashika njia ya upande mwingine, nami nikawafuata na nusu ya watu, tukienda ukutani juu, tukaupita mnara wa Tanuru, tukaufikia ukuta mpana,

39kisha tukapita juu penye lango la Efuraimu vilevile penye lango la Mji wa Kale na penye lango la Samaki, tukaupita mnara wa Hananeli na mnara wa Mea, tukalifikia lango la Kondoo, wakasimama penye lango la Kifungoni.

40Kisha makundi yote mawili ya kushukuru wakajisimamisha penye Nyumba ya Mungu pamoja na mimi na nusu ya watawalaji.

41Ndipo, yalipolia matarumbeta ya watambikaji Eliakimu, Masea, Minyamini, Mikaya, Eliyoenai, Zakaria na Hanania.

42Nao Masea na Semaya na Elazari na Uzi na Yohana na Malkia na Elamu na Ezeri waliokuwa waimbaji wakaimba wakiongozwa na Iziraya.

43Kisha siku hiyo wakatoa ng'ombe nyingi za tambiko, wakafurahi, kwa kuwa Mungu amewafurahisha na kuwapatia furaha kubwa, hata wanawake na watoto wakafurahi, mashangilio ya furaha hiyo ya Yerusalemu yakasikilika hata mbali.

Kuweka wasimamizi wa vipaji, Nyumba ya Mungu ilivyotolewa.

44Siku hiyo wakawekwa watu wa kuviangalia vyumba vya vilimbiko na michango na malimbuko na mafungu ya kumi, wayakusanye mashambani kwenye miji yote, watu waliyoagizwa na Maonyo kuwatolea watambikaji na Walawi, kisha wayaweke humo, kwani Wayuda waliwafurahia watambikaji na Walawi kwamba: Wanasimama kazini.[#Neh. 10:36; 13:5.]

45Nao wakalinda ulinzi wa Mungu wao na ulinzi wa matakaso, nao waimbaji na walinda malango wakazishika zamu zao, kama Dawidi na mwanawe Salomo walivyoviagiza.

46Kwani nazo hizo siku za kale za Dawidi na za Asafu walikuwako wakuu wa waimbaji na nyimbo za kumshangilia na za kumshukuru Mungu.[#1 Mambo 25.]

47Siku za Zerubabeli na za Nehemia Waisiraeli wote walitoa mafungufungu ya kuwapa waimbaji na walinda malango siku kwa siku yaliyowapasa. Hivyo vipaji wakavitakasa, kisha wakawapa Walawi, nao Walawi walipokwisha kuvitakasa wakatoa humo vya kuwapa wana wa Haroni.[#Neh. 10:38.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania