Mashangilio 100

Mashangilio 100

Kumshukuru Mungu na kupaingia Patakatifu pake.

1Mpigieni Bwana shangwe, nchi zote! Mtumikieni Bwana na kufurahi!

2Tokeeni mbele yake na kupiga shangwe!

3Tambueni, ya kuwa aliye Mungu ndiye yeye Bwana! Yeye ndiye aliyetufanya, sio sisi wenyewe, tu watu wa ukoo wake na kondoo wa malishoni pake.[#Sh. 95:7.]

4Ingieni milangoni mwake na kumshukuru! Ziingieni nyua zake na kumshangilia! Mshukuruni! Nalo Jina lake likuzeni sana!

5Kwani Bwana ni mwema, nao upole wake ni wa kale na kale, nao welekevu wake ni wa vizazi na vizazi.[#Sh. 106:1.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania