The chat will start when you send the first message.
1Ndivyo, Bwana Mungu anavyosema kwa ajili ya Edomu:
Tumesikia mbiu kwake Bwana,
ya kuwa mjumbe ametumwa kwenda kwa mataifa kwamba:
Ondokeni! Na tuondoke kwenda kupigana naye!
2Utaniona, nikikufanya kuwa mdogo katika mataifa,
ubezwe kabisa wewe!
3Majivuno ya moyo wako yamekudanganya
ukaaye nyufani kwenye miamba katika makao yaliyoko huko
juu,
ukasema moyoni mwako: Yuko nani atakayenibwaga chini?
4Lakini ijapo uvijenge vituo vyako juu kabisa kama tai,
ijapo utue katikati ya nyota,
huko nako nitakubwaga chini; ndivyo, asemavyo Bwana.
5Kama wezi wangekujia,
au kama waangamizaji wangekujia usiku,
wasingeiba tu, mpaka wakitoshewa?
Lakini nawe ungekuwa umeangamizwa kabisa.
Kama wachuma zabibu wangekujia,
6Lakini tazameni, mali za Esau zilivyotafutwa zote,
malimbiko yake nayo yalivyochunguzwa!
7Wote, uliofanya maagano nao, wamekukimbiza hata mipakani;
wote, uliopatana nao, wamekudanganya, wakakushinda,
waliokula chakula chako wamekutegea matanzi chini,
lakini mwenyewe huyatambui maana.
8Ndivyo, asemavyo Bwana:
Siku hiyo, nitakapowapoteza werevu wa kweli kwake Edomu,
sipo, utambuzi nao utakapopotea milimani kwa Esau?
9Ndipo, mafundi wenu wa vita, ninyi Watemani,
watakapokata tamaa,
kusudi kila mmoja ang'olewe milimani kwa Esau kwa kuuawa.
10Kwa hivyo, ulivyomkorofisha ndugu yako Yakobo,
soni zitakufunika, mpaka uangamie kale na kale.
11Kwani walisimama upande mwingine siku ile,
wengine walipoziteka mali zake,
wageni walipoingia malangoni mwake na kuupigia Yerusalemu
kura,
ndipo, wewe nawe ulipokuwa kama mwenzao wao hao.
12Lakini usimwonee ndugu yako, akipatwa na siku mbaya,
siku ikiwa ya kuona mambo mageni!
Wala usiwafurahie wana wa Yuda siku, wakiangamia!
Wala usiwe na madomo makubwa siku, wakisongeka!
13Wala usiingie malangoni mwao walio ukoo wangu siku,
wakiteseka!
Wala usiwaonee nawe, wakipatwa na mabaya siku,
wakiteseka!
Wala usiinyoshe mikono yako kukamata mali zao siku,
wakiteseka!
14Wala usisimame penye njia panda kuwaua watu wao
waliokimbia!
Wala masao yao usiwatie mikononi mwa adui siku,
wakisongeka!
15Kwani siku ya Bwana iko karibu, iwajie wao wa mataifa
yote;
ndipo, utakapofanyiziwa, kama ulivyofanya,
matendo yako yakikurudia kichwani pako.
16Kwani kama ulivyokunywa katika mlima wangu mtakatifu,
ndivyo, mataifa yote watakavyokunywa pasipo kukoma,
watakunywa na kumeza vibaya, wawe kama watu wasiokuwapo
kabisa.
17Lakini mlimani pa Sioni watakuwapo waliojiponya, napo
patakuwa Patakatifu.
18Nao walio mlango wa Yakobo watakuwa moto,
nao walio mlango wa Yosefu watakuwa miali ya moto,
lakini walio wa mlango wa Esau watakuwa majani makavu,
ndiyo watakayoyawasha na kuyala.
Kwa hiyo hawatakuwapo walio masao ya Esau, kwani Bwana
ameyasema.
19Nao wakaao upande wa kusini wataitwaa milima ya Esau,
nao wakaao mrimani wataitwaa nchi ya Wafilisti,
nayo mashamba ya Efuraimu nayo mashamba ya Samaria
watayatwaa,
nao Wabenyamini watatwaa Gileadi.
20Navyo vikosi vya wana wa Isiraeli waliotekwa na
kuhamishwa
ndio watakaoitwaa nchi ya Kanaani mpaka Sareputa,
nao Wayerusalemu waliotekwa na kuhamishwa Sefaradi
wataitwaa miji iliyoko upande wa kusini.
21Kisha waokozi wataupanda mlima wa Sioni,
waipatilize milima ya Esau;
lakini ufalme utakuwa wake Bwana.