The chat will start when you send the first message.
1Ikawa, boma lilipokwisha kujengwa, nikatia milango, wakawekwa walinda malango na waimbaji na Walawi,
2nikamwagiza ndugu yangu Hanani na Hanania, mkuu wa boma, kushika amri humu Yerusalemu, kwani huyu alikuwa mtu mwelekevu mwenye kumcha Mungu kuliko wengine wengi.
3Nikawaambia: Malango ya Yerusalemu yasifunguliwe, mpaka jua liwake na nguvu; tena walinzi wakingali wanasimama, malango yafungwe na kutiwa makomeo. Tena mweke wenyeji wa Yerusalemu kuwa walinzi kila mtu na zamu yake ya kulinda hapo panapoielekea nyumba yake.
4Lakini mji ulikuwa mpana pande zote na mkubwa, lakini watu waliomo walikuwa wachache, hata nyumba mpya hazikujengwa.
5Mungu akanitia moyoni, niwakusanye wakuu wa miji na watawalaji nao watu, waandikwe milango yao. Nikaona chuo kilichoandikwa udugu wao walionza kurudi na kupanda huku, nikaona yameandikwa haya:
(6-73: Ezr. 2.)6Hawa ndio watu waliokaa majimboni waliporudi kutoka mafungoni kwenye kutekwa; ndio wao, Nebukadinesari, mfalme wa Babeli, aliowateka na kuwahamisha, nao wakapata kurudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake.
7Walikuja pamoja nao Zerubabeli, Yesua, Nahemia, Azaria, Ramia, Nehamani, Mordekai, Bilsani, Misipereti, Bigwai, Nehumu na Baana. Hesabu ya waume wa Waisiraeli ni hii:
8Wana wa Parosi 2172;
9wana wa Sefatia 372;
10wana wa Ara 652;
11wana wa Pahati-Moabu, ndio wana wa Yesua na wa Yoabu, 2818;
12wana wa Elamu 1254;
13wana wa Zatu 845;
14wana za Zakai 760;
15wana wa Binui 648;
16wana wa Bebai 628;
17wana wa Azgadi 2322;
18wana wa Adonikamu 667;
19wana wa Bigwai 2067;
20wana wa Adini 655;
21wana wa Ateri walio wa Hizikia 98;
22wana wa Hasumu 328;
23wana wa Besai 324;
24wana wa Harifu 112;
25wana wa Gibeoni 95;
26waume wa Beti-Lehemu na wa Netofa 188;
27waume wa Anatoti 128;
28waume wa Beti-Azimaweti 42;
29waume wa Kiriati-Yearimu, wa Kefira na wa Beroti 743;
30waume wa Rama na wa Geba 621;
31waume wa Mikimasi 122;
32waume wa Beteli na wa Ai 123;
33waume wa Nebo wa pili 52;
34wana wa Elamu wa pili 1254;
35wana wa Harimu 320;
36wana wa Yeriko 345;
37wana wa Lodi, wa Hadidi na wa Ono 721;
38wana wa Senaa 3930.
39Watambikaji walikuwa hawa: wana wa Yedaya wa mlango wa Yesua 973;
40wana wa Imeri 1052;
41wana wa Pashuri 1247;
42wana wa Harimu 1017.
43Walawi walikuwa hawa: wana wa Yesua wa mlango wa Kadimieli na wana wa Hodawia 74.
44Waimbaji walikuwa wana wa Asafu 148.
45Walinda malango walikuwa wana wa Salumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni, wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Sobai, watu 138.
46Watumishi wa Nyumbani mwa Mungu walikuwa hawa: wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaoti,
47wana wa Kerosi, wana wa Sia, wana wa Padoni,
48wana wa Lebana, wana wa Hagada, wana wa Salmai,
49wana wa Hanani, wana wa Gideli, wana wa Gahari,
50wana wa Raya, wana wa Resini, wana wa Nekoda,
51wana wa Gazamu, wana wa Uza, wana wa Pasea;
52wana wa Besai, wana wa Munimu, wana wa Nefisisimu,
53wana wa Bakibuki, wana wa Hakufa, wana wa Harihuri;
54wana wa Basiliti, wana wa Mehida, wana wa Harsa;
55wana wa Barkosi; wana wa Sisera, wana wa Tema;
56wana wa Nesia, wana wa Hatifa.
57Wana wa watumwa wa Salomo walikuwa hawa: wana wa Sotai, wana wa Sofereti, wana wa Perida,
58wana wa Yala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli,
59wana wa Sefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokereti-Hasebaimu, wana wa Amoni.
60Watumishi wa Nyumbani mwa Mungu na wana wa watumwa wake Salomo wote pamoja walikuwa 392.
61Nao hawa ndio waliopanda toka Teli-Mela, Teli-Harsa, Kerubu-Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuijulisha milango ya baba zao, wala vizazi vyao, kama ndio Waisiraeli:
62wana wa Delaya, wana wa Tobia, wana wa Nekoda; nao walikuwa watu 642.
63Tena kwao watambikaji: wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai aliyechukua mmoja wao binti Barzilai wa Gileadi, awe mkewe, kwa hiyo aliitwa kwa jina lao.
64Hawa walikitafuta kitabu chao cha udugu wao, lakini hawakukiona, kwa hiyo wakakatazwa utambikaji.
65Mtawala nchi akawaambia: Msile kabisa vyakula vitokavyo Patakatifu Penyewe, mpaka atakapoondokea mtambikaji mwenye Urimu na Tumimu (Mwanga na Kweli).[#2 Mose 28:30.]
66Huo mkutano wote pamoja walikuwa watu 42360,
67pasipo watumwa na vijakazi wao, nao walikuwa 7337; tena walikuwako waimbaji wa kiume na wa kike 245.
68Farasi wao walikuwa 736, nyumbu wao 245,
69ngamia 435, tena punda 6720.
70Wakuu wengine wa milango wakatoa vipaji vya kufanyia hizo kazi za jengo: mtawala nchi alitoa na kutia katika kilimbiko: vipande vya dhahabu vilivyoitwa Dariko 1000, ndio shilingi kama 40000, na vyano 50 na mavazi ya watambikaji 530.[#Neh. 7:65.]
71Nao wakuu wa milango wengine wakatoa na kutia katika kilimbiko cha jengo: vipande vya dhahabu vilivoitwa Dariko 20000, ndio shilingi kama 800000, na vipande vya fedha vilivyoitwa Mane 2200, ndio shilingi kama 440000.
72Nao watu wengine wakatoa Dariko za dhahabu 20000, ndio shilingi kama 800000, na Mane za fedha 2000, ndio shilingi kama 400000 na mavazi ya watambikaji 67.
73Kisha watambikaji na Walawi na walinda malango na waimbaji nao watu wengine na watumishi wa Nyumbani mwa Mungu nao Waisiraeli wote wakakaa katika miji yao. Mwezi wa saba ulipofika, wana wa Isiraeli walikuwamo bado mijini mwao.