Mashangilio 1

Mashangilio 1

Kitabu cha kwanza.

Wamchao Mungu hufanikiwa, wasiomcha hupotea.

1*Mwenye shangwe ni mtu asiyefuata shauri lao wasiomcha Mungu, asiyesimama njiani kwao wakosaji, asiyekaa penye kao la wafyozaji.[#Sh. 26:4; 119:1; Fano. 4:14; Yer. 15:17.]

2Ila hupendezwa na Maonyo yake Bwana, hayo Maonyo yake ndiyo, ayawazayo mchana na usiku.[#Sh. 119:35,47,70,97; Yos. 1:8; 5 Mose 6:7.]

3Kwa hiyo atakuwa kama mti uliopandwa penye vijito, uzaao matunda yake, siku zinapotimia, nayo majani yake hayanyauki; yote ayafanyayo hufanikiwa.[#Sh. 92:13-15; Yer. 17:8.]

4Lakini wasiomcha Mungu sivyo walivyo, wao hufanana na makapi, upepo uyapeperushayo.[#Sh. 35:5; Iy. 21:18; Hos. 13:3.]

5Kwa hiyo wasiomcha Mungu hawataopolewa kwenye mapatilizo, wala wakosaji kwenye mkutano wao waongofu.

6Kwani Bwana huijua njia yao walio waongofu, lakini njia yao wasiomcha Mungu itapotea.*

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania