4 Mose 21

4 Mose 21

Kumshinda mfalme wa Aradi.

1Mfalme wa Kikanaani wa Aradi aliyekaa upande wa kusini aliposikia, ya kuwa Waisiraeli wanakuja wakiifuata njia ya wapelelezi, akapigana nao Waisiraeli, akateka wengine wa kwao.

2Ndipo, Waisiraeli walipomwapia Bwana kiapo cha kwamba: Ukiwatia watu hawa mikononi mwetu, tutaiangamiza miji yao kwa kuitia mwiko wa kuwapo.[#5 Mose 13:15; Yos. 6:17; Amu. 1:17; 1 Sam. 15:3.]

3Bwana akazisikia sauti zao Waisiraeli, akawapa hao Wakanaani, nao wakawaangamiza wao pamoja na miji yao kwa kuitia mwiko wa kuwapo; kwa hiyo wakapaita mahali pale Horma (Mwiko).[#4 Mose 14:45.]

Nyoka ya shaba.

4Kisha wakaondoka kwenye mlima wa Hori wakishika njia ya kwenda kwenye Bahari Nyekundu, waizunguke nchi ya Edomu. Watu walipotaka kuzimia roho kwa kuchoka njiani,

5wakamgombeza Mungu, hata Mose kwamba: Kwa nini mlitutoa Misri, tujifie huku nyikani? Kwani hakuna chakula wala maji, nazo roho zetu zinachukizwa na chakula hiki kikosacho nguvu.

6Ndipo, Bwana alipotuma nyoka za moto kuwajia hao watu; nao walipowauma watu, wakafa watu wengi kwao Waisiraeli.[#1 Kor. 10:9.]

7Ndipo, watu walipomjia Mose, wakasema: Tumekosa tulipomgombeza Bwana, hata wewe. Tuombee kwake Bwana, awaondoe hawa nyoka kwetu! Mose alipowaombea hao watu,

8Bwana akamwambia Mose: Jitengenezee nyoka ya moto, uitungike kuwa kielekezo! Itakuwa, kila aliyeumwa na nyoka atakapoitazama atapona.[#Yoh. 3:14.]

9Mose akatengeneza nyoka ya shaba nyekundu, akaitungika kuwa kielekezo, ikawa hivyo: nyoka alipomwuma mtu, naye akaitazama hiyo nyoka ya shaba, akapona.

Makambi ya Waisiraeli.

Waisiraeli walipoondoka huko, wakapiga makambi Oboti.

10Walipoondoka Oboti wakapiga makambi Iye-Abarimu katika nyika inayoelekea Moabu upande wa maawioni kwa jua.

11Walipoondoka huko, wakapiga makambi kwenye kijito cha Zeredi.[#4 Mose 33:43-49.]

12Walipoondoka huko, wakapiga makambi kwenye kijito cha Zeredi.

13Walipoondoka huko wakapiga makambi ng'ambo ya huko ya Arnoni ulioko nyikani, utokao mipakani kwa Waamori, kwani Arnoni ulikuwa mpaka wa Wamoabu kuwatenga Wamoabu na Waamori.

14Kwa hiyo inasemwa katika kitabu cha vita vya Bwana:[#Yos. 10:13.]

15Bonde la Sufa na vijito vya Arnoni,

napo vijito vinaposhukia,

panapopafikia napo mahali penye mji wa Ari

ndipo panapouegemea mpaka wa Moabu.

16Toka hapo wkafika Kisimani;

ndiko kwenye kile kisima, Bwana

alikomwambia Mose kwamba: Wakusanye watu, niwape maji!

17siku zile Waisiraeli waliuimba wimbo huu:

18Bubujika, kisima! Haya! Kiimbieni!

Waliokichimba kisima hiki ndio wakuu;

kweli majumbe wa watu ndio waliokifukua.

kwa kutumia bakora na fimbo zao za kifalme.

Toka huko nyikani wakaenda Matana.

19Toka Matana wakaenda Nahalieli, toka Nahalieli wakaenda Bamoti,

20toka Bamoti wakaenda bondeni kwenye mbuga za Moabu zilizoko kwenye mlima na Pisiga uelekeao jangwani.

Kumshinda Sihoni.

21Waisiraeli wakatuma wajumbe kwa Sihoni, mfalme wa Waamori, kwamba:[#5 Mose 2:26-37.]

22Tunataka kupita katika nchi yako; hatutaondoka njiani kuingia mashambani au mizabibuni, wala hatutakunywa maji ya visimani, ila tunataka kuishika njia ya mfalme tu, hata tuupite mpaka wako mwingine.[#4 Mose 20:17.]

23Lakini Sihoni hakuwapa wana wa Isiraeli ruhusa kupita mipakani kwake, ila Sihoni akawakusanya watu wake wote, akatoka kwenda nyikani kuwazuia Waisiraeli. Alipofika Yasa akapigana nao Waisiraeli.

24lakini Waisiraeli wakampiga kwa ukali wa panga, wakaichukua nchi yake toka mto wa Arnoni mpaka mto wa Yakobo, wana wa Amoni walikokaa, kwani mipaka yao wana wa Amoni ilikuwa yenye nguvu.

25Waisiraeli wakaiteka hiyo miji yote, kisha Waisiraeli wakakaa katika miji yote ya Waamori, namo Hesiboni na katika mitaa yake yote.

26Kwani Hesiboni ulikuwa mji wa Sihoni, mfalme wa Waamori; naye aliupigania kale na mfalme wa Moabu, ndipo, alipoichukua hiyo nchi yake na kuitoa mkononi mwake mpaka mto wa Arnoni.

27Kwa hiyo wenye kutunga mafumbo walisema:

Njoni Hesiboni, mji wa Sihoni ujengwe na kutiwa nguvu!

28Kwani moto umetoka Hesiboni,

miali ya moto imetoka mjini mwa Sihoni,

ikaula mji wa Ari wa Moabu nao wenyeji wa vilimani

kwa Arnoni.

29Umepatwa na mambo, wewe Moabu!

Mmeangamia ninyi, watu wa Kemosi!

Wamewakimbiza wana wenu wa kiume,

nao wana wenu wa kike wamempa Sihoni, mfalme wa Waamori!

30Tulipowapiga mishale, ndipo, Hesiboni ulipoangamia mpaka Diboni, tukaiharibu nchi mpaka Nofa, tukafika hata Medeba.

31ndipo, Waisiraeli walipokaa katika nchi ya Waamori.

Kumshinda Ogi.

32Kisha Mose akatuma watu kwenda Yazeri kupeleleza, nao wakaiteka mitaa yake na kuwafukuza Waamori waliokuwamo.

33Kisha wakageuka, wakaishika njia ya kupanda Basani. Lakini Ogi, mfalme wa Basani, akatoka kuwazuia, yeye na watu wake wote, wakapigana huko Edirei.[#5 Mose 3:1-11.]

34Bwana akamwambia Mose: Usimwogope, kwani nimemtia mkononi mwako pamoja na watu wake wote, hata nchi yake, umfanyizie, kama ulivyomfanyizia Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekaa Hesiboni.[#Sh. 136:17,22.]

35ndipo, walipompiga yeye na wanawe na watu wake wote, wasisaze kwake hata mmoja aliyeweza kukimbia, kisha wakaitwaa nchi yake.

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania